ITV: Mh. Mengi adai Manji amerudisha fedha za kifisadi

............. wajinga ndio waliwao, nchi yako, fedha zako, unatetewe, wewe huoni unaona uhasimu wa kibiashara, Mzee Mengi, uchungu ninao ila swala sina ujasiri wako leo! tuvute tutakufuata, wajinga wapo wapuuze maana akili mgando nazo akili!

Sio kwamba sijadhamini mchango wa Mengi kututetea lakini bila ku neutralize nimeelezea upande mwingine wa shilingi wa nguvu ya Mengi ya kupambana na Manji na asipambane na mafisadi wengine kwa nguvu hiyohiyo. You should not quote me wrong sir.
 
Sio kwamba sijadhamini mchango wa Mengi kututetea lakini bila ku neutralize nimeelezea upande mwingine wa shilingi wa nguvu ya Mengi ya kupambana na Manji na asipambane na mafisadi wengine kwa nguvu hiyohiyo. You should not quote me wrong sir.
Hapo tunakwenda pamoja kaka, one thing you should take note pls, Mafisadi wote Mzee wetu anapambana nao kwa usawa, ila kumbuka vitu vitatu vya muhimu: 1: Wakati wote walikuwa "confronted" Huyu Mmoja alichaguliwa na wenzake kujibu mapigo, front man wa wafisadi. 2: Huyu Bwana anakwapua bila kificho na anatumia dharau kubwa shauri ya kuwa na "contacts" within the system. 3: Ushahidi wake upo kila mahali hadi kwa AG aliyepelekwa akaaanza kujiuma uma, badala ya kuufanyia kazi akaamuru huyo shahidi ahojiwe vyombo vya usalama.

Sasa kama sio Mzee Mengi aliyebaki kusema watu wote hata viongozi wanamgwaya mkubwa huyu, labda tungesema kaloga, lakini uchawi wa kwao sijui kama unavuka daraja hadi kwetu huku!!!
 
huu ni wakati wa watanzania kuacha uoga wa kijinga na kufanya maamuz magumu...! kama vibaka mnavyowafanya mitaan kwenu......!
 
Bwana Mengi anadai Manji alikomba Bil.40 za EPA na kukaa nazo miaka miwili, kuzifanyia biashara zake na kupata faida ya Bil.10 na sasa amezirudisha kama alivozichukua. Bila riba bila lolote.

Kwa mujibu wa Bwana Mengi Manji alitakiwa kulipa riba ya Bil.16.

Kama ni kweli Manji ni noma. Na hajakamatwa wala nini.
Manji akamatwe na nani?
 
Hapa Tz Rais tunaemtaka ni kama vile Jerry Rolling aliekuwa rais wa ghana aliyefanya house cleaning, nas io vinginevyo!
 
labda tungesema kaloga, lakini uchawi wa kwao sijui kama unavuka daraja hadi kwetu huku!!!

jamani manji siyo mchawi. jamaa ana hela chafu.

hivi mnajua kama Manji anaweza kununua eneo lote linalokingamana na Nyerere Road kuanzia Kamata mpaka Eapoti na akajenga vitega uchumi?

mimi sijui alipata wapi hayo maela, ila jamaa ana maela.
 
Mengi na Manji wote ni mafisadi, wananichekesha jinsi tu wanavyoshindana kuumbuana ufisadi wao. Mengi anatake advantage ya kutumia vyombo vyake vya habari kupublicise ufisadi wa mwenzie. Pia kutumia vyombo vyake kujionyesha kama mtu saaafi, kumbe kuficha siri iliyopo behind, Mengi ni mafya haswaa.
Kama anasema Manji alitakiwa kulipa riba ya 16bn na hapohapo anasema alipata faida ya 10bn mbona sipati connection hapo, inamaana kapata faida ndogo kuliko riba aliyotakiwa kulipa? Au mtoa mada kuna kitu umechanganya?
Ila nahitimisha kwa kusema kwamba Manji na Mengi wote ni mafisadi!
HIYO RATE YA 16 BIL NI KWA MUJIBU WA INTEREST RATE WA MOST MABENKI YA TANZANIA.
onesha hata kwa hisia ni wapi Mengi amefisadi considering serikali yetu ilivyo ungekuta kashafilisiwa siku nyingi.
 
Hana haja ya kutaja Manji mwenyewe alisema kwenye magazeti kwamba alirudisha na anaishitaki Kagoda kwa kutaka kumdhulumu.
 
Wote mafisadi hao.
Kwanini unakuja hapa untoa maneno kama mtu mwenye kubanwa na kitu. Nini? Elezea ufisadi wao wote wawili. Kuna kitu kimoja ambacho nadhani jamii ya kitanzania inaweza kuwa imekwamishwa na siasa za kipindi fulani, kwamba kila mfanyabiashara au tajiri ni mwizi. I think you are one of those who carry that syndrome!
 
Huyo anaendekeza bifu zake na Manji, hana lolote. Kama ana uchungu na watanzania mbona wafanyakazi wake wanamshinda kuwalipa.
 
unajua Mengi na Manji wanabifu binafsi la kuchukuliana wandani wao.Sasa wanaoneshana ubabe.

Mambo ya mabifu yao , au wanawake wao achana nayo hayakuhusu , muhimu kujua je Manji aliiba hizo pesa au hakuiba!!? na kama amerudisha , sheria inasemaje mwizi akirudisha kuku aliyekuwa amemwiba??. Hiyo ndiyo hoja ya kujibu
 
Sikujua Mengi ni 'mheshimiwa'. Kumbe ukiwa na hela tu unapewa hiyo title ya mheshimiwa?
 
Baadaye utasikia mfanya biashara maarufu kaichangia CCM 500 milioni tena huo mchango hupokelewa na mwenyekiti kwa mbwembwe nyingi na huku Kapteni nonino akiimba kwaya CCM nambari wani,kumbe hiyo hela ni yetu wenyewe lakini kwa umbumbu wetu tumeruhusu wajanja wanemeeke,hakika hivi viserikali corrupt vya Afrika vimekuwa mzigo kwa raia wake wenyewe .Pia najiuliza kila kwenye wizi wa mabilioni wahusika wakuu ni hawa gabachori na maburushi
 
Vita vyao ni vigumu sana hao wawili,wote ni wezi,wote ni magamba,wote ni kandambili,ila mmoja ana fursa ya kuiba kuliko mwenzie
 
Cha kusikitisha, watanzania wote makatuni. Hakuna hata mmoja anaejali wala kuelewa, tumekalia ushabiki tu bila kuchukua hatua kwa vitendo. Nashauri threads kama hzi za ufisadi sijui kashfa ziundiwe link yake ya udaku au vijimambo.
 
Back
Top Bottom