ITV vs StarTv

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,279
8,494
Nimekuwa mtzamaji mzuri sana wa vituo hivi vi2 vya TV, nimeshawishiwika kuwashirikisha wana JF kwa pamoja tuweze kuangalia mapungufu na mazuri ya vituo hivi ili kuweza kuwashauri waendelee kutuletea habari zilizokamilika.

ITV.
  • Taarifa yao ya habari inaboa, haitoi picha halisi ya matukio na hasa kwa upande wa taarifa za kimataifa huwa wanatoa vichwa vya habari pekee.
  • Wamekuwa ni wabaguzi wakionyesha kutowajali watazamaji wa vipindi vyao km hali ilivyo hivi sasa kwa mashabiki wa simba kunyimwa habari zinazoihusu timu yao.
  • Reporters huwa hawawezi kupiga stand up wakiwa sehemu ya tukio kitu ambacho ni muhimu sana ili kujenga imani kwa watazamaji kuwa anayeripoti alikuwepo sehemu ya tukio.
  • Taaluma ya uandishi inaelekea kuwa mbali sana na waandishi wa kituo hiki.
StarTV
  • Taarifa yao ya habari kidogo inavutia kwani huwa wanajaribu kuingia kwa undani zaidi na hata habari za kimataifa kuna mtu anaitwa Samadu Hasani huwa anaripoti vizuri sana.
  • Pamoja na kuhusika na tukio la kuzuiwa kupiga picha na kurusha mechi za ligi ya Voda laivu, wameendelea kurusha habari za Simba bila kinyongo.
  • Bado pia kuna udhaifu wa reporters kupiga stend up kwenye matuikio
  • Taaluma inaonekana lakini sio sana.
Nawaachia wengine kuwasaidia hawa jamaa ili waweze kujirekebisha na kusonga mbele.
 
Taaluma inakuwaje mbali? umetumia mizania ipi? au gut feeling yako? Nadhani fanya utafiti halafu uje na kitu kamili. Personal feelings bila support haitakuwa na msingi mzuri wa kusimama. Mambo ya Simba kutotangazwa si issue kubwa kihivyo angalia mpangilio wa vipindi kwa ujumla na sio ku zero inn kwenye Simba tuuuuu!!! Hebu chukua ratiba ya wiki halafu chambua na linganisha!!
 
Hebu ngoja tusubiri matapeli wa clouds tv yao itakuwaje...
Maana kwa sasa wanaturusha tu majoka
 
Ratiba ya wiki inaweza kuwa nzuri, lakini presentation ikawa mbovu. Ndio wanataarifa ya habari kwenye ratiba yao, je wanavyoripoti ni sahihi? wewe binafsi unapata kile unachokihitaji kwenye kile kipindi. Na hilo la simba ni mfano mmoja wapo tu, leo ni Simba, kesho itakuwa ni jamii fulani, labda Wamasai kwa kuwa tu viongozi wao wamegoma kuwaruhusu ITV warushe jinsi ngombe wao wanavyojifungua!!!!!!!
 
1. Bill kwanini ITV na Star TV tuu, mbona kuna TBC na Channel Ten, kwanini hukuwaweka?.2. Sio kweli taarifa za habari ITV zinaboa, uless kwako ikishakosekana habari za simba, basi ndio taarifa nzima inaboa?.3. Hiyo unayoiita stand up, inaitwa cut ya "piece to camera", mbona wote wanazitumia vizuri tuu?.4. Taaluma pia imesimama wima, unless kama ulitegemea TV zetu ziripoti kama CNN, SKY au BBC, hapo nitakuelewa japo kidogo.
 
Hebu ngoja tusubiri matapeli wa clouds tv yao itakuwaje...
Maana kwa sasa wanaturusha tu majoka
hawa wanakuja kuburudisha na kuhamasisha ngono na upuuuzi kwa vijana wetu wadogo.......kweli hawana jipya.

ITV
Wamekuwa ni wabaguzi wakionyesha kutowajali watazamaji wa vipindi vyao km hali ilivyo hivi sasa kwa mashabiki wa simba kunyimwa habari zinazoihusu timu yao

HILI NI KUNDI ama genge la waandishi mufilisi.....wasio jali afya ya jamii ila utashi wao, muda si mwingWi mwangi wa haya utaivuruga ITV.
 
Nimekuwa mtzamaji mzuri sana wa vituo hivi vi2 vya TV, nimeshawishiwika kuwashirikisha wana JF kwa pamoja tuweze kuangalia mapungufu na mazuri ya vituo hivi ili kuweza kuwashauri waendelee kutuletea habari zilizokamilika.

ITV.
  • Taarifa yao ya habari inaboa, haitoi picha halisi ya matukio na hasa kwa upande wa taarifa za kimataifa huwa wanatoa vichwa vya habari pekee.
  • Wamekuwa ni wabaguzi wakionyesha kutowajali watazamaji wa vipindi vyao km hali ilivyo hivi sasa kwa mashabiki wa simba kunyimwa habari zinazoihusu timu yao.
  • Reporters huwa hawawezi kupiga stand up wakiwa sehemu ya tukio kitu ambacho ni muhimu sana ili kujenga imani kwa watazamaji kuwa anayeripoti alikuwepo sehemu ya tukio.
  • Taaluma ya uandishi inaelekea kuwa mbali sana na waandishi wa kituo hiki.
StarTV
  • Taarifa yao ya habari kidogo inavutia kwani huwa wanajaribu kuingia kwa undani zaidi na hata habari za kimataifa kuna mtu anaitwa Samadu Hasani huwa anaripoti vizuri sana.
  • Pamoja na kuhusika na tukio la kuzuiwa kupiga picha na kurusha mechi za ligi ya Voda laivu, wameendelea kurusha habari za Simba bila kinyongo.
  • Bado pia kuna udhaifu wa reporters kupiga stend up kwenye matuikio
  • Taaluma inaonekana lakini sio sana.
Nawaachia wengine kuwasaidia hawa jamaa ili waweze kujirekebisha na kusonga mbele.

