Israel toka 1948 na Jeshi la IDF

Tanzanite klm

JF-Expert Member
May 7, 2013
453
376
HISTORIA YA TAIFA LA ISRAEL TANGU 1948 NA VITA VITA KUU ILIZOPIGANA.
UTANGULIZI (softcopy iliyokamilika ipo sasa 3000 tsh pekee)

Katika karne ya 19 idadi kubwa ya Wayahudi waliishi katika maeneo kadhaa ya Milki ya Urusi yaliyotwaliwa na milki hiyo mnamo 1800.
Uadui dhidi ya Wayahudi ulitokea katika utawala wa Kirusi. Kuanzia mwaka 1880 kulitokea ghasia mbalimbali ambako Wayahudi walishambuliwa katika miji ya Urusi. Wimbi la pili la ghasia hizo zilizoitwa pogromu zilikatokea mwaka 1905, ambapo Wayahudi zaidi ya 2000 waliuawa mjini Odessa .

Wakati ule Wayahudi wa Urusi walianza kuhamia nje: wengi wao walikwenda Marekani, lakini wachache walielekea Palestina.
Mapogromu yalikuwa pia chanzo cha harakati mpya ya Uzayuni (Zionism) kati ya Wayahudi wa Ulaya. Uzayuni ulilenga kuwapa Wayahudi eneo maalum ili wapate kujenga upya taifa katika dola lao wenyewe, ambako wangekuwa wenyeji, si kundi la pekee katikati ya watu waliowadharau.

Mwaka 1896 Theodor Herzl (1860-1904) aliandika kitabu "Dola la Wayahudi" alimodai kuundwa dola la pekee kwa ajili ya Wayahudi. Mkutano wa kwanza wa wafuasi wake ulichagua jina la "zion" ambalo lilikuwa jina asilia la mlima wa hekalu mjini Yerusalemu; wakachagua jina hilo kwa sababu linataja mahali patakatifu zaidi pa Uyahudi.

Mkutano huo uliazimia kuwa "Uzayuni unalenga kuunda makazi salama yaliyokubaliwa rasmi kwa ajili ya taifa la Kiyahudi katika nchi ya Palestina".

Wazayuni walikusanya pesa kote Ulaya wakanunua ardhi katika Palestina na kuanzisha vijiji kwa ajili ya Wayahudi waliohima huko.
Palestina katika Milki ya Ottoman mwaka 1914

Vita ya Kwanza ya Dunia ilikwamisha mipango yote kwa sababu Palestina ilikuwa sehemu ya Milki ya Ottoman iliyoshiriki katika vita pamoja na Ujerumani na Austria dhidi ya Urusi, Ufaransa na Uingereza.

Mwaka 1917 wakati ambapo jeshi la Uingereza lilifaulu kusogea mbele kutoka Misri na kuingia Palestina, waziri wa mambo ya nje Arthur James Balfour alitoa tamko la Balfour yaani tamko rasmi kuwa Uingereza inataka kusaidia mipango ya kuanzisha makazi ya Kiyahudi katika Palestina. Wakati uleule Waingereza waliwaahidi Waarabu kuundwa kwa dola la Kiarabu kwenye maeneo yaliyokaliwa nao katika Milki ya Ottoman. Lakini wakati huohuo walipatana na Ufaransa kuhusu ugawaji wa maeneo ya Kiarabu ya Milki ya Ottoman.

Kwenye mkutano wa amani wa Paris wa mwaka 1919, ulioandaa Mkataba wa Versailles, mwakilishi wa Waarabu, Faisal bin Hussein bin Ali al-Hashimi, alipatana na mwakilishi wa Wazayuni, Chaim Weizmann, kuwa anakubali uhamisho wa Wayahudi kuja Palestina, na Palestina kuwa eneo la pekee tofauti na Dola la Waarabu ambayo Faisal alilenga kujenga Uarabuni pamoja na Syria na Irak. Haki za wakazi Waarabu zilitakiwa kulindwa na maendeleo ya pamoja kati ya wakazi Waarabu na Wayahudi kujengwa. Lakini Uingereza na Ufaransa

waliendelea kugawa Mashariki ya Kati, hivyo Waarabu wengi hawakuona ya kwamba mapatano ya Faisal yalikuwa na umuhimu tena.
Baada ya vita Uingereza ilichukua utawala wa Palestina kama eneo la kudhaminiwa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa(League of Nation). Idadi ya Wayahudi waliofika kutoka nchi za Ulaya iliongezeka, lakini bado Wayahudi wengi walihamia Marekani, si Palestina. Hata hivyo shirika za Uzayuni ziliendelea kununua ardhi, kuanzisha vijiji vya Ujamaa vilivyoitwa Kibbutz hata Tel Aviv ilikua kama mji wa Kiyahudi kandokando ya Yafo ya Kiarabu. Mnamo 1931 asilimia 17 ya wakazi wa Palestina walikuwa Wayahudi.

Katika Palestina mufti mkuu wa Yerusalemu, Mohammed Amin al-Husseini, alichukua uongozi wa Waarabu akapinga kufika kwa Wayahudi wapya. Serikali ya Kiingereza ilisitasita kuamua juu ya msimamo wake - haikuzuia kufika kwa Wayahudi, lakini haikuwasaidia kujiimarisha nchini. Mashambulio dhidi ya Wayahudi yalianza mwaka 1921. Mwaka 1929 Wayahudi 67 waliuawa mjini Hebron. Kati ya 1936 na 1939 kulitokea ghasia kubwa ya Waarabu dhidi ya polisi na jeshi la Kiingereza na dhidi ya makazi ya Wayahudi.

