Jaji Mkuu: Mahakimu acheni kuahirisha kesi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
Mohamed Chande(1).jpg

Jaji Mkuu Othman Chande


Jaji Mkuu Othman Chande, ameiomba serikali kuboresha majengo ya Mahakam yaliyochakaa na amewataka mahakimu kuacha tabia ya kuahirisha kesi bila sababu za msingi hali ambayo inaleta usumbufu mkubwa kwa watu wanaokwenda kutafuta haki mahakamani.

Aidha ameiomba serikali kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya kuendesha shughuli za kimahakama ili ziweze kusaidia katika upatikanaji wa vitendea kazi na changamoto zingine zinazozikabili mahakama nchini.

Akifungua Mkutano wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) jijini hapa jana, Jaji Mkuu Chande alisema kwa upande wa mahakama baadhi ya mahakimu wamekuwa wakiahirisha kesi bila sababu za msingi.

Kwa upande wa mawakili amewasa kutojali zaidi maslahi yao katika utendaji wa kazi bali mewataka kuacha kujali maslahi yao zaidi kwa kuwatoza fedha nyingi wateja wao, bali wazingatie kutetea haki zao mahakamani.

Alisema kwa kufanya hivyo, kunaleta malalamiko kati ya mtuhumiwa aliyefungua kesi na kwa yule ambaye amefunguliwa kesi hali ambayo inapelekea baadhi yao kukosa imani kwa mahakama.

Kuhusu mawakili alisema wakiwa maafisa wa mahakama, si busara kwao kujali zaidi fedha suala ambalo linaafanya wengi kukosa huduma ya kutetewa na kupata haki zao mahakamani.

Aliongeza kuwa baadhi ya wananchi hawana uwezo wa kawaida kupata mawakili wa kuwatetea kutokana na fedha lakini kisheria inatakiwa mawakili kujitolea kuwasaidia washtakiwa kwenye kesi zao hivyo kuweni na moyo wa huruma na si kuangalia maslahi yenu binafsi.

Naye Rais wa TLS, Francis Stolla, aliiomba serikali kutenga fedha kwa wakato za mashauri ya kesi za uchaguzi na yale ya dharura ili kesi hizo ziweze kuamuliwa kwa wakati badala ya kupoteza muda.

Pia alisema wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maktaba, vitabu vya sheria pamoja na tatizo la russhwa kwa baadhi ya wanasheria ambao wanatia doa taaluma hiyo na kusisitiza kuwa taaluma hiyo ni muhimu katika kusaidia jamii mbalimbali.

CHANZO: NIPASHE

 
Back
Top Bottom