Aisee umewapatia kweli hawa. Mtangazaji wa taarifa ya habari wa ITV anajiita ALBERT NYITWA anachapia Kiswahili kwa kwenda mbele. Kupanda mazao shambani anasema KUPANDIKIZA, Kuharakisha anasema KUHAIRISHA, na maneno kibao kila siku na sijamsikia hata siku moja akisema "samahani, nitarudia hapo" kama wenzake wafanyavyo. Yaani yeye sijui ni kabila gani lugha ya Kiswahili inagongana saaaana!
 
umesema kweli hawa jamaa wanaboa, kwani hata baadhi ya waeangazaji wake ni wake wake wasikuwa na pumzi za kutangazia, mfano ni Gamba, huyu jamaa anafanya kazi kwa kubahatisha ila anahema sana wakati wa kutangaza sijui ni bahati au ukabila ndio kigezo cha kupata kazi ITV, kwa kitaaluna ni hovyo
 
Aisee umewapatia kweli hawa. Mtangazaji wa taarifa ya habari wa ITV anajiita ALBERT NYITWA anachapia Kiswahili kwa kwenda mbele. Kupanda mazao shambani anasema KUPANDIKIZA, Kuharakisha anasema KUHAIRISHA, na maneno kibao kila siku na sijamsikia hata siku moja akisema "samahani, nitarudia hapo" kama wenzake wafanyavyo. Yaani yeye sijui ni kabila gani lugha ya Kiswahili inagongana saaaana!
Albert Nitwa ni mtangazaji gwiji, alianzia RTD akaenda BBC.
 
Huu nao ni mtazamo ila kwangu mimi ITV nikiwa home siiangalii manake inaonekana ni TV ya familia zaidi. Kwa wakati ule nilipokuwa home Mengi hakuacha kuonekana kwenye taarifa ya habari hata kama alilolifanya halikuwa NEWZ. Kimsingi Star wanawafunika ITV. Ni mtazamo tu wala msirumbane wakubwa!
 
acheni hayo majungu yasiyo na mbele wala nyuma,,,,,what,s simba anyway....mbona hukuchambua tbc1 na ch10......kumbuka itv ni umbeatable,ukienda kule vijijini mpaka seti ya tv huwa inaitwa itv

tchao
 
Mkuu najua tatizo lako kubwa ni habari za simba, klabu kubwa sana hii na ile ya jangwani, mimi nilidhani ktk karne hii ya digital hizi klabu zingekuwa na tv stations zao, kwa mantiki hiyo kukidhi kiu ya nyie washabiki mnaotafuta habari kwa udi na uvumba
 
acheni hayo majungu yasiyo na mbele wala nyuma,,,,,what,s simba anyway....mbona hukuchambua tbc1 na ch10......kumbuka itv ni umbeatable,ukienda kule vijijini mpaka seti ya tv huwa inaitwa itv

tchao
inaweza kuwa hivyo, maana ni Kituo cha muda mrefu, ni sawa na handset miaka ya tisini ziliitwa mobitel, dawa ya kupolishi viatu iliitwa Kiwi, kalamu ya wino iliitwa Biki, hizo ni brand ambazo watumiaji walidhani ni name of products.....hivyo kwa kadri siku zinavyoenda ITV inaonekan ni kituo cha hovyohovyo kuliganisha na vingine vyoote nnchi hii.
wasipokua makini miaka si mingi watu watahamishia mawazo na fikra zao TBC.
 
ha ha ha ni mlio wa kengele au kengele yenyewe. Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh haya hiyo clouds. masikhara haya kama radio yenyewe tu inazungumza hainihu... itakuwa telewavisheni? ITV na simba ha ha ha tunaojua stori huwa tuanacheka historia hujirudia ubora definetely star wamedhamiria staa yaani huko anga za juu na independent nao watabakia watu huru wakito dakika 7 za bulletin kwa mtu wanayemjali na kumjua cloud Tv ni mlio tu wa mbuzi, mbuzi mwenyewe hayupo inaweza kuwa gramafoni
 
inaweza kuwa hivyo, maana ni Kituo cha muda mrefu, ni sawa na handset miaka ya tisini ziliitwa mobitel, dawa ya kupolishi viatu iliitwa Kiwi, kalamu ya wino iliitwa Biki, hizo ni brand ambazo watumiaji walidhani ni name of products.....hivyo kwa kadri siku zinavyoenda ITV inaonekan ni kituo cha hovyohovyo kuliganisha na vingine vyoote nnchi hii.
wasipokua makini miaka si mingi watu watahamishia mawazo na fikra zao TBC.
Nguvumali Big up kaka yaani waambie watu kwani si ndio ukweli kalamu biki ha ha ha na tv itv si ndio aliingia bara watu wakadhani ni tv ni itv ha ha ha lakini yote tisa kumi ni kweli staa ni ugali kwa bata hatudiskass stesheni zaidi ya ITV na Star Tv shauri la TBC na Channel teni au Tumaini au Mlimani achana nalo tunadiskas wawili nani kaenda shule katika hili.
 
Back
Top Bottom