Jaji Lubuva: Msitegemee jipya kutoka kwangu

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
MWENYEKITI mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji mstaafu Damian Lubuva, amesema katika utekelezaji wa majukumu yake watu wasitegemee mapya kutokana na mfumo uliopo kumtaka aendeleze yaliyokuwa yakifanywa na mtangulizi wake, Jaji Lewis Makame.

Jaji Lubuva alisema hayo muda mfupi baada ya kuapishwa Ikulu Dar es Salaam na Rais Jakaya Kikwete.

Alisema Rais Kikwete alipompa taarifa ya uteuzi wake, alisita kuchukua nafasi hiyo kwa sababu ina changamoto nyingi hasa kipindi hiki cha mchakato wa mabadiliko ya katiba.

"Nimekuwapo kwenye utumishi wa umma kama jaji kwa muda mrefu, lakini niliposikia uteuzi huu nilisita kwa kuwa ni kipindi kigumu hiki cha sasa. Hata hivyo, nilikubali nafasi hiyo baada ya kutafakari," alisema Jaji Lubuva.

Alisema kutokana na mfumo uliopo hana jipya, ila ataendeleza pale Jaji Makame alipoachia mpaka mfumo huo utakapobadilika."Tutaendeleza shughuli za tume kama ilivyo na kuboresha daftari la wapigakura kuanzia sasa ili kuondoa malalamiko," alisema.

Jaji Lubuva alisema atahakikisha hapendelei chama chochote katika uchaguzi wowote utakaofanyika, hivyo vijiandae kufanya uchaguzi huru na haki.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Malaba, ambaye naye aliapishwa jana alisema anajua Nec kuna changamoto nyingi, lakini atapambana nazo ili kufanya kazi kwa ufanisi."Ninajua kuna changamoto nyingi na hatutapendelea kama tulivyoapa pale," alisema Malaba.Mwingine aliyeapisha jana ni Makamu Mwenyekiti wa Nec, Hamid Mahmoud Hamid.


Source: Mwananchi

Maoni yangu

Tunapohitaji Rais ateue watu wenye mawazo mapya, lengo letu linakuwa ni kuachana na utamaduni wa kuteua watu wasio innovative na wanaofanyakazi kwa mazoea kama hawa wastaafu wetu ambao kila kukicha Rais anaendelea kuwateua. Hivi kama hawa wastaafu wangekuwa ni potential si tungewasikia wakati wa utumishi wao kabla hawajastaafu???Kwann tunapewa watu waliochoka fikra na mawazo na wanaokuja kula fedha za walipa kodi bila ya kuwa na significant contribution kwa taifa letu?? Kuna ugumu gani kwa m/kiti wa tume ua uchaguzi kuongoza mabadiliko ya huo anaouita mfumo uliopo???Huo mfumo kauweka nani had usibadilike??Kama hawezi kazi ni kipi kilimfanya aikubali???Hizi njaa jamani zitawacost!!!

Lubuva anasema waziwazi tena bila aibu kuwa tusitegemee jipya, hivi kwa kauli hiyo anataka kuwaambia nini watanzania?? Tena anasema ataendeleza yale yaloyaliyoachwa na mtangulizi wake, Lewis Makame, Hivi Lewis Makame alifanya yapi mazuri zaidi ya kutuletea utata katika chaguzi zetu???Ni utendaji mbovu wa Tume ya uchaguzi chini ya Makame umekuwa ukilalamikiwa kila uchaguzi, Ni mfumo mbovu wa uchaguzi chini ya Makame unaoshindwa hata kutangaza idadi kamili za wapiga kura kila uchaguzi ktk kata na majimbo. Huu mwaka naona umeanza vibaya!!!!

KAMA LUBUVA UNAFIKIRIA KUENDESHA HIYO OFISI KWA MAZOEA NA KWA KUENDELEZA YALE ALIYOYAACHA MAKAME, TEGEMEA YALIYOMKUTA KIVUITU WA TUME YA UCHAGUZI WA KENYA. USIFIKIRIE KWAMBA TUTAENDELEA KUWA WAJINGA SIKU ZOTE.
 
Nafikiri Lubuva yuko right kabisa. There is nothing he can do. Na heri amekuwa mkweli mapema kabisa kuepuka lawana. Kutokana mfumo mzima uliopo hana jipya na hataweza kuwa na jipya. Haweze kusema ana jipya wakati hana. Huo ndio ukweli. Amesema ukweli hata kama unauma.
 
Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi amesema waTz wasitegemee jipya lolote kutoka kwake kwa mfumo huu uliopo sasa,source Mwananchi
 
Hata kuleta transparency kwenye kujumlisha matokeo ya uchaguzi nayo hawezi? Kama ndo hivyo basi safari ya ukombozi bado ndefu.
 
​jamaa ni mtu makini yeye amesema lazima mfumo wa chaguzi na usimamizi wa tume ubadilike na katiba ndio itakuwa mkombozi na si yeye binafsi kwani kama mfumo utakuwa kama wa sasa basi ata yeye hatokuwa na uwezo wa kubadili matokeo ya mfumo huu
 
Mheshimiwa Lubuva ni mkweli! Tuache kulalamikia kila kitu, Katiba mpya ndiyo suluhisho na ndiyo itakayompa Mhe. Lubuva uhuru na uhalali wa kuyatenda mambo mapya anayoyafikiria.
 
Kwani unadhani yeye yupo juu ya katiba, anafata jinsi katiba na sheria zinavyosema. Kwasababu tumeshaona mapungufu mbalimbali, basi tuyaibue kwenye mchakato wa Katiba mpya.
 
bongo bado serikali inaona raia wake wapo primitive level na raia wake wanajiona wako the highest stage ndio kazi inapokuwepo hapo..

RIP TZ
 
Mbona kasema kitu cha kweli na wazi. Mkitaka tuibadilike badilisheni Katiba na sheria. Marefa mbalimbali mchezo uleule.

MMKJ: Hata bila ya kubadilika kwa katiba angeweza kuleta tofauti. Wapi katika Katiba ya sasa inasema Mkiti wa NEC lazime avuruge uchaguzi?
 
Naweza kubadilisha mfumo kwa kuandika mapendekezo ili nec itumie mfumo wa computer kumuwezesha kila mtz mwenye haki ya kupiga kura apige hata kama hayupo sehemu aliyojiandikisha hili linawezekana kwa katiba yetu pia kuruhusu watz waliopo nje nao kupiga kura. Huwezi ukamuambia mtu asisafiri hata kama kuna ulazima wa kusafiri kisa asubiri kupiga kura! Hii kitu Lubuva unaweza kubadilisha ili mtu awe huru kufanya shughuli zake bila wasiwasi.
 
kesha liswa ya kuongea, lakini kama anataka naye kuweka historia afanye kufuata sheria atafanikiwa
 
Nina wasiwasi na swala zima la katiba mpya,hawa jamaa wanaweza wakaichelesha hadi 2016,kwa maslahi yao na familia zao,ndio maana Lubuva ameongea ukweli kwamba hawezi kubadilisha mfumo uliopo.
 
kiravu amestaafu, sasa mbona wamemchagua lubuva ambaye naye anatakiwa awe alishastaafu au atastaafu soon?:shock:
 
Mheshimiwa Lubuva ni mkweli! Tuache kulalamikia kila kitu, Katiba mpya ndiyo suluhisho na ndiyo itakayompa Mhe. Lubuva uhuru na uhalali wa kuyatenda mambo mapya anayoyafikiria.
Kwani haya mambo ya hovyo yanayoratibiwa sasa na NEC kama uwizi wa kura na uwepo wa daftari la hovyo la wapiga kura yameruhusiwa na hii Katiba iliyopo???? Siamin kama suluhisho pekee ni Katiba, zipo sheria na kanuni mbalimbali kandamizi zinazousiana na uchaguz zinaweza kurekebishwa zikaleta ahueni kuliko ilivyo sasa. Kwa mfano mwaka 2010 waTZ wengi hasa wanafunzi wa vyuoni walishindwa kupiga kura kwa kuwa waliondolewa vyuoni na kurudi makwao, Je na Lubuva naye atafanya upuuzi wa hivyo wa kunyima raia haki zao ya kupiga kura???
 
Back
Top Bottom