Jack ateswa na usagaji

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Jack ateswa na usagaji

Na Gladiness Mallya
MSHIRIKI wa Miss Tanzania 2005 akitokea Kanda ya Ilala, Jaqueline Patrick (pichani) ameibuka na kusema anateswa sana na wasichana wenzake ambao ni waumini wa mchezo mchafu wa usagaji.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa, wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Jack alisema anawashangaa sana wasichana wenye tabia hiyo na kwamba hawezi hata kuthubutu kuwa na rafiki mwenye tabia hiyo ambayo yeye ameiita ya kipuuzi.

“Sijui ni kwa nini wanafanya uchafu wa aina hiyo? Yaani mimi naogopa hata kuwa na rafiki msagaji. Ni hatari, maana anaweza kunishawishi. Kwa kweli nakaa mbali sana na wasichana wa aina hiyo,” alisema Jack na kuongeza:

“Lakini kama ningekuwa na uwezo ningefungua kituo rasmi cha kutoa elimu elekezi juu ya tabia hiyo mbaya. Sina fedha, lakini naamini watu wa haki za binadamu na ustawi wa jamii watakuwa wamenisikia. Wanaweza kufanya kitu kwa wasichana wa aina hiyo.”

chanzo:Jack ateswa na usagaji - Global Publishers
 
Ah hao nao wanapenda kuuza sura kwenye magazeti matokeo yake wanakashfiwa kwenye gazeti.na sikuizi haipiti mwezi unatangaziwa habari ya star huyu msagaji sijui hata hizi pic wakiwa wana fanya huo ufuska wanazipata wapi hawa watu wamagazeti.
 
Wadaku bwana mambo yao ndo hayo, kichwa cna habari na story tofauti kabisa... Ila Jamaa wanauza magazeti kweli kweli!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom