Itakuchukua Miaka Mingapi Upinzani kuja kushika Dola

Kwa sisi ni ngumu kwasababu Vyama vyetu vya Upinzani wapo/wako kimaigizo zaidi.

Kama wangekuwa na msimamo, na kuwa kitu kimoja bila mambo ya maigizo.

Nna hakika ingewezekana.

Ila kwa mwenendo wetu huu wa kiSIASA?! Abadan
 
Pohamba usiwe mnafiki kwa nafsi yako . Kikwete aliweka mazingira magumu ya kukubaliana, si neno hawakupata Katiba ya wananchi kipindi hicho Lakini CCM si Mungu kitafika kipindi Katiba na Tume huru vyote vitapatikana. Tanzania sio kisiwa

Wewe sio Mnafiki Ila hujui kuwa ukiingia kwny Mijadala yote iwe ya kiuchumi au Kisiasa lazima uwe na hoja zako mezani pia lazima ujipange kuwa Kama Nina hoja 5 basi Mwisho wa Mjadala tukishavutana naweza kubaki na tatu au mbili, na ukiona unaingia kwny Mjadala na hoja zako kadhaa na ukalazimisha zote zipite otherwise unasusa basi Jua kuwa huna utaalam wa Dialogue!

Fikiria CCM walikubali kuachia Tume huru, Kuhoji Mahakamani Matokeo ya Urais na wao wakakazia zibaki Serikali mbili sasa hapo Wapinzani walipaswa wajue wao ndio Washindi kwa kuwa katika hoja kuu tatu Mbili zimepita lakini kwa umaarufu wa Muda mfupi wakashauriane hata hayo mawili wasusie ili wapate yote matatu ( Serikali 3, Tume huru, kuhoji Matokeo ya Urais Mahakamani) na Matokeo yake wamekosa yote:

Miaka miwili imepita wanarudi kupigania Jambo moja la Tume huru sasa Wewe unaona Hilo ni sawa?

Jifunzeni kukubali kukosolewa, tuliandika sana kuwa mtaikumbuka sana fursa ya Tume huru mliyoichezea Leo kiko wapi?
 
Hata Kama Watu wameichoka CCM wanaendelea kuichagua kwa kuwa hakuna mbadala!

Hivi kweli Uchoke Ufisadi wa CCM umchague Lowassa?

Hivi kweli ukerwe na Ukwepaji wa Kodi umchague Mbowe?

Hivi kweli uchoke usanii wa CCM umchague Lipumba?

Hivi kweli uchoke ujanja ujanja wa CCM umchague Zitto?

Ni sawa na wale wanaoilaumu kila Siku Radio Clouds kuwa inanyonya Wasanii lakin ukitafuta Rafio isiyonyonya huioni.

Wapinzani watumie nguvu kubwa kuonesha kuwa wanafaa kuongoza Nchi sio kutumia nguvu zote kutuambia kuwa CCM haifai kwani si tunajua haifai?!,

Hivi kweli Unafunga Safari kutoka Mtaa Ufipa kwenda mpaka Ikungi Singida au Mbambabay Ruvuma kumwambia Mkulima kuwa Serikali imekutelekeza kwenye Baa la Njaa? (Yeye ndio wa kuwaambia Nyie kuwa katelekezwa sio Nyie kumwambia )

Tumieni Muda mwingi kueleza kwanini nyie mnafaa na sio kutumia Muda wote kuwaambia CCM haifai.
Kina wana point dunia hii balaaa...mkuu umeongea vema

Big up
 
Tumeona mifano ya Nchi kama Gambia,Ghana wao wameweza ila kule Uganda ni kinyume Mzee Besigye amepambana mpaka basi nasidhani kama ana hamu na siasa tena na kwa upande mwingine Zimbabwe Mzee Morgan Tsangirai nahisi hata Siasa hataki tena.

Kwa upande wa Jirani Zetu mzee Odinga Amejitahidi kufurukuta ila wapi.

NA hapa kwetu JE kuna siku kweli Upinzani utakuja kushika Dola au ndio Ndoto za Alinacha au baada ya miaka kama 100 hivi wakiwa na sera nzuri za kimaendeleo naza kueleweka na wanachi?
Mifano uliyotoa vipi tume zao za uchaguzi ni huru na za haki? chaguzi zao pia ni huru na za haki? The list goes on kwa nchi za kiafrika zenye kubadilishana madaraka na upinzani
 
Upinzani utakuchukua nchi siku ambayo!

1. Siku ambayo upinzani wataungana na kuwa kitu kimoja..

2. Siku upinzani watakapo acha unafiki na kuwa wakweli..mfano: lowassa akiwa ccm alikuwa fisadi ila alipoenda ukawa akawa msafi..

3.siku upinzani wataacha kuchumia tumbo na waweke utz mbele

4.siku wakieleza kwanini wao wanafaa na sio Taabu ingine
Siasa ni kama mchezo wa drafti au bao. Siku ukiwekwa ama kuingizwa kingi hitoki
 
Wewe sio Mnafiki Ila hujui kuwa ukiingia kwny Mijadala yote iwe ya kiuchumi au Kisiasa lazima uwe na hoja zako mezani pia lazima ujipange kuwa Kama Nina hoja 5 basi Mwisho wa Mjadala tukishavutana naweza kubaki na tatu au mbili, na ukiona unaingia kwny Mjadala na hoja zako kadhaa na ukalazimisha zote zipite otherwise unasusa basi Jua kuwa huna utaalam wa Dialogue!

Fikiria CCM walikubali kuachia Tume huru, Kuhoji Mahakamani Matokeo ya Urais na wao wakakazia zibaki Serikali mbili sasa hapo Wapinzani walipaswa wajue wao ndio Washindi kwa kuwa katika hoja kuu tatu Mbili zimepita lakini kwa umaarufu wa Muda mfupi wakashauriane hata hayo mawili wasusie ili wapate yote matatu ( Serikali 3, Tume huru, kuhoji Matokeo ya Urais Mahakamani) na Matokeo yake wamekosa yote:

Miaka miwili imepita wanarudi kupigania Jambo moja la Tume huru sasa Wewe unaona Hilo ni sawa?

Jifunzeni kukubali kukosolewa, tuliandika sana kuwa mtaikumbuka sana fursa ya Tume huru mliyoichezea Leo kiko wapi?
Watu.mnaufahamu mkubwa aisee napata vitu kusoma hoja zako
 
miaka 25 itatosha sana, watakaobahatka kuwepo 2045 watashuhuduia, hakka nawaambia
 
Upinzani watashika dola siku ambayo ccm itaweza kubadilisha mgombea kwa miaka mitano na siku 10
 
Tumeona mifano ya Nchi kama Gambia,Ghana wao wameweza ila kule Uganda ni kinyume Mzee Besigye amepambana mpaka basi nasidhani kama ana hamu na siasa tena na kwa upande mwingine Zimbabwe Mzee Morgan Tsangirai nahisi hata Siasa hataki tena.

Kwa upande wa Jirani Zetu mzee Odinga Amejitahidi kufurukuta ila wapi.

NA hapa kwetu JE kuna siku kweli Upinzani utakuja kushika Dola au ndio Ndoto za Alinacha au baada ya miaka kama 100 hivi wakiwa na sera nzuri za kimaendeleo naza kueleweka na wanachi?
Uchaguzi utakaofutia kuundwa kwa TUME huru ya uchaguzi ndio kadirio la upinzani kuweza kushika hatamu za uongoxi. Kama TUME huru itapatikana baada ya miaka 500,basi mwaka wa uchaguzi baada ya TUME huru CCM bye bye
 
Back
Top Bottom