It can only happen in Bongo.

uporoto01

JF-Expert Member
May 23, 2008
4,700
1,415
Juzi nilipokuwa naangalia habari ya saa 2 usiku ITV tulionyeshwa watu wakilalamika wilayani Sengerema mkoani Mwanza baada ya Tanroads kuweka mzani wa kupimia magari(weightbridge) kwenye barabara ya CHANGARAWE! Magari yalioonekana kuzidisha kipimo yalikua yanalipishwa faini kwa KUHARIBU barabara.Kote ulimwenguni kuna utaratibu wa kuzuia magari kuzidisha uzito kwenye barabara za lami na nchini ZAmbia niliona utaratibu wa magari mazito kwenye migodi ya shaba kutengenezewa barabara za changarawe kuepusha magari hayo kupita kwenya njia za lami.
 
Mkuu Lagat...., swala la kuweka mizani kwenye barabara za changarawe ni la kawaida sana. Kumbuka kuwa pamoja na kwamba inaonekana kwamba barabara za changarawe ni za kawaida (non-engineered) ukweli ni kwamba nazo pia zinatakiwa kufanyiwa matengenezo ya kawaida na pia zinatakiwa ziwe na aina flani ya kuzuia magari yenye uzito zaidi ya kiwango kuzitumia kupunguza "premature failure". Tuelewe kwamba hata barabara za changarawe pia zimefanyiwa uhakiki (design) kwa kufuata viwango na kanuni za barabara za Tanzania kama nchi. Kuna nchi kama Sudan, Uganda, Namibia, Msumbiji ambapo wana barabara za changarawe na wanafanya udhibiti wa uzito pia. Kwa hili lazima tukubali ukweli kuwa lazima uzito udhibitiwe!!
 
Morani,
Hapo tupo wote kabisa Mhanidisi wangu. Ndiyo maana huwa ninalaani wana siasa kuingilia mambo yasiyowahusu. Bahati muulizaji si mwana siasa maana angelikuwa Lowassa ingelikuwa kasheshe.
Jamani, hata barabara za changarawe zinajengwa. Zinawekewa mifereji ili maji yasiingie chini ya barabara na kuiharibu. Zinawekewa slope ili maji yatititike mapema (kama sikosei ni kwenye 6%). Hivyo hata hiyo ya changarawe ina hadhi zote za kuwa barabara kasoro tu ni kuwa juu yake haina Zage la lami au la cement.
 
Back
Top Bottom