Uingereza ilifaulu kukandamiza ghasia hii kwa jeshi lake. Wayahudi walianzisha vikundi vyenye silaha vilivyolenga kutetea vijiji vya Kiyahudi na kulipiza kisasi kwa mashambulio. Vikundi hivyo viliendelea na baadaye kuwa chanzo cha jeshi la Israeli (IDF)

Siasa ya chuki dhidi ya Wayahudi iliyoendeshwa na Chama cha Nazi chini ya dikteta Adolf Hitler katika Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya iliongeza namba ya Wayahudi waliopaswa kuondoka Ulaya.

Baada ya mwaka 1933 takriban wakimbizi Wayahudi 250,000 walifika Palestina - hii ilikuwa sababu moja ya ghasia ya Waarabu dhidi ya Wayahudi miaka 1936-1939. Hadi mwaka 1945 Wayahudi walikuwa asilimia 33 ya wakazi wote wa Palestina.

Baada ya vita kuu ya pili kulikuwa na laki za Wayahudi waliowekwa huru kutoka makambi ya Kinazi na wengi wao walielekea Palestina. Hapo Serikali ya Uingereza, ilisita kuamua kama itekeleze ahadi zake kwa Waarabu au kwa Wayahudi, iliomba Umoja wa Mataifa uamue juu ya hatma ya Palestina, maana ilikuwa eneo la kudhaminiwa na lilikua chini ya uangalizi wa Uingereza na asili ya mamlaka hii ilikuwa imepitwa na wakati kwa sababu ilitokana na The league of Nation (Shirikisho la Mataifa )na sasa kulikuwa kumeanzishwa Umoja wa Mataifa (UN).

Kuundwa kwa Dola la Israeli

Mwaka 1947 Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ulipigia kura mpango wa ugawaji wa Palestina. Mataifa 33 yalipiga kura ya ndiyo, 13 hapana, 10 hayakusimama upande wowote. Hivyo eneo la Palestina lilitakiwa kugawiwa kwa dola la Kiyahudi na dola la Kiarabu . Mamlaka ya Uingereza yalitakiwa kwisha tarehe 14 Mei 1948.

Waarabu walipinga ugawaji kwa kudokeza ya kwamba mpango wa ugawaji haukuwa wa usawa kwa sababu zifuatazo-

Mosi ni kuwa mwaka 1947 Palestina ilikuwa na wakazi 1,845,000. Watu 1,237,000 au theluthi mbili walikuwa Waarabu, wakati watu 608,000 tu au theluthi moja walikuwa Wayahudi.

Pili ni kuwa kutokana na ugawaji wa ardhi dola la Kiyahudi lilitakiwa kupokea asilimia 56 cha ardhi, pamoja na maeneo yaliyofaa zaidi kwa kilimo ingawa mali ya Kiyahudi wakati ule ilikuwa asilimia 7 tu ya ardhi yote ya Palestina.

Tatu ni kuwa Katika eneo la Dola la Kiyahudi takriban 40% ya wakazi wangekuwa Waarabu. Sehemu kubwa ya ardhi katika sehemu ya Dola la Kiarabu ilikuwa mlimani na haikufaa vema kwa ajili ya kilimo.

Wawakilishi wa Kiyahudi walisema idadi ya Wayahudi itaongezeka haraka kutokana na uhamiaji wa Wayahudi wengine - wakati ule walikuwa bado laki za Wayahudi katika makambi kutoka nchi za Ulaya, ni hao ambao hawakuuawa na Wajerumani katika Holocaust.
Mara baada ya azimio la UN mapigano yalianza katika Palestina na kuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini. Vikundi vya wanamgambo wa Kiarabu vilishambulia makazi ya Kiyahudi kote nchini. Wayahudi pia walikuwa na vikundi vya wanamgambo.

Tarehe 14 Mei mkutano wa wawakilishi Wayahudi ulitangaza Dola la Israeli kama nchi mpya. Waingereza waliondoa jeshi lao.

Tarehe 15 Mei 1948 majeshi ya Misri, Yordani, Lebanoni, Syria na Irak yaliingia Palestina yakatwaa maeneo ya Kiarabu na kushambulia makazi ya Kiyahudi. Katika vita ya miezi 10 jeshi la Israeli lilifaulu kusimamisha wapinzani na kuwarudisha nyuma. Jeshi la Kiarabu pekee lenye uwezo lilikuwa Kikosi cha Jordani.

Wakati wa kusimamisha mapigano Israeli ilikuwa imeongezeka maeneo yake ikatawala asilimia 78 za eneo la kukabidhiwa la awali yaani maeneo yote yaliyowahi kukusudiwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Dola la Kiyahudi pamoja na nusu ya maeneo yaliyokusudiwa kwa ajili ya Dola la Kiarabu.

Ukanda wa Gaza ulitawaliwa na Misri na Ukingo wa Magharibi wa Yordani (mto) pamoja na mji wa kale wa Jerusalemu ukawa chini ya milki ya Jordani.

