Jaji Mkuu amkemea Rais na kumuonya kutoingilia uhuru na utendaji wa Mahakama!

Kumekucha !
Hapa kwetu bado. Licha ya kwamba mchakato wa kumtumbua jaji mkuu ni mgumu sana, judge mkuu hana ujasiri wa kumkemea Rais. Rais huwa mara nyingi anaisema mahakama (mhimili unaojitegemea na unaopaswa kuwa huru); hakuna judge aliyewahi kumkemea Rais wetu. Woga ni hisia mbaya kuliko zote!
 
Naam, ni kweli. Jaji Mkuu hakuweza kuendelea kuvumilia tuhuma zinazotolewa na Rais wa nchi dhidi ya majaji akihoji hukumu zinazotolewa katika kesi zinazofunguliwa dhidi yake. Kila mara Rais huyo amekuwa akiziponda hukumu hizo akidai zinatolewa na majaji walioteuliwa na Rais waliomtangulia ambao walikuwa na misimamo tofauti katika kutekeleza majukumu yao.

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni wapi anapata ujeuri wa kuingilia uhuru wa mahakama ambayo ni mhimili huru na kuhusisha hukumu zinazotolewa akihoji itikadi na uzalendo wa majaji hao. Jaji Mkuu amemtahadharisha Rais kwamba majaji wanatimiza majukumu yao kulingana na Katiba ya nchi inayolinda uhuru wa mhimili huo na kumtaka Rais azingatie hilo.

Kwa habari kamili bonyeza hapa: Chief Justice Roberts rebukes President Trump
nikajua bongo kumbe umekurupuka
 
Nikajiuliza "Ni huyu huyu Ibrahim" "Profesa" wa kitanzania?
 
Kwa kuwa ni US, sina hata interest ya kusoma kwani ni kawaida huko kuwa hivyo, in short, that's not a news.
 
Naam, ni kweli. Jaji Mkuu hakuweza kuendelea kuvumilia tuhuma zinazotolewa na Rais wa nchi dhidi ya majaji akihoji hukumu zinazotolewa katika kesi zinazofunguliwa dhidi yake. Kila mara Rais huyo amekuwa akiziponda hukumu hizo akidai zinatolewa na majaji walioteuliwa na Rais waliomtangulia ambao walikuwa na misimamo tofauti katika kutekeleza majukumu yao.

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni wapi anapata ujeuri wa kuingilia uhuru wa mahakama ambayo ni mhimili huru na kuhusisha hukumu zinazotolewa akihoji itikadi na uzalendo wa majaji hao. Jaji Mkuu amemtahadharisha Rais kwamba majaji wanatimiza majukumu yao kulingana na Katiba ya nchi inayolinda uhuru wa mhimili huo na kumtaka Rais azingatie hilo.

Kwa habari kamili bonyeza hapa: Chief Justice Roberts rebukes President Trump
Nimekuja mbio nikidhani ni Tanzania, kumbe huko kwa wastaarabu ,mbona huko ni kawaida yao kabisa mkuu.
 
Naam, ni kweli. Jaji Mkuu hakuweza kuendelea kuvumilia tuhuma zinazotolewa na Rais wa nchi dhidi ya majaji akihoji hukumu zinazotolewa katika kesi zinazofunguliwa dhidi yake. Kila mara Rais huyo amekuwa akiziponda hukumu hizo akidai zinatolewa na majaji walioteuliwa na Rais waliomtangulia ambao walikuwa na misimamo tofauti katika kutekeleza majukumu yao.

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni wapi anapata ujeuri wa kuingilia uhuru wa mahakama ambayo ni mhimili huru na kuhusisha hukumu zinazotolewa akihoji itikadi na uzalendo wa majaji hao. Jaji Mkuu amemtahadharisha Rais kwamba majaji wanatimiza majukumu yao kulingana na Katiba ya nchi inayolinda uhuru wa mhimili huo na kumtaka Rais azingatie hilo.

Kwa habari kamili bonyeza hapa: Chief Justice Roberts rebukes President Trump

Kule kwetu jaji mkuu anaitwa Cheaf Nanga.
 
Back
Top Bottom