Elections 2010 ITV ina mpango wa kuyumbisha uamuzi wa Tendwa?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Wana-JF:

Kesho (Ijumaa), kituo cha televisheni cha ITV katika kipindi chake cha Kipima Joto saa 3 usiku, mada kuu itakuwa ni Sheria ya Matumizi ya Fedha katika kampeni iliyotiwa saini na JK April mwaka huu.

Ni sheria ambayo tayari imeanza kuwekwa majaribuni na iwapo makali yake au la yanaweza kujulikana wiki ijayo kutokana na maamuzi ya Msajili wa Vyama katika pingamizi la Chadema dhidi ya JK.

Mimi sipingi kwa ITV kufanya mjadala huo ambao wananchi pia wamearifiwa kuchangia kwa simu, ila nina wasiwasi wa timing ya kipindi hicho wakati huu ambapo maamuzi ya Tendwa yanasubiriwa.

Sote tumeshajua ule upande ITV unaegemea katika kampeni hizi (CCM) na hofu yangu ni kwamba pengine kipindi hicho kimeandaliwa maalum katika ku-influence maamuzi ya Msajili wa Vyama katika pingamizi hilo la kihistoiria.

Nina maana hapa ingawa mada ni Sheria hiyo yote kwa ujumla, lakini ni dhahihiri watakaojadili hawataacha kutia mkazo katika hilo pingamizi. Hivyo watoa mada wanaweza kuwa wameandaliwa ili ku-influence uamuzi. Hawa ni pamoja na wale "watakaopiga simu."

Ingefaa kipindi hiki kingeahirishwa hadi baada ya ruling ya Tendwa.
 
Marksman una akili sana kwa kuona kitu kama hicho kuwa kinakuja, ni kweli unavyosema vipindi kama hivi vya kabla ya tukio fulani huwa vina influence fulani kwenye maamuzi hasa ya kisheria.

Ila kwa nchi kama yetu ambayo si democractic kitu hicho huwa hakipo kwa vile tayari maamuzi huwa yameshafikiwa. Kwa mfano suala hili la pingamizi lilivyo ni dhahiri wengi kama siyo wote tunajua nini ambacho Tendwa ataongea ndiyo maana hata Chadema siku ya kwanza walitoa caution kama hiyo.

ITV na vyombo vya IPP wanajulikana kwa umangimeza, utakumbuka hata uchaguzi wa 1995 sikumoja kabla ya kupiga kura walituwekea picha za mapigano ya Rwanda, kwa hiyo sioni ajabu ila waelewe kwamba hata waandishi wa habari waliokuwa wana engineer vita vya Rwanda wakati huu wanajuta magerezani.
 
Kwani namba ya hicho kipindi chao kikiwa hewani ni ngapi au nizungumze na nani ili na mimi niwe mgeni wa kutoa mawazo yangu?
 
Kwanza ITV (CCM) wanaweza wasirushe watu hewani live yaani wa-filter kwanza "matusi"! tena kwa mtindo huu wa kujisajili namba wanaweza kukutafuta baadae UWT! heheheh Uhuru wa kujieleza huo!
 
Kwani namba ya hicho kipindi chao kikiwa hewani ni ngapi au nizungumze na nani ili na mimi niwe mgeni wa kutoa mawazo yangu?

Jamani mwenye namba ya kipindi hicho atupatie kabla ya hiyo kesho ili tuweze kujianda na maswali yetu... Maana wanaweza waka waanda watu wao... MM nikipata nitakutumia kwa SMS
 
Kwanza ITV (CCM) wanaweza wasirushe watu hewani live! tena kwa mtindo huu wa kujisajili namba wanaweza kukutafuta baadae UWT! heheheh Uhuru wa kujieleza huo!

Ili nalo linawezekana kabisa endapo watataka kufanya usanii
 
Ooh my God... Freemasons in the battle once again. Haven help our nation!!
 