Zaidi ya wakazi Waarabu 700.000 walilazimika kuondoka au walimkimbia kutoka miji na vijiji vyao, wakikaa nje ya maeneo yaliyotawaliwa sasa na Israeli. Waarabu 150,000 hivi walibaki ndani ya maeneo haya sasa kama raia Waarabu wa Israeli. Baada ya vita Israeli ilikataa kurudi kwa waliokuwa nje. Ndiyo asili ya Wakimbizi Wapalestina wanaoishi Syria, Lebanoni, Yordani na Misri, pamoja na hao wanaoendelea kukaa katika makambi katika maeneo ya Gaza na Ukingo wa Magharibi.

Madola yote ya Waarabu isipokuwa milki ya Jordani yalikataa kuwapa wakimbizi hao haki za uraia, na kwa hiyo hadi leo wajukuu wamebaki kama wakimbizi katika nchi za kigeni bila uraia; wakisafiri wanatumia vitambulisho vilivyotolewa na UN, wanakosa haki ya kutafuta kazi au kushiriki katika siasa kama raia wa kawaida, hata kama familia zimeshaishi katika nchi hizo hadi kizazi cha tatu au nne.

Tangu kwa Isreal kujitangazia uhuru wake imekuwa ikiishi katika mazingira ya vita dhidi ya majirani zake kwa muda mrefu sana,imekuwa ikipigana vita vya mara kwa mara, lakini katika kitabu hiki nita chambua kwa kina vita zile kuu zilizopiganwa na Israel na majirani zake pia operesheni za kijeshi kubwa zilizowahi kufanywa na jeshi la israel ikiwepo
Vita ya uhuru ya 1948
 Dakika tisini entebe yaani 90 minutes at entebe,
 Vita ya Israel na Misri 1956
 Vita ya siku sita(six day war) ya mwaka 1967.
 Vita ya Yom Kippur ya 1973
 OPeration ya kuiba ndege ya mig ya kisoviet kutoka Iraq  Operation ya kulipua vinu vya nuclear vya Iraq
 Operation ya kulipua vinu vya nuclear vya Syria.

Baada ya vita ya 1948-1949 nchi jirani zilikataa kutambua dola la Israeli. Hali ya vita ikaendelea ingawa bila mapigano kati ya majeshi makubwa. Wanamgambo wa Wafedayin Wapalestina waliendelea kuvuka mpaka kutoka makambi ya wakimbizi na kushambulia vijiji vya Kiyahudi. Wanamgambo hao walipata mara nyingi silaha na mafunzo kutoka kwa majeshi ya Misri na Syria.

Vita ya 1948-1949 ilisababisha ghasia na mashambulio dhidi ya Wayahudi walioishi katika nchi za Kiarabu. Nchi kadhaa za Kiarabu ziliweka sheria za ubaguzi dhidi ya Wayahudi. Hivyo katika miaka baada ya kuundwa kwa Israeli karibu Wayahudi wote waliondoka au walifukuzwa katika nchi za Kiarabu na kufika kama wakimbizi katika Israel, Marekani au Ulaya. Jumla ya wakimbizi hao Wayahudi karibu ililingana na idadi ya Waarabu waliofukuzwa kutoka Palestina. Hivyo idadi ya wananchi Wayahudi wa Israeli iliongezeka sana.
Uhusiano mbaya kati ya Israeli na majirani Waarabu ulisababisha vita zaidi.

Mwaka 1956 Israeli ilishambulia Misri katika vita ya Suez kufuatana na mpango wa pamoja na Ufaransa na Uingereza baada ya kuona ununuzi wa silaha nyingi na Misri.

VITA VYA SIKU SITA.
Madai ya Waisraeli yanaanzia katika misingi ya kidini ambapo katika Biblia (kitabu kitakatifu kwa Wakristo na Wayahudi), kitabu cha kwanza cha nabii Musa kiitwacho Mwanzo sura ya 12 inaonesha jinsi Ibrahim anavyoitwa na mwenyezi Mungu ili kumtumikia.

Eneo hilo la Palestina (zamani lilijulikana kama Kaanani)ndiyo chimbuko la dini kuu tatu zenye msingi wa Ibrahim ambazo ni dini ya Wayahudi, Ukristo na baadaye Uislam.

Dini ya wayahudi yenye misingi ya Biblia Agano la Kale likianza na vitabu vitano vya Musa (Mwanzo, Kutoka, Hesabu, Mambo ya Walawi na Kumbukumbu la torati), Ukristo ukianza misingi kwenye Agano la Kale hadi Agano Jipya na Uislam ukishika vitabu vinne Tourat ya nabii Musa (a.s), Zabur ya nabii Dawood (a.s), Injili ya Issa bin Mariam (a.s.) au Yesu na Quran ya Muhamad (s.a.w)

Ibrahim mwenyeji wa Uru wa Ulkadayo (Mesopotamia) leo Iraq wa kabila la Waebrania anahama kutoka Iraq na kwenda Haran Syria na baadaye kutelemkia Kaanani (Uyahudi) ambapo Mwenyezi Mungu anamtokea katika njozi na kumwapia Ibrahimu kuwa ardhi yote hiyo amepewa yeye na uzao wake na kuahidiwa baraka yaani kubarikiwa kwa kila atakaye mbariki na kwamba jamaa zote za dunia zitajibarikia.

Pamoja na ahadi hiyo Mungu anamwambia nabii Ibrahimu kuwa uzao wake utakwenda utumwani Misri kwa miaka mia nne hadi kizazi cha nne ndipo watakapookolewa na kupandishwa Kaanani (Palestine).

Mizizi ya ugomvi huo inaanzia karne ya 19 wakati wa vuguvugu la utaifa la Uzayuni na Uarabu (Arab nationalism) vuguvugu la wayahudi (Jewish National Movement) lilianzishwa kuwa la kisiasa mwaka 1892 dhidi ya Urusi na Ulaya. Mkakati ulianza kwa wayahudi wote popote walipo kurejea katika nchi ya Palestina ambapo walipachukulia kuwa ndiyo nchi yao ya asili.

Katika kutimiza azma yao World Zionist Organization na Jewish National Fund walihimiza uhamiaji na kufadhili ununuzi wa ardhi chini ya utawala wa Ottoman na Uingereza katika Palestina.

Mgongano huo ukianzishwa na Uingereza kwa kile kilichafahamika kama Hussein-McMahon Correspondence na Balfour Declaration of 1917, na kufuatiwa na milipuko ya mapigano ya mara kwa mara kati ya Wayahudi na Waarabu katika eneo la Palestina.

Hakuna asiyekumbuka jinsi kiongozi wa Wanazi Adolf Hiltler alivyowafanyia wayahudi kwa maangamizi makuu ya Nazi Holocaust, ikiwa ni jitihada ya kulifuta taifa hilo..

Azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1947 liliridhia kugawanywa kwa nchi ya Palestina kwa wayahudi na wapalestina ambapo wayahudi walikubali na wapalestina wakiungwa mkono na Umoja wa Nchi za kiarabu wakikataa na kusababisha kuzuka vita baina yao.
Vita hivyo viliwafanya wapalestina kuhama na kukimbilia nchi jirani za kiarabu wakiwa wakimbizi yaani Al-Naqba.

Israeli ilijitangazia uhuru wake Mei 14 mwaka 1948 kufuatia uhuru huo mataifa ya kiarabu Misri, Lebanon, Syria, Jordan na Iraq yaliivamia Israeli na kuzuka vita ya iliyojulikana kama 1948 Arab-Israel war. Israeli iliibuka kidedea ikiyateka maeneo zaidi ya ramani ya awali na kugawa mji wa Yerusalem.

Mwaka 1964 wapalestina walianzisha chama cha Palestinian Liberation Organization (PLO) ambacho hakikutambuliwa na Israeli.
Katika vita vya Siku Sita 1967 vya Israeli na waarabu ambavyo Israeli ilishinda kwa kishindo ikiacha hasara kubwa kwa maadui zake viliifanya nchi hiyo kujiongezea ukubwa mara tatu ya ule wa awali.

Siri ya ushindi wa vita hivyo ulitokana na mbinu na maandalizi mazuri yaliyokuwa yamefanywa na hasa ni kule kuvamia kabla ya adui hajakushambulia. Kama wangesubiri washambuliwe basi Israeli ingefutwa katika ramani ya dunia kama waarabu walivyokuwa wameazimia.

Vita hiyo ya 1967 Israeli ilipigana na Misri, Syria, Lebanon, Jordan zikisaidiwa kijeshi na Sudani, Iraq, Algeria nchi zilizopeleka askari na silaha, Urusi ikisaidia mataifa hayo kwa wingi wa silaha. Kabla ya vita mataifa ya Marekani, Uingereza na Ufaransa yalipeleka silaha kwa Israeli na kuifanya isiwe na wasiwasi katika matumizi ya silaha.

Nini chanzo cha vita hiyo? Israeli na majirani zake walikuwa wakiishi katika hali ya uhasama tangu 1948 baada ya azimio la umoja wa mataifa la mwaka1947, lililoamuru kugawanywa kwa nchi hiyo, waarabu walikuwa bado wanayo hasira juu ya uwepo wa taifa hilo mashariki ya kati. Viongozi mbalimbali wa nchi za kiarabu waliazimia kuifuta Israeli kwenye ramani ya dunia.

Israeli iligombana na Syria ilipoanza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji kuyatoa mto Jordan na kusambaza katika nchi hiyo. Jeshi la Syria likatumia milima/miinuko ya Golan ilinayopata futi 3000 juu ya Galilaya kushambulia vijiji na mashamba.

Mashumbulio ya Syria yaliongezeka sana mwaka 1965 -66, Israeli ikilalamika Umoja wa Mataifa ambao ulisisitiza kuacha mapigano bila kuchukua hatua yoyote kwa Syria ambapo hata ulipotoa azimio la kulaani mashambulizi hayo yalipingwa kwa kura ya veto na Urusi.
Mashambulizi hayo yalienda sanjali na vitendo vya kigaidi dhidi ya taifa hilo ambapo mwaka 1965 Rais wa Misri Gamal Abdel Nasser alisema “hatutaingia Palestina nchi ikiwa imefunikwa kwa mchanga bali damu”. Baada ya miezi michache Nasser alisema tena kuwa azma ya waarabu ni kuona wapalestina wanakombolewa, kwa kifupi ni kuiondoa dola ya kiyahudi kwa maangamizi.

Aprili 7, 1967 Syria ikitumia ndege aina ya MiG21 ilizokuwa imepewa na Urusi ilishambulia vijiji (kibbutzim) kutokea Miinuko ya Golan, Jeshi la Israeli lilitungua ndege sita za Syria.

