Jaji Mihayo azungumza kuhusu Twiga Cement kununua hisa za Tanga Cement, akemea uvunjaji wa sheria

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Oct 4, 2022
1,179
2,283
HATIMAYE Jaji Mstaafu Thomas Mihayo ameamua kuvunja ukimya kwa kueleza kuwa wanasheria waliipotosha Serikali na Mawaziri kuhusu kuendelea na mchakato wa kampuni ya Saruji ya Twiga kununua hisa za Tanga Cement wakati mahakama ilizuia kuwapo kwa muunganiko wa kampuni hizo.

Pia amesema tayari Baraza la Ushindani wa Biashara (FCT) lilishatoa uamuzi wa kuzuia muunganiko wa kampuni hizo baada ya wadau waliopinga suala hilo kufungua shauri na hatimaye kutolewa zuio.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Jaji Mihayo amewaambia waandishi wa habari baada ya kupitia hatua kwa hatua uamuzi wa kisheria uliotolewa, ameshangazwa na hatua ya Serikali ya kuendelea na mchakato ilhali ulishazuiwa.

Jaji Mihayo amesema Mahakama ikishaamua jambo, liwe zuri au baya, linapaswa kuheshimiwa. Kwenda kinyume cha uamuzi wa mahakama ni kuidharau mahakama. Katika suala hili la muunganiko wa Twiga na Tanga Cement mahakama ilishatoa uamuzi kwamba jambo hilo halipaswi kuendelea.

Amesisitiza kwa mantiki hiyo Serikali kupitia FCC (Tume ya Ushindani) haikupaswa kwenda kinyume bali kuheshimu. Kama ilikuwa haijaridhika, kwa mujibu wa FCA (Sheria ya Ushindani), ilipaswa kuiomba FCT kufanya marejeo ya jambo hilo badala ya kuendelea. ” Hi ni kuidharau mahakama.”

Wakati wa majumuishi ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Asharu Kijaji, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Patrobas Katambi, walisimama bungeni na kutetea uamuzi wa kuendelea na mchakato huo huku wakibainisha kwamba serikali haijavunja sharia.

Dk. Kijaji na Dk. Nchemba walisema serikali iliamua kuendelea na mchakato kwa kuwa mazingira ya awali kwa maana ya soko, yalikuwa yamebadilika na kwamba hakukua na zuio katika mchakato mpya bali ile wa kwanza.
Hata hivyo Jaji Mihayo wakati anatoa mtazamo wake binafsi kama mwanasheria nguli nchini wakati anaelezea hoja za mawaziri hao amesema hata kama mazingira yalikuwa yamebadilika suala hilo lilikuwa limezuiwa bila masharti yoyote, hivyo sheria imekikuwa na amri ya mahakama imedharauliwa.

Amesema kwamba “Kinachoonekana dhahiri hapa kutokana na kauli za mawaziri ni kwamba wanasheria katika wizara husika waliwapotosha mawaziri na serikali kwa ujumla kuhusu suala hili. Mahakama ikishatoa uamuzi na kama hakuna aliyepinga au uamuzi huo kutenguliwa unabaki kuwa sahihi. Kwa hiyo kufanya kinyume cha uamuzi au amri iliyotolewa ni kuidharau mahakama.

” Kuwapo kwa jambo kama hilo, la kutotii uamuzi au amri ya mahakama katika nchi inayofuata utawala wa sheria ni hatari kwa maslahi ya taifa na hata maendeleo kwa ujumla. Ukweli ni kwamba jambo hilo halileti picha nzuri katika utawala wa sheria, “amesema Jaji Mihayo ambaye pia alitumia nafasi hiyo kujibu maswali ya waandishi wa habari waliokuwa wanataka kufahamu vema suala la mchakato huo.

FCC ilitangaza muunganiko wa kampuni kupitia Scancem International DA ambayo ni sehemu ya Heilderberg Cement inayomiliki Twiga Cement na Tanga Cement, jambo ambalo lilipingwa na lilipingwa FCT na wadau wa saruji ambao ni kampuni ya Saruji ya Chalinze, Chama cha Kutetea Haki za Watumiaji wa Bidhaa na Peter Heller kwamba kunaweza kutokea athari katika soko la saruji.

Walisema iwapo Twiga itaruhusiwa kununua hisa za Tanga Cement, kuna uwezekano wa kuwapo na ukiritimba katika soko kwa kuwa Twiga Cement kupitia muungananiko huo, itakuwa na zaidi ya asilimia 68 katika soko. Hali hiyo, walisema inaweza kusababisha upangaji wa bei, hivyo watumiaji wa bidhaa kushindwa kumudu gharama.

FCT ilikubali maombi hayo na kutoa uamuzi kwamba mchakato huo unazuiwa, hivyo hakuna chochote kinachopaswa kuendelea lakini baadaye FCC ilitangaza upya mchakato huo na kuipa Twiga Cement nafasi ya kununua hisa kama mwekezaji ndani ya Tanga Cement.

Kutokana na hatua hiyo, wadau wanaopinga ununuzi huo, waliwasilisha maombi kutaka FCT kukazia hukumu iliyotoa juu ya katazo la kuendelea kwa mchakato huo. Wadau hao walisema kitendo cha FCC kuendelea na mchakato huo ilhali kuna zuio la kufanyika kwa jambo hilo, ni kinyume cha sheria zinazosimamia masuala ya miunganiko ya kampuni kwa kuwa suala hilo lilishasimamishwa.

Wakili Mkuu wa Kampuni ya Mawakili ya MSL Attorneys wanaowatetea wadau hao, Melkisedech Lutema, akizungumza hivi karibuni baada ya kuendelea kwa mchakato huo, alisema kitendo cha FCC kuendelea na mchakato wakati kuna uamuzi wa kisheria kuzuia suala hilo, ni ukiukwaji mkubwa wa kisheria.

“Kisheria, jambo lolote likitolewa uamuzi katika chombo chochote kilichowekwa kisheria, halipaswi kuendelea kufanyika. Na suala la muunganiko wa Twiga na Tanga Cement limezuiwa na hakuna mtu aliyepinga kwa kukata rufani au kuomba mapitio.

“Ni muhimu ikaeleweka kuwa uamuzi uwe sawa au si sawa na hakuna mtu aliyeupinga ni lazima uheshimiweKwa hiyo mtu yeyote anayeendelea anakiuka sheria na anapaswa kuchukuliwa hatua. Kwa hili tumeiomba FCT kukazia hukumu ili uvunjaji huu wa sheria usiendelee,” alisema jaji Mihayo.
 
Nchi zetu nyingi za Africa ni masikini kwa sababu ya maamuzi ya ubinafsi na kukosa uzalendo kwa baadhi ya watu waliopewa dhamana. Nchi zinanuka rushwa Kila Kona. Sasa Kwa sasa baada ya siasa kushika hatamu kumetokea ugonjwa mwingine sugu wa wateule kuwa wanafiki na kujipendekeza ili kulinda masilahi yao na wale wanaowateua. Madhara yake ndiyo km haya, kutoheshim sheria na kujali masilahi ya wengi (Wananchi).

Mbali na Tanzania kuweka utaratibu wa vijana kupitia JKT ili kujifunza uzalendo lakini wapi ni km kutwanga maji kwenye kinu. Hadi kuna kipindi Wabunge waliambiwa wahudhurie mafunzo ya JKT ili kujifunza uzalendo. Nakumbuka Ester Blaya et al walienda huko lakini wapi. Kwanza waliporudi baada ya uchaguzi wa mwaka 2020 kushindwa(kwa mjibu wa NEC) ndiyo kwanza walijichagua na kujipeleka bungeni kuapishwa bila ridhaa ya chama Chao(kwa mjibu wa viongozi wa CHADEMA). Tangu kipindi hiki chote wamekuwa wakila kodi za Wananchi, millions and millions of money. Sasa hapo uzalendo walioenda kujifunza huko JKT uko wapi. Hata baada ya kupelekwa mahakani lakini wapi, bado wameendelea kung'ang'ania. Na kwa mlolongo ule ule hata vyombo vya maamuzi vimekosa maamuzi ya haraka kuokoa pesa za walipa kodi, hapo uzalendo na uadilifu viko wapi.

Haya, ngoja tusubiri majibu ya serikali kwa jaji Mihayo.
 
CamScanner 06-05-2023 13.32.jpg

Nimemfahamu huyu Jaji muda mrefu kidogo, tokea miaka ya 80!

Katika suala la Tanga Cement kuchukulliwa na Twiga Cement bado ana mawazo ambayo mimi ninayaona kama hegemonic, anataka kwa lazima tukubaliane na mawazo ya Majaji , mawazo ambayo wakati mwingine yanakuwa tofauti kabisa na hali halisi.

Tanga Cement wamefilisika, wanataka kuuza shares. mnunuzi Twiga Cement yupo na anataka kununua hisa ili akiendeshe kiwanda cha Tanga.

Wajanja kupitia watu wanaojiita Chainze Cement, ambao wala hawajulikani wananufaika au kudhurika vipi, wameenda mahakamani kupinga Tanga Cement kuchukuliwa na Twiga Cement.
Hao Chalinze Cement wameenda Mahakamani kwa kutumia maamuzi ya Fair Competition Commission(FCC).

Maamuzi ya FCC ilikuwa ni kubatilisha ununuzi wa Tanga Cement na Twiga Cement, kwa kisingizio ati siyo fair busness.
Mahakama Kuu ikakubaliana na hilo.

Kwenye ground hao Majaji na FCC hawajui inaelekea Chalinze Cement ilikuwa imecheza mchezo wa kifisadi.
Chalinze Cement haikuwa imesajiliwa kihalali, wamiliki wake hawajulikani, ofisi zake hazijulikani zilipo.

