Israel yaua wapalestina 100 wanaosubiri msaada wa chakula

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,505
51,106
Kama kawaida yao, ukishazoea kuua utaendelea kuua tu.

Wale wanaoitwa Taifa teule wameendelea na kazi yao ya kufanya wanachoweza kwa ufanisi mkubwa. Leo wameua wapalestina masikini 100, wasio na silaha, ambao wana njaa wakati wakisubiri msaada wa chakula. Wanajeshi wa Israel limefyatulia kundi la watu risasi na kuua wapalestina 100.

Haya yakiwa yanafanyika kuna watu wanafurahi, wanapenda, wanachekelea na wanatamani hawa wapalestina wasio na hatia wanedelee kuuawa

Taarifa za hilo tukio unaweza kuipata hapa:

Nchi iko vitani dhidi ya MAGAIDI, hao ni collateral death siyo murder. Taarifa za kiinteligensia zinasema walikuwa magaidi waliojichanganya na raia wanaosubiria msaada wa chakula, Ukizingatia magaidi hayana military uniform.

HAMAS, walisema wana pumzi ya kupigana muda mrefu, Israel ikawapelekea vita chumbani sasa wapigane vizuri. Wanapo ua Muisrael hata mmoja utasikia Allah Akbar kibao, sijui sasa hivi wanaongea nini huko.
 
Kwa nini Gaza iliishambulia Israeli na kuteka baadhi ya Wayahudi na hawataki kuwaachia?

Ni ujinga kuandika habari za kuegemea upande bila kuzitaja sababu za kwa nini mauwaji yanaendelea kati ya Palestine na Israel
Kama ni raia wema kwanini serikali yao haiwahamishii sehemu salama huko Palestina
 
Kwa nini Gaza iliishambulia Israeli na kuteka baadhi ya Wayahudi na hawataki kuwaachia?

Ni ujinga kuandika habari za kuegemea upande bila kuzitaja sababu za kwa nini mauwaji yanaendelea kati ya Palestine na Israel
Hamas ilishambulia sio Gaza, ni sawa na Al shabaab watulipue hapa Dar alafu eti twende Mogadishu tulipue mahospitali na mashule true watoto na wamama!! Sasa inahusiana nini?
 
Kitendo cha Israel kupeleka ndege na kuua watu wanaokaribia kufa kwa njaa wakisubiri chakula ni tangazo la wazi la kushindwa vita kwa taifa hilo la kiyahudi.

Ukiondoa ukimya wa mataifa ya kifalme ya kiarabu yanayoongozwa na watu kama mwanamfalme wa Saudia waliokaa kimya,viongozi wa nchi nyingi wamelaani kitendo hicho.

Jumla ya watu 112 tayari wametangazwa kufa katika shambulio hilo la ndege kaskazini ya Gaza.Watu wengine karibu 1000 wameumia vibaya katika shambulio hilo.

Idadi hiyo ya watu ilikuwa imejikushanya karibu na malori machache ya misaada wakati ndege za kivita ziliporuka juu yao na kuanza kuwadondoshea mabomu mazito juu yao.

1709269110284.png

Kama kawaida yao, ukishazoea kuua utaendelea kuua tu.
Wale wanaoitwa Taifa teule wameendelea na kazi yao ya kufanya wanachoweza kwa ufanisi mkubwa. Leo wameua wapalestina masikini 100, wasio na silaha, ambao wana njaa wakati wakisubiri msaada wa chakula. Wanajeshi wa Israel limefyatulia kundi la watu risasi na kuua wapalestina 100.
Haya yakiwa yanafanyika kuna watu wanafurahi, wanapenda, wanachekelea na wanatamani hawa wapalestina wasio na hatia wanedelee kuuawa

Taarifa za hilo tukio unaweza kuipata hapa:

View: https://www.youtube.com/watch?v=geGQHEiHZPw

Ni hatari, wapalestina wenye akili walishaonyesha kuipinga hamas, inatakiwa Hamas watangaza tumeshindwa vita tunaomba vita viishe na waachie mateka waliobakia ili vita viishe, na siyo kwamba nchi za kiarabu zimeshindwa kumsaidia Palestina, wangeweza lakini wanachoogopa ni kununua ugomvi, unaweza kuingia vitani kumsaidia itaonekana ndo ulimtuna hamas ashambulie Israel 7 Oktoba na kuteka, na inaonekana anasaidiana na hamasa kushikilia mateka, kosa lingine walilolifamyani kufanya maandamano ya kuwapongeza hamas baada ya kuushambulia Israel, kwa picha ile Israel alihisi nazungumza na maadui.
 
Waliyataka walipovamia Israel October 7 walitarajia nini?
Aljazira hawajawahi hata siku moja kutangaza kwamba wapiganaji wa Hamas wameuawa ila wanatangaza
1. Watoto na wanawake wameuwawa
2. Wanajeshi wa Israel wameuwawa
Maswali ya kujiuliza hao watoto na wanawake ndo wanapigana na Israel? Maana tunasikia tu ndio wameuwawa. Je Hamas wako wapi? Na wamekimbilia nchi gani? Na kwanini Arab league wasitoe jeshi na kwenda kuwasadia wapalestina wasiokuwa na hatia? Wanaogopa nini kupeleka jeshi? Kwa hiyo kati ya Allah na USA wanamuogopa nani? Wanaishia kusema Allah awape wepesi watu wa Ghaza, mara USA ndo anamsaidia Israel, je msada wa USA ni mkubwa kuliko Allah? Mbona Arab league wanaongea wasichokiishi? Baadhi ya nchi wameishia kuwasifu hamas huku watu wanaangamia.
 
Kwa nini Gaza iliishambulia Israeli na kuteka baadhi ya Wayahudi na hawataki kuwaachia?

Ni ujinga kuandika habari za kuegemea upande bila kuzitaja sababu za kwa nini mauwaji yanaendelea kati ya Palestine na Israel
Kung'ang"ania mateka ni mbinu ya kupunguza kushambuliwa sana na kuwa na sauti ya kutoa madai hata yasiyowezekana.
 
Back
Top Bottom