Urusi iliipa taarifa isiyo sahihi Syria kuwa Israeli inajiandaa kwa vita licha ya Israel kukanusha lakini Syria ilijipanga ikiweka makubaliano ya ushirikiano na Misri.

Tarehe 15 Mei, 1967 siku ya uhuru wa Israeli, majeshi ya Misri yalivuka kuelekea Sinai karibu na mpaka na Israeli ambapo siku tatu baadaye tarehe 18 jeshi la Syria likajipanga kwa vita katika milima ya Golan.

Baada ya majeshi ya Misri na Syria kujipanga kwa vita, Gamal Abdel Nasser aliamuru jeshi la umoja wa mataifa UN Emergency Force (UNEF), lililokuwa Sinai likiikinga Israeli tangu 1956 kuondoka mara moja bila kushirikisha umoja huo.

Mei 22, Misri ilifunga mlango bahari wa Tiran na kuzuia meli zote za kutoka mashariki kuingia Israeli na kuzuia meli za Iran zilizokuwa zinapeleka mafuta ya petroli na kuifanya nchi hiyo kutokuwa na njia inayopitika (uamuzi wa Misri ulikiuka sheria za kimataifa).

Radio Sauti ya Waarabu ikisema “kwa kuwa sasa jeshi la kimataifa lililokuwa linaikinga Israeli limeondoka hatutavumilia zaidi wala kulalamika umoja wa mataifa ila jambo moja tutakalofanya ni kuipiga vita na kutokomeza siasa za kizayuni”.

Naye waziri wa ulinzi wa Syria Hafez Assad alisema “majeshi yetu yako tayari kuifuta Israeli” nukuu kwa kimombo ‘Our forces are now entirely ready not only to repulse the aggression, but to initiate the act of liberation itself, and to explode the Zionist presence in the Arab homeland. The Syrian army, with its finger on the trigger, is united....I, as a military man, believe that the time has come to enter into a battle of annihilation” alisema hayo Mei 20, 1967.

Rais wa Marekani Johnson alilaani na kusema kitendo cha Misri ni kinyume na sheria ya bahari iliyopitiwa mwaka 1958 ambapo umoja wa mataifa ulitambua haki ya Israeli kutumia mlango bahari wa Tiran (Straits of Tiran) kupitisha meli.

Nasser aliendelea na vitisho akiitaka Israeli kuingia vitani akidai kuwa hawatasikiliza shauri lolote la masikilizano kwani wao wako vitani na Israeli tangu mwaka 1948. Aliongeza kusema kuwa majeshi ya Misri, Jordan, Syria na Lebanon yametulia mipakani mwa Israeli na nyuma yao yapo majeshi ya Iraq, Algeria, Kuwait, Sudan, Saudi Arabia na ulimwengu wote wa kiarabu. Alijigamba zaidi kwa kusema kwa tendo hili dunia yote itastaajabia na kujua kuwa waarabu wapo wamejizatiti kwa vita.

Rais wa Iraq Abdur Rahman Aref alisema “Uwepo wa taifa la Israeli ni kosa ambalo ni lazima lirekebishwe, huu ni wakati wa kufuta aibu ambayo tumekuwa nayo tangu 1948, lengo letu ni kuifuta Israeli kwenye ramani”. Iraq ilipeleka majeshi yake Juni 4 kujiunga na Misri, Jordan na Syria.

Majeshi ya kiarabu yanayokadiliwa askari 465,000, zaidi ya vifaru 2,800, na ndege 800 viliizunguka Israeli. Kipindi hicho Israeli ilikuwa kwenye hali ya tahadhari kwa wiki tatu muda huo iliutumia kuingiza silaha toka mataifa ya magharibi Marekani, Ufaransa na Uingereza. Silaha zilishushwa katika mji wenye bandari wa Haifa.

Israeli kwa kuwafahamu adui zake walivyo waliwafanyia kamchezo ka hadaa, kwanza ilifungua mpaka wake na Misri ili kuruhusu wapelelezi wa Misri kuingia na kutoka. Pili oparesheni ya kuhamisha silaha zilizowasili katika mji wa Haifa wakazipeleka ghuba ya Aqaba eneo lenye pori na miamba wakati wa mchana na kuzirudisha Haifa usiku na kuzihifadhi kwenye mahandaki. Jambo jingine lililowasaidia Israeli ni hadaa iliyofanywa, Waarabu walipotangaza vita na kuitisha Israeli, iliwaita makamanda wote waliokuwa likizo kurudi kazini na mawaziri waliokuwa ziarani kurudi mara moja, jambo lililofanywa na Misri pia.

Baada ya wiki hizo tatu za maandalizi ya nguvu Israeli ikatangaza kuwa makamanda waliokuwa likizo waendelee na likizo zao inaonesha waarabu walikuwa wanawatisha tu hakutakuwa na vita.

Kipindi hicho Marekani ilijaribu kuzuia vita kwa kuishauri Misri kusitisha mpango wa vita lakini haikuwezekana kumshauri raisi wa Misri Gamal Abde Nasser hali iliyomfanya Rais wa Marekani Johnson kuonya kuwa “Israeli haitakuwa pekee vitani labda ikitaka kuwa hivyo”
Juni 5, 1967 waziri mkuu wa Israeli Levi Eshkol aliamuru kuishambulia Misri, hapo Israeli ilikuwa peke yake, lakini yenye makamanda waliojizatiti kwa mkakati maalum. Jeshi lote la anga la Israeli ukiacha ndege 12 tu ziliachwa kulinda anga la Israeli, majira ya saa 1.14 asubuhi (saa moja asubuhi) walipiga mabomu viwanja vyote vya ndege za kivita vya Misri wakati marubani wa ndege hizo wakipata kifungua kinywa.

