Itikadi ya NCCR-Mageuzi: Katika Muhtasari

Msingi wa Endelezo:

Endelezo la Uhai na Raslimali (Maendeleo Endelevu)
  • Shughuli za kiutu za mtu ziko katika namna ambayo si ya madhara kwa uhai wa watu, viumbe wengine na chochote kilichomo katika mazingira/raslimali.


  • Tunahitaji maendeleo endelevu


  • Mtu mwenye utu, hachukulii udhuru wa mahitaji yake yatokanayo na mazingira kumfanya awe mharibifu wa kila kilichomo katika mazingira yake, bali mahitaji ya kiutu hutoshelezwa kwa namna ya kistaaarabu .


  • Hayawani wasio na utu, hawashangazi wanapokuwa wakatili katika harakati zao za kujitafutia mahitaji na wala hawatambui kama wanafanya ukatili. Chukulia mfano wa chui katika mbuga za Serengeti na kwingine,jinsi maisha yake yanavyoongozwa na sirika ya kuua takribani kila mnyama mnyonge anayekatiza mbele yake hata kama tayari amekwisha kupata kimtoshacho kwa ajili ya siku. Ataendelea kuua tu hata asivyovihitaji, na huo ndio uhayawani halisi.
Nukuu:"Earth provides enough to satisfy every man's need, but not every man's greed" (Mahatma Gandhi).

  • Mtu mwenye utu hawezi kufanya vitendo vya kimaendeleo bila kuzingatia manufaa yake kiutu.


  • Maendeleo ya viwanda na technolojia, kama ni ya madhara kwa watu, basi hayo si maendeleo ya kiutu bali matumizi ya kiayawani ya karama ya maarifa.


  • Ugunduzi wa technolojia sio ukamilifu wa mambo bali ukamilifu wake ni uboreshaji wa utu wamtu.

 
Fascinating! Ought to be examined on the extent to which it can stand spatial, temporal and praxis tests
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom