in and out
Member
- Jun 30, 2011
- 69
- 6
chama cha democrasia na maendeleo (chadema)kimesema, endapo kitapewa ridhaa na wanainchi ya kuunda serikali ktk uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kitahakikisha kinaanzisha utaratibu wa kufanya maombi maalum kwa taifa ili mungu aweze kufanikisha ndoto ya watanzania ya kuwa na maisha bora. Ahadi hiyo ilitolewa jumapili iliyopita na mwenyekiti wa CHADEMA mheshimiwa Freeman mbowe, alipokuwa mgeni rasmi katika hafla maalum ya uzinduzi wa kitabu cha kuhamasisha maendeleo ya watanzania kilicho andikwa na mtume john nengala Lobulu. katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye kanisa la Maranatha Christian Center lililopo kinondoni, jijini Dar es salam na kuhudhuriwa na watu wa kada mbalimbali , mbowe ambaye ni mbunge wa hai, mkoani kilimanjaro na kiongozi wa upinzani bungeni, alisema maombi ni muhimu kwa ustawi wa taifa, hivyo yanapaswa kupewa uzito na kuwa sehemu ya utamaduni wa watanzania. "kutokana na umuhimu wake ndio maana tumeahidi kwamba tukifanikiwa kupata ridhaa ya kuongoza nchi hii kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 tutaanzisha utaratibu maalumu wa kuliombea taifa, katika maombezi hayo kila mmoja kwa imani yake aliombee taifa ili mungu aweze kufanikisha malengo yetu, maombi ni jambo muhimu sana kwa taifa lazima yapewe kipaumbele," alisema. Awali, kabla ya kuzindua kitabu hicho kiitwacho Vikwazo vya mafanikio yako na jinsi ya kuvishinda. Mbowe alitoa wito kwa watumishi wa mungu pamoja na viongozi wa serikali kutofanya kazi kwa maslahi binafsi, badala yake watumike kwa kutengeneza mazingira yatakayonufaisha kizazi kijacho badala ya kuendelea na hali ya sasa ambapo wanaonekana kufanya kazi kibinafsi zaidi. Hata hivyo, alisema ili hali hiyo iweze kufanikiwa kuna haja kwa watanzania bila kujali tofauti zao za kiimani kujikita zaidi katika maombi ili taifa liwe na viongozi wenye hofu ya mungu ambao watafanya kazi kwa maslahi ya taifa na kizazi kijacho kwani bila hofu ya mungu kutawala miongoni mwa viongozi ni vigumu kuwajibika kwa wanainchi bali wataendelea kujali maslahi yao binafsi na kuwaacha wanainchi wakiendelea kuteseka.