Ndani ya masaa mawili ndege 300 za Misri zilikuwa zimeshapigwa mabomu na kuharibiwa kabisa, masaa machache baadaye ndege za Israeli zilishambulia majeshi ya anga ya Jordan na Syria na kiwanja kimoja cha Iraq.

Jioni ya siku ya kwanza ya vita ndege zote za Misri na Jordan na nusu ya ndege za Syria zilikuwa zimeharibiwa zikiwa viwanjani. (ujanja wa kuzipiga zikiwa kwenye hanger kabla hazijaruka ulitumika).

Misri iliyokuwa na nguvu za kijeshi na jeshi kubwa la ardhini lenye vifaru na magari ya vita ilianza matayarisho ya kuyavusha kwenye mfereji wa Suez (madarajani) likafauru kuvusha askari 20,000 hadi penisula ya Sinai.

Israel ikiwa inaangalia mwenendo wote wa majeshi ya Misri iliacha operesheni hiyo ifanyike ya uvushaji askari na silaha kuelekea Sinai na kisha ikatuma ndege zake kuvunja madaraja ya Suez na kuhakikisha hakuna msaada wa kijeshi wala chakula utakaovuka kusaidia kikosi kilichokwisha vuka.

Kisha vilianza vita vya ardhini ambapo mapigano makubwa ya kihistoria ya vifaru yalitokea baina ya majeshi ya Misri na Israeli katika jangwa la Sinai.

Baada ya Jordan kushambuliwa wapalestina wapatao 325,000 walioishi Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan walilazimika kukimbia na kwenda nchini Jordan kuepuka vita.

Kikosi kidogo cha mashujaa wa Israeli kiliwekwa kuzuia majeshi ya Syria wakati vita vikali vikiendelea baina ya Israeli na Misri na Jordan hadi walipoona wamedhoofisha majeshi hayo ndipo kikosi kizima cha jeshi la anga kiliposhambulia ngome ya Syria kwenye milima Golan, Juni 9, baada ya siku mbili za mashumbulizi ya nguvu (heavy bombardment) walifaulu kupenya safu ya Syria.

Baada ya siku sita za mapigano Israeli ilikuwa na uwezo wa kuingia Cairo, Damascus na Amman bila kikwazo, wakati huo lengo la kuiteka Sinai na Miinuko ya Golan lilikuwa limefikiwa. Viongozi wa Israeli hawakuwa na nia ya kupiga miji mikuu ya nchi hizo, jambo ambalo walikuwa na uwezo nalo.

Zaidi ya hayo Urusi ikiwa imechanganyikiwa na mafanikio ya Israeli ikawa inatishia kuingilia vita. Wakati huo waziri wa Mambo ya nje (Secretary of State kama wanavyomwita) wa Marekani Dean Rusk aliishauri Israeli kukubali wito wa kusimamisha mapigano, Israeli ilikubali Juni 10 ilisimamisha mapigano.

Ushindi wa Israeli uliigharimu. Katika kushambulia milima ya Golan wanajeshi 115 wa Israeli walipoteza maisha ikipoteza ndege 46 kati ya 200 wakati upande wa waarabu Misri askari 15,000, Syria 2500 na Jordan 800.

Mwisho wa vita Israeli ilikuwa imejiongezea ukubwa wa eneo mara tatu kutoka maili za mraba 8000 hadi 26,000, ushindi huo uliifanya Israeli kuutwaa mji wa Yerusalem, mkondo bahari wa Sinai, Golan Heights, Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.
Licha ya vita hiyo Israeli iliwashauri wapalestina kuendelea kuishi chini ya utawala wa Israeli ambapo baadhi ya familia za wapalestina zilizokuwa zimetengana waliweza kuungana na wengine hawakuwa na imani na Israeli.

Mwezi Novemba 1967, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio na 242 lililowataka Israeli na Waarabu kuwa na amani ambapo Israeli ilitakiwa kuondoka katika Ardhi ilizoteka kwa makubaliano ya kuwa na amani na majirani zake.

Mwandishi maarufu wa habari za Waarabu katika Israeli Don Peretz aliyetembelea Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan siku chache baada ya vita alithibitisha kuona jinsi Israeli ilivyojitahidi kurejesha hali ya kawaida ya maisha na kuzuia kuhama kwa waarabu maeneo hayo.

VITA YA TATU YA ISREAL NA WAARABU INAYOJULIKANA KAMA YOM KIPUR WAR.
06-10-1973 nchi za kiarabu zilijipanga vilivyo ili tu kurejesha ardhi zao walizopoteza katika vita vilivyovunja record ya Dunia vita vilivyopiganwa kati ya nchi za Ki-arabu na Israel kwa mda wa siku sita Mwaka 1967 na majeshi ya nchi za Ki-arabu kusalimu Amri na kuacha ardhi zao kutekwa na askari wao kwa mamia kupoteza maisha yao na Maelfu kutekwa.