Hawa Majaji wanashindwa kulielewa hilo kwa kutumia Common Sense, na kuelewa kuwa hapo kuna kaufisadi.

Sasa huyu Jaji Mihayo, amesikika magazetini na kwenye vyombo vya habari akitetea utopolo wa hiyo Chalinze Cement na kuilaumu serikali kuwa inadhalilisha mahakama.

Mimi sijui huyu Jaji Mihayo ana matatio gani ya kuelewa ufisadi ulio wazi katika suala zima.
 
Wanamtandao wanataka wauziwe wao hiyo Tanga cement kwa bei ya kutupa. Tuna mambo ya ajabu sana nchi hii.
 
Sio serikali tu hata wananchi ambao Wana upeo mkubwa,wakati nawa chini kabisa walisha idharau mahakama na majaji muda mrefu sana tokana na mahakama kupitia majaji na mahakimu kuidhalilisha mahakama kwa maamuzi ya kijinga na kipupavu ambayo hayawezi fanywa na mtu mjinga mfano ulio dhahiri ni kesi ya Mwenyekiti wa chama Cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), mahakama ilionesha uzwazwa wa kiwango Cha SGR

Mbegu walio panda majaji na mahakimu ndio mavuno yake yanaonekana sasa,wajinga wakubwa
 
Hii Nchi kila kukicha wanadharau maamuzi ya mahakama harafu baadae utasikia ndege imeshikwa yaani hawajui madhara yake kabisaa..
 
View attachment 2646768
Nimemfahamu huyu Jaji muda mrefu kidogo, tokea miaka ya 80!

Katika suala la Tanga Cement kuchukulliwa na Twiga Cement bado ana mawazo ambayo mimi ninayaona kama hegemonic, anataka kwa lazima tukubaliane na mawazo ya Majaji , mawazo ambayo wakati mwingine yanakuwa tofauti kabisa na hali halisi.

Tanga Cement wamefilisika, wanataka kuuza shares. mnunuzi Twiga Cement yupo na anataka kununua hisa ili akiendeshe kiwanda cha Tanga.

Wajanja kupitia watu wanaojiita Chainze Cement, ambao wala hawajulikani wananufaika au kudhurika vipi, wameenda mahakamani kupinga Tanga Cement kuchukuliwa na Twiga Cement.
Hao Chalinze Cement wameenda Mahakamani kwa kutumia maamuzi ya Fair Competition Commission(FCC).

Maamuzi ya FCC ilikuwa ni kubatilisha ununuzi wa Tanga Cement na Twiga Cement, kwa kisingizio ati siyo fair busness.
Mahakama Kuu ikakubaliana na hilo.

Kwenye ground hao Majaji na FCC hawajui inaelekea Chalinze Cement ilikuwa imecheza mchezo wa kifisadi.
Chalinze Cement haikuwa imesajiliwa kihalali, wamiliki wake hawajulikani, ofisi zake hazijulikani zilipo.

Hawa Majaji wanashindwa kulielewa hilo kwa kutumia Common Sense, na kuelewa kuwa hapo kuna kaufisadi.

Sasa huyu Jaji Mihayo, amesikika magazetini na kwenye vyombo vya habari akitetea utopolo wa hiyo Chalinze Cement na kuilaumu serikali kuwa inadhalilisha mahakama.

Mimi sijui huyu Jaji Mihayo ana matatio gani ya kuelewa ufisadi ulio wazi katika suala zima.

Nakubaliana na wewe kabisa kuwa huyu Jaji mstaafu Mihayo ana matatizo ya kimaadili na hayajaanza leo hata nashangaa wanamteua kuwa Mwenyekiti wa Mashirika makubwa kama Vodacom na TTB bila kumfanyia due diligence!! Huko nyuma akiwa Jaji enzi ya marehemu Jaji Mkuu Nyalali alishasimamishwa kazi na kukutwa na hatia ya kupokea rushwa na hatimaye kuja kutolewa na marehemu Jaji James Mwalusanya on appeal!!

Kuhusu stand yake juu ya acquisition ya Tanga cement na Twiga cement it does not make sense asserting that investors will be discouraged by the government decisions going against decisions made by a corrupt judiciary ; in fact investors will be discouraged to come to Tanzania if the government interferes with their investment decisions!!

The basis for the court to deny the acquisition of Tanga cement by Twiga cement was based on the wrong premises that it would thwart fair competition which is not true! Twiga cement would be a monopoly if and only if they were the sole producers of cement in the country in which case they could corner the market at the detriment of consumers. As the situation of cement production in the country is dictated by many producers as enumerated below by their brands:

Dar es salaa: TWIGA ,NYATI, KISARAWE, DIAMOND, CAMEL, LULU, HUAXIN

Mtwara: DANGOTE

Mbeya: MBEYA CEMENT

Tanga: HUAXIN, SIMBA, KILIMANJARO


Kilimanjaro: MOSHI CEMENT

It is very lear therefore that there is fair competition in the cement industry such that prices cannot be dictated by a few producers to hurt consumers.
 
Back
Top Bottom