Kama wao CCM watakua wamearifiwa kuchangia hoja kwa simu na nyinyi mnangoja nini kuchangia hoja zenu kwa kuisaidia chadema? Mmekalia chuki tu, siasa zenyewe hamzijui. Mimi ningewashauri kuelimisha umma juu ya KILIMO KWANZA, na kuachana na mambo ya siasa. Naimekuaje leo hii ITV inaegemea upande wa CCM wakati IPP na ITV na CHADEMA wanakula sahani moja? Na kuhusu pingamizi hilo ni la kawaida tu, pingamizi nyingi zimeshakuja kwa CCM na si za msingi, itakuaje pingamizi hilo liwe la kihistoria? Usiwe na hofu kaka. CCM ni chama makini, na imepita kwenye mambo mengi, CCM nambari 1!!!!!!
 
Kama wao CCM watakua wamearifiwa kuchangia hoja kwa simu na nyinyi mnangoja nini kuchangia hoja zenu kwa kuisaidia chadema? Mmekalia chuki tu, siasa zenyewe hamzijui. Mimi ningewashauri kuelimisha umma juu ya KILIMO KWANZA, na kuachana na mambo ya siasa. Naimekuaje leo hii ITV inaegemea upande wa CCM wakati IPP na ITV na CHADEMA wanakula sahani moja? Na kuhusu pingamizi hilo ni la kawaida tu, pingamizi nyingi zimeshakuja kwa CCM na si za msingi, itakuaje pingamizi hilo liwe la kihistoria? Usiwe na hofu kaka. CCM ni chama makini, na imepita kwenye mambo mengi, CCM nambari 1!!!!!!

We ni mgeni hapa na ni mgeni wa siasa naomba usichangie pumba hapa badala yake kaa pembeni soma mijadla ya great thinkers na ujifunze. Baada ya mwaka rudi uchangie utakuwa umeshajifunza.
 
Kwani namba ya hicho kipindi chao kikiwa hewani ni ngapi au nizungumze na nani ili na mimi niwe mgeni wa kutoa mawazo yangu?
Namba hutolewa wakati wa kipindi kikiwa hewani. wataonesha kwenye kioo cha TV yako shekhe. wala usihangaike kuitafuta mda huu maana wanaweza hata kubadili namba wale.
 
ITV(ccm) wamezidi kwa uzandinki

Kuna watu wataojiwa bila ya kupiga simu na watu hao wameandaliwa
upigaji wa simu unaweza kuwa controlled mana wapigaji simu watakuwa wanajulikana
 
Kama watakaokuwepo ni watu aina ya Palamagamba Sibudi, ntajua kabisa kimeandaliwa kuibeba CCM...
 
Kama kipindi hicho kweli kitaruhusu watu kupiga simu na kutoa maoni yao, ni vyema kujiandaa kwa kuisoma na kuielewa sheria hiyo kipengele kwa kipengele.

Naishauri CHADEMA ichukue hatua za kulinda haki yake ya kimsingi ili kipindi hicho isitumike kubadilisha maamuzi ya Msajili wa vyama vya siasa. Njia ninazopendekeza ni:

  1. Kuandaa wanasheria watakaokitathmini kipindi hicho ili kama kikikuika misingi ya sheria ITV ichukuliwe hatua
  2. Kujiandaa wenyewe kwa kuwa na watu watakaopiga simu na kutoa maoni yenye ufafanuzi wa kina
  3. Kuhakikisha kuwa madhara yoyote yanayoweza kutokea kutokana na kurushwa kwa kipindi hicho yanafanyiwa kazi, ili kuzua kupotea kwa haki
Itakuwa busara na haki kwa watanzania kama ITV itaheshimu haki za watu wote na kuepuka kupotosha sheria kadiri inavyowezekana. Njia ya kuhakikisha hilo, ni kutumia wanasheria mahiri wasio na upendeleo kwa upande wowote. Kama ikiwezekana, Mabere Marando na Tundu Lissu pia waalikwe ili ku-balance mjadala.

Ni ushauri tu.
 
Back
Top Bottom