Vita hii iliacha maumivu na makovu makubwa sana katika ulimwengu wa Kiarabu hata kupelekea nchi hizo hasa Misri na syria kuanza mikakati ya kukomboa ardhi zao zilizotekwa na Majeshi ya Israel,kwa maana syria milima ya Ki-mbinu ya Golan ilikuwa imetekwa na kwa upande wa Misri ilipoteza Jangwa lote la sinai ikiwa pamoja na Mfereji wa Suez nchi hizi zilikuwa na machungu sana hasa ikichukuliwa kuwa nchi iliyowashinda ni ndogo sana hivyo mipango iliyofanywa mwaka 1973 ni kuzikomboa ardhi zilizotekwa baadaye kuifutilia mbali Israel katika uso wa Dunia.

Mipango ya kuivamia Israel ilipangwa ifanyike siku ya Jumamosi ambapo kulikuwa na sikukuu ya Kiyahudi inayojulikana kama YOM-KIPPUR,Siku hiyo Israel ilipata changamoto kubwa ambayo katika historia ya nchi hiyo Kivita haijawahi kutokea, maana siku hiyo Maelfu ya vifaru na Makumi elfu ya Majeshi na ndege za kijeshi zilifanya shambulizi la kushitukiza na kwa pamoja katika mipaka ya Israel ya kusini na kaskazini hii ilikuwa Ishara tosha kuwa Syria na Misri zilikuwa zinataka kurudisha ardhi zao zilizotekwa katika vita vya siku sita vya mwaka 1967.

CHANZO CHA VITA YA YOM-KIPPUR.
Baada ya Israel kushinda vita vya 1967 Israel ilipata ardhi kubwa ambayo ilipaswa kulindwa kwa gharama yoyote ili kupata Muafaka wa kisiasa kati ya nchi hiyo na nchi za Kiarabu kwa upande wa Misri Israel ilichukua Sinai na Suez canal hivyo Jeshi la Israel lilipata changamoto kubwa sana kulinda mpaka wote wa sinai na Mfereji wa Suez,Majeshi ya Israel yaliweka vituo vya ulinzi vilivyojulikana kama BAR-LEV line, na kwa upande wa Syria Israel ilichukua Milima ya Golan ambayo kwa Israel lilikuwa eneo jipya lililotakiwa kulindwa kwa nguvu zote maana Ki-Jeshi lilikuwa ni strategic la kimbinu sana Maana milima hiyo ya Golan iko kwenye mwinuko kwa hiyo eneo hilo likishikiliwa na Syria ina maana Majeshi ya Syria yana Uwezo wa kumiliki Kijeshi ndani ya Israel kilomita zaidi ya 25 na wakati huohuo Israel haingekuwa na uwezo wa kupata target Shabaha nzuri kupiga majeshi ya Syria yaliyoko kwenye milima hiyo ya Golan na ndiyo maana

mpaka leo Israel haiwezi kuiachia milima hiyo maana kufanya hivyo ni sawa na kujitoa MHANGA kwa jeshi la Israel,Badala yake Inataka kuirudisha milima hiyo kwa kubadilisha na AMANI na Syria ili wawekeane mkataba wa AMANI na kutoshambuliana na Israel ili iweze kupata uhakika wa kutoshambuliwa toka milima hiyo ya Golan.

Baada ya vita vya 1967 Msri na Syria zilianza kujenga majeshi yao ili waweze kukomboa ardhi zao zilizotekwa, Nchi hizo zilihitaji zana za kivita zaa kisasa ili kuweza kummaliza adui yao Israel walihitaji sana kupata silaha toka Urusi wakati huo USSR. Walihitaji kupata Ndege aina ya MIG na vifaru aina ya T-62 Vilevile makombora ya kuangushia ndege aina ya SA-2,3,6 na SA-7 pamoja na silaha za kubomolea Vifaru aina ya SAGGER ANT-TANK GUIDED MISSILES.

Kufikia mwezi October 1972 Rais wa misri wakati huo Anwar Sadat aliwahi kuongea na makamanda wake kuhusu kuishambulia israel na ilipofikia mwezi may 1973 vyombo vya kijasusi vya Israel vilikuwa vimepata habari kuwa Misri itaishambulia Israel kupitia mfereji wa Suez Misri walikuwa wanajua kuwa kama Misri itaishambulia Israel basi Syria nayo ingejiunga na kuishambulia Israel kutokea Kaskazini. Vilevile Israel walidaganyika kuwa Misri itaishambulia Israel mara tu itakapopokea ndege aina ya MIG-23 na SCUD-D toka Urusi Jeshi la Israel lilijua kuwa Misri haijapokea silaha hizo toka Urusi hivyo iliamini Misri haiwezi kuanzisha vita hivyo kabla ya kupokea silaha hizo toka Urusi.

Mwezi May na Mwezi August 1973 Majeshi ya Misri yalifanya mazoezi makubwa ya kijeshi katika eneo la mpaka na Israel,Israel nayo ilipoona hivyo ilianza kukusanya askari wake kwa maandalizi ya vita lakini baada ya pale hakukuwa na harakati zingine za kijeshi katika eneo hilo la mpaka hivyo Jeshi la Israel liliona kuwa hiyo ilikuwa kawaida tu yaani waliona kama yalikuwa mazoezi ya kawaida tu.

