Jaji Lubuva: Msitegemee jipya kutoka kwangu

Nani atategemea jipya kutoka kwa kizee kama hicho chenye umri miaka 99.
 
Mbona kasema kitu cha kweli na wazi. Mkitaka tuibadilike badilisheni Katiba na sheria. Marefa mbalimbali mchezo uleule.

Hizo ni pumba MMK!Wizi wa kura hauruhusiwi hata kwenye katiba ya sasa!Tusipokuwa na viongozi waadilifu na wabunifu hata Mungu atupe katiba hatutafika popote!
 
Hapo wale wote wanaoituhumu NEC kuvuruga uchaguzi kila mara kwa taratibu zake zisizolidhisha pande zote, ni muda muafaka wa kuboresha mbinu za kuziba mianya yote inayoweza kuzibika kama walivyojaribu kuziba chaguzi zilizopita.
 
Kama kweli kasema hana jipya basi he is failure, kiongozi anaamini hana jipya then anakubari kuapishwa. Wazee wetu wanatutafutia sababu ya kutupa radhi.

Jipya sio katika kubadilisha sheria tu, manake mara zote sheria iko too general ila tafsiri ndio sarakasi zinapoanzia. Bado anayonafasi ya kutafuta mapya kama sio mtu wa kuganga njaa, kwa mfano:
  • Kutengeneza mipango mkakati ya kuhakikisha kila mtu mwenye sifa ya kupiga kura anapiga kura
  • Awe na mikakati mipya ya kuhakikisha anaandikisha watu wengi zaidi na kuwahamasisha wapige kura kwa wingi wake manake chaguzi zilizopita chini 50% ndio wanapiga kura
  • Uwazi katika zoezi zima bado unamashaka lukuki na jipya linatakiwa katika kuhakikisha zoezi zima la uchaguzi linakuwa la haki na pasina shaka upendeleo na matumizi ya usalama wa taifa kuiba kura yanakoma.
  • Jipya linatakiwa katika uandaaji wa vifaa na usambazaji katika vituo vya kupigia kura kutilia maanani miundombinu mibovu na umeme
  • Kubadilisha kabisa utendaji na muonekano wa tume kutoka taasisi ya CCM na ofisi ya serikali kuwa engine ya mabadiliko na demokrasia
  • Kuweka mfumo wa kisasa na teknolojia ya kisasa katika kupokea, kuchambua, kutoa, na kutunza taarifa zinazohusu uchaguzi pamoja na kupunguza muda wanao tumia kutangaza matokeo
  • Kuweka mifumo mipya kabisa ya mawasiliano, kuelimisha taasisi zingine pamoja na wadau majukumu yao wakati wa uchaguzi
  • Kuanza kufanya maandalizi ya uchaguzi mapema na sio miezi michache kabla ya uchaguzi.
 
Mbona sisi makazini kwetu mfanyakazi mpya wa shirika au kampuni anaambiwa mwanzo tu kabisa kwamba anatarajiwa afanye mapya ili kuboresha utendaji na ufanisi wa kampuni au shirika lake? chini ya katiba hii hii?

Mwenyekiti wa NEC nae anatarajiwa kufanya mapya kuboresha hali ilivyo na kama hawezi basi hafai. Watu wa design hii wanaofanya kazi kwa mazoea wanatuchosha kweli kweli.
 
Lubuva amekuwa wazi na amesema ukweli. Hatutarajii mstaafu kama yeye awe chachu ya mabadiliko na hasa ukizingatia kuwa kilichobaki kwake kwa sasa ni kusukuma siku kuelekea kwenye "senility". Na kwa mtazamo wangu Mwenyekiti wa hii tume ya uchaguzi ana "influence" ndogo sana kwenye mfumo na matokeo ya uchaguzi wa nchi hii. Yeye kazi yake ni ya kupewa matokeo yaliyokwishapikwa na kuyatangaza kama kasuku.
 
kiravu amestaafu, sasa mbona wamemchagua lubuva ambaye naye anatakiwa awe alishastaafu au atastaafu soon?:shock:

Hata mimi sioni sababu ya kumtoa Kiravu wakati alishawafanyia kazi nzuri tu. Baada ya kumtoa Jaji mstaafu wangempa Rubuva kwa kuwa naye ana sifa ya ustaafu!!
 
Mbona sisi makazini kwetu mfanyakazi mpya wa shirika au kampuni anaambiwa mwanzo tu kabisa kwamba anatarajiwa afanye mapya ili kuboresha utendaji na ufanisi wa kampuni au shirika lake? chini ya katiba hii hii?

Mwenyekiti wa NEC nae anatarajiwa kufanya mapya kuboresha hali ilivyo na kama hawezi basi hafai. Watu wa design hii wanaofanya kazi kwa mazoea wanatuchosha kweli kweli.

Naamini wafanyakazi wengi unaowaongelea ni vijana au at least bado hawajafikia umri wa kustaafu. Hapa tunamuongelea Lubuva ambaye kimsingi ni mstaafu na ameshapita umri wa kufikiria au kuleta mambo mapya. Kimsingi alitakiwa awe anacheza na wajukuu au vitukuu huku akisuburi pensheni yake na siku atakayochukuliwa na mtoa maisha.
 
Hii inanipa wasiwasi kwamba hata kwenye chaguzi zijazo bado uchakachuaji wa kura utaendelea kufanyika!
 
Nafikiri Lubuva yuko right kabisa. There is nothing he can do. Na heri amekuwa mkweli mapema kabisa kuepuka lawana. Kutokana mfumo mzima uliopo hana jipya na hataweza kuwa na jipya. Haweze kusema ana jipya wakati hana. Huo ndio ukweli. Amesema ukweli hata kama unauma.

Na aliyemteua alitaka mtu asiye na jipya. ukipewa hii nafasi ukaleta jipya wanakutoa kama kamanda Basilio ambaye alikuwa rpc arusha sasa anasoma magazeti Dar .Mzee wetu Damian hongera endeleza ya zamani tu
 
Mbona sisi makazini kwetu mfanyakazi mpya wa shirika au kampuni anaambiwa mwanzo tu kabisa kwamba anatarajiwa afanye mapya ili kuboresha utendaji na ufanisi wa kampuni au shirika lake? chini ya katiba hii hii?

Mwenyekiti wa NEC nae anatarajiwa kufanya mapya kuboresha hali ilivyo na kama hawezi basi hafai. Watu wa design hii wanaofanya kazi kwa mazoea wanatuchosha kweli kweli.

Hivi unategemea ni kutoka kwa mstaafu?? Hebu check hiki kipande hapa chini!!

[h=1]Brain function can start declining 'as early as age 45'[/h]The brain's ability to function can start to deteriorate as early as 45, suggests a study in the British Medical Journal.
University College London researchers found a 3.6% decline in mental reasoning in women and men aged 45-49.
They assessed the memory, vocabulary and comprehension skills of 7,000 men and women aged 45 to 70 over 10 years.
The Alzheimer's Society said research was needed into how changes in the brain could help dementia diagnoses.
Previous research had suggested that cognitive decline does not begin much before the age of 60.
But the results of this study show that it could in fact begin in middle age.
This is important, the researchers say, because dementia treatments are more likely to work at the time when individuals start to experience mental impairment.
The UCL researchers tested the cognitive functions of 5,198 men and 2,192 women aged 45 to 70, who were all UK civil servants, from 1997 to 2007.
Individuals were tested for memory, vocabulary and aural and visual comprehension skills.
Differences in education level were taken into account........
Source: BBC
 
Anaweza kukataa kumtangaza mgombea ambaye amepatikana kwa kura zilizopikwa mezani badala ya zile zilizopigwa vituoni

Hiyo itampa heshima kwa vizazi 100 vijavyo!nadhani hana cha kupoteza kwa umri wa mika 60 na zaidi
 
Jamani Rais anafikiria kweli kabla hajateua hao wanagawiwa madaraka wapate kuendelea kula baada ya kufanya unyama wa ufisadi kwa muda mrefu? huyu Hamid Mahmoud Hamid alikuwa Jaji Mkuu wa Mahkama ya Zanzibar tangu miaka ya themanini, wanawe wamepata kupewa vibali vya kuwa Wanasheria wakubwa bila kuwa na elimu hiyo hata kidogo, na kuishia kushinda kesi kwa mikwara na misaada ya baba lao Jaji Mkuu na kuburuza haki za wengi Zanzibar nzima kwani wao waliangalia pesa tu na si haki.
Jamani hili Hamid Mahmoud ni fisadi au siyo?
 
Bro mbona hapa unatuuliza sisi tena???si wewe ndo umetuambia hayo maneno???sisi ni wageni kabisa!!!
 
Mbona kasema kitu cha kweli na wazi. Mkitaka tuibadilike badilisheni Katiba na sheria. Marefa mbalimbali mchezo uleule.

Sawa mkuu! Huo ndio ukweli mia kwa mia. Nampongeza kwa kuzungumzia daftari la wapiga kura. Hilo ni jipya ... maana walioondoka walikuwa wanalifumbia macho hilo.
 
Ndg,wana JF tusipende kupoteza muda kwa kubishia ukweli.
Nani hajui katiba hii ndiyo inayomwongoza Rais kuteua hata mtoto wake au Hawala wake?
Nani hajui kwamba katiba hii inagawa majukumu kwa yeyote anayeteuliwa kwamba,utatekeleza majukumu yako kaadiri itakavyo pendekezwa au kuagizwa na Rais.
Kwa hiyo Jaji Lubuva hajavunja katiba,anasema hana nafasi ya kuleta miujiza kwa mfumo huu uliomteua ndiyo utakao mwongoza,amekuwa muwazi!!!!!!!!!
Ndo maana wenye akili juu ya Uteuzi wake au mtu yoyote anayeteuliwa na Rais hatushangai wala kushangilia kwmba kuna faraja inakuja,Maana tunajua kwamba atafanya kazi kadiri itakavyompendeza Rais!
Siyo kadiri itakavyoupendeza Ummah.
Comrades,tusimlaumu!
Tujilaumu kuwa sehemu ya baraka hizi za mamlaka makubwa ya Urais
Kunung'unika wakati tunajua sisi ndo mwanzo...mwisho.Haisaidiii
 
Hivi hawa wanaanza kazi lini? Maana website ya Tume ya Uchaguzi bado inaonyekuwa Judge Lewis M. Makame ni mwenyekiti wa tume na mkurugenzi ni Kiravu. Pia webiste ina breaking news ya kutangazwa kwa uchaguzi mdogo jimbo la Igunga.
 
Kumpa cheo hiki Mzee kama huyu ni kuepusha mabadiliko.Lakin kwa upande mwingine wanamwonea.Hv atavumilia kwel kuona mageuz dhahir yatakayotokea?Ni kumtia presha tu mzee ndiyo maana amechagua njia nyepesi (kutojiandaa) ambayo ni hasara kwa Tanzania.Mtu akiteuliwa aanze na fikra na kuziweka waz na kuleta maendeleo ndiyo mabadiliko chanya.
 
Back
Top Bottom