de'levis
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 1,222
- 1,567
Nimemwona nikajiuliza kama magamba nao wamesikiliza. Maana tukisema sisi tunaambiwa ni cdm! Kwani cdm si watu.
Wote tunakumbuka udikteta wa ma dc na ma rc. Tuliona walimu wakichapwa viboko. Tunaona rc Arusha akilazimisha bendera za cdm zishushwe kwenye matawi ya chama huko Arumeru! Tumemsikia Mbunge akilalamika dc kuingia kwenye boma na kuchukua mbuzi na ng'ombe kama wake. Huu udikteta unalindwa na katiba. Halafu tunaletewa mswada unaomwongezea rais udikteta! Tukikataa kuujadili, bunge linageuka "lango la jiji"
Acha watutukane wanavyotaka, watudharau, watudhalilishe, lakini hoja ya msingi inabaki palepale, Hatuutaki huo mswada!
we waache waendelee kuchanja chale kwenye kidonda kibichi....wanadhani sisi ni wajinga sana na watu wa kuburuzwa tu...tutawaonyesha waa wasidhani wanalofanya ni sahihi