Septemba 25,1973 Mfalme hussein wakati huo alikutana na waziri mkuu wa Israel wakati huo Mama Gold Meir wakati huo Mfalme Hussein alishakutana na Rais Sadat na Assad wa Syria na alimwonya waziri mkuu wa Israel kuhusiana na kukalia eneo la Syria la milima ya Golan na Sinai eneo la Misri,Baada ya kumalizika kikao hicho na Mfalme Hussein waziri mkuu wa Israel pamoja na waziri wa ulinzi wa Israel wakati huo MOSHE DAYAN pamoja na vyombo vya Kijasusi vya Israel waligundua moja kwa moja kuwa Misri ingewashambulia wakati wowote.

Masaa machache tu kabla ya Misri kuishambulia Israel tarehe 06-10-1973 waziri mkuu Golda Meir na waziri wa Ulinzi Moshe Dayan na Mkuu wa utawala jeshini Gen.David Elazar kwa pamoja waliamua kuwaita wanajeshi wa anga wale wa akiba na wale wa vifaru wale wa akiba maana walijua hapo sasa vita haiepukiki.

Kabla ya vita siku hiyo majeshi ya pande zote mbili yalikuwa na zana zilizokuwa zinakisiwa kuwa hivi:
ISRAEL
WAARABU
NDEGE VITA
358
998
VIFARU
2100
4350
MELI VITA
37
137
Ilipofika saa nane kamili mchana majeshi ya Msri na yale ya Syria yalianza kumimina makombora kuelekea katika sehemu zilizokuwa zinakaliwa na Israel,Misri na Syria zilichagua siku ya jumanosi maana ilikuwa ni sikukuu ya kiyahudi ya YOM KIPPUR waliona siku hiyo wayahudi wote huwa wanasherehekea hivyo ilikuwa upenyo mzuri sana kwao.

Kwa upande wa Sinai majeshi ya Msri yaliweza kuvuka mfereji wa Suez kupitia sehem tano tofauti na kwa upande wa mizinga Misri iliweza kukipiga kituo cha wanaanga wa Israel waliokuwa Refidim katika jangwa la sinai na vikosi vingine vya mizinga vya Israel vilishasmbuliwa na mizinga ya Misri,na kufikia saa 11 jioni maelfu ya Wanajeshi wa misri walikuwa wamefika upande na kulikamata eneo lote la mashariki mwa mfereji wa Suez na wakati wa usiku vikosi vya vifaru vilivuka mfereji wa Suez hapo ndipo hali ya uwanja wa vita ilibadirika kabisa kwa Israel uwepo wa askari wa miguu wa Israel na mizinga yao hakukuweza kuyasimamisha majeshi ya Misri. Division ya 252 na Brigedi ya 14 ya kikosi cha vifaru viliadhirika vibaya sana asilimia kubwa ya vifaru vyao vilikuwa vimeangamizwa na silaha aina ya SAGGER ANT-TANK GUIDED MISSILES toka Misri.

Jeshi la anga la Israel lilipoitwa ili kudhibiti majeshi ya Misri,Ndege hizo zilijikuta zinaangushwa na mizinga ya kuangushia ndege, Misri iliweza kuzitungua ndege za Israel kiasi cha kuzimalizia uwezo wa kushambulia na baada ya kujipanga vizuri na kujua namna ya kukwepa makombora ya kuangushia ndege aina ya SA-7 ndege za Israel ziliweza kuziangamiza helcopter zilizokuwa zimebeba Makamandoo wa misri na kuweza kuzitungua ndege 7 aina ya MIG kwenye uwanja wa mapambano. mapambano hayo yalifanyika kusini mwa mfereji wa Suez ndege hizo ziliangushwa na ndege za Israel aina ya PHANTOM.

Kwa upande wa milima ya Golani majeshi ya Syria yaliweza kusonga mbele huku mizinga na vifaru pamoja na askari wa miguu waliweza kumiminia mizinga,risasi majeshi ya Israel kwa saa nzima mfululizo wakati huo Israel ilikuwa na Brigedi mbili za vifaru Division ya 36th ndiyo ilikuwa mstari wa mbele na Brigedi 188th nayo ilikuwa na jukumu la kulinda sehemu ya kusini ya mlima wa Golani na Brigedi ya 7th ilikuwa na jukumu la kulinda sehemu ya kaskazin mwa mlima Golan hivyo vifaru vya Israel havikuweza kuvishambulia vikosi vya Syria sababu havikuwa kwenye RANGE ya kuweza kushambuliwa.

Mapigano ya vifaru yalianza tu siku hiyo baada ya jua kuzama majeshi ya Syria yaliweza kupenya ngome za Majeshi ya Israel kwa kuwa walikuwa wanatumia NIGHT-VISION viona usiku hivyo vilisaidia sana majeshi ya vifaru vya Syria vifaru vya Israel vilivyokuwa upande wa kaskazini havikuweza kufua dafu mbele ya vikosi vya Syria,vifaru vya Syria viliweza kushika sehemu ya kusini mwa mlima Golan na ilipofika asubuhi ya tarehe 07-10-1973 vifaru zaidi ya 600 vilikuwa vimeingia ndani ya ardhi ya Israel na vilikimbilia kwenda kulishika Daraja mhimu la mto Jordan na kambi ya kijeshi ya Nafar,Israel pia ilipoteza mlima wa HELMON ambao ulikuwa wa kimbinu strategic nao uliangukia mikononi mwa majeshi ya Syria hili lilikuwