Mcheza Karate
JF-Expert Member
- Jun 30, 2011
- 690
- 350
Wakati chama cha ANC cha Afrika kusini kikisherehea siku yake ya kuzaliwa matukio mawili muhimu kwangu nimeona. Mosi ni Rais wa zamani Thabu Mbeki kuhudhuria sherehe hizo kwa mara ya kwanza tangu aondolewe madarakani mwaka 2007, kitendo kilichomfanya rais Zuma alipokuwa anahutubia amtaje mara mbili kuwa "Mbeki amehudhuria leo". Tukio la pilh ni rais Jacob Zuma kumwaga pongezi kwa chama cha mapinduzi na MWL, NYERERE kwa kuwapa ANC makazi Morogoro wakati wakipigania Uhuru. Hakika nimeamini Nyerere hajafa. Fikra na mchango wake unaonekana. Hili ni somo kwa viongozi wetu wengine kama JK.