Jamaa Anayekula Nyama za Maiti Azua Kizaa zaa Indonesia

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
2576774.jpg

Sumanto alipofikishwa mahakamani mwaka 2003 kwa kuchimbua maiti kaburini na kuila Tuesday, July 21, 2009 8:53 AM
Jamaa mmoja wa nchini Indonesia ambaye anapenda sana nyama kiasi cha kwamba alifukua maiti ya mwanamke mmoja kutoka kaburini na kuipika na kuila. Hivi sasa wanakijiji wanamwogopa na hawataki arudi kijijini kwao. "Nyama yake ilikuwa tamu sana " alisema mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Sumanto akiwa chumbani kwake kwenye kituo cha kiislamu cha kurekebisha tabia cha watu wenye matatizo ya akili kilichopo kwenye mji wa Java.

"Napenda nyama za aina zote ilimradi iwe imepikwa." alisema Sumanto na kuongeza "Nimeacha kula nyama za watu, siku hizi nakula spinach".

Katika nchi nyingi mtu kama huyu mkulima mwenye umri wa miaka 37 kutoka kijiji cha Palumutan angepewa tiba ya kisaikolojia akiwa kwenye sehemu yenye ulinzi.

Hali ilikuwa tofauti nchini Indonesia kwani alitupwa jela miaka mitano kwa tuhuma za wizi wa maiti na kusababisha mvurugano kwenye jamii. Alichiwa huru baada ya hukumu yake kuisha na kuruhusiwa kurudi kijijini mwake bila kufuatiliwa nyenendo zake.

Majirani zake walishtushwa na kumuogopa walipomuona tena na walikataa kata kata kuishi naye na kusababisha taasisi hiyo ya kiislamu kumchukua na kumweka kwenye kituo chao cha kusaidia watu wanaonekana kuwa na matatizo ya akili wakipewa miongozo bora ya maisha.

"Hakuna mtu aliyetaka kumsogelea, wanakijiji wote walikuwa wakimuogopa sana wakimwita "Mla Nyama za Watu" alisema mkurugenzi wa kituo cha taasisi hiyo, Supono Mustajab.

Wafanyakazi katika taasisi ya kidini ambayo Sumanto aliwekwa baada ya kutoka jela na kufukuzwa kijijini kwake walisema kuwa Sumanto alikuwa ni mtu mwenye vurugu na alionekana kukata tamaa alipotoka jela mwaka 2006.

"Maisha ya jela hayakuwa mazuri kwake kwani alikuwa hali wala kunywa chochote, alikuwa mwenye hasira sana. Ilitibidi tukilinde chumba chake usiku na mchana ili asiwafanyie vurugu wengine" alisema Mustajab.

Kama wenzake kwenye kituo hiki ambao wamekata tamaa ya maisha, alifunzwa kusoma Koran na kuhimizwa kushiriki kwenye michezo, kilimo na uvuvi ili kuondoa sress zake"

"Hivi sasa hali yake imekuwa nzuri sana" alisema Mustajab kuongeza kuwa anawalipia pango la nyumba watu masikini kama Sumanto kwani na wao ni binadamu.

Hali kwenye kijiji chake haijabadilika kwani wakazi wa kijiji cha Palumutan bado wanamzungumzia mtu ambaye alikuwa akiogopwa kwa kula nyama za paka, mijusi na mende.

Jirani wa Sumanto mwenye umri wa miaka 43 aliyejulikana kwa jina la Ngadiah, alisema kuwa hatakaa akasahau harufu ya kifo aliyokuwa akiinusa wakati Sumanto alipokuwa akinywa supu ya nyama ya binadamu kwenye bakuli.

"Unamzungumzia Sumanto?, yule mlaji nyama za maiti? alikuwa ni mtu mwenye hasira ambaye alikuwa akituibia mara kwa mara kuku wetu na mchele" alisema jirani huyo.

"Vurugu kubwa itazuka hapa kijijini kama atarudi tena. Sitaki arudi aje aniue halafu anifanye chakula chake cha jioni".

Familia ya Sumanto ilibidi wahamie nje kidogo ya kijiji kuwakimbia wanakijiji waliokuwa wakiwatolea macho muda wote.

Baba yake Sumanto mwenye umri wa miaka 65 alielezea kummiss mwanae ingawa hawezi kumchukua na kukaa naye.

"Pamoja na ubaya wake, yule ni mwanangu na ningependa nimchukue lakini majiani watamsumbua na watamfukuza nje ya kijiji, sijui nitafanyaje" alisema baba yake.

Mustajab alisema kuwa Sumanto alikuwa tayari kurejea kwao lakini msimamizi wa kituo hicho alifikiria tofauti.

"Katika mlo wake mmoja, Sumanto atamaliza sahani mbili kubwa za wali, mishikaki 60 na vipande 16 vikubwa vya nyama pamoja na vipande nane vya nyama ya kuku" alisema msimamizi huyo na kuongeza "Hivi anavipata hapa kirahisi itakuwaje akirudi huko kijijini hawezi kula kama hivi kutokana na kipato chake kidogo, nina wasiwasi atarudia kula nyama za maiti".

Hata hivyo Sumanto anakanusha madai hayo na kudai akizidiwa ataganga njaa na maji na vidonge vya vitamin.

"Nyama ni bora kuliko mboga za majani, lakini kama nikikosa nyama nitakula majani kwani yanaleta afya zaidi, nitayakaanga kuyafanya yawe na ladha nzuri" alisema.

Sumanto alidai kuwa siku hizi amekuwa mtu mwenye upendo zaidi na anajiona mwenye uhuru zaidi.

"Nasikitika watu wamesema maneno mengi mabaya juu yangu, nitajitahidi kuhakikisha kuwa wanakijiji wananifungulia tena mioyo yao na kunikubali tena" alimalizia Sumanto.
http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2576774&&Cat=7
 
Lakini picha siyo yake. Nahisi ni picha ya mmoja wa watuhumiwa wa mabomu ya Bali, Indonesia wakati wa trial.
 
Back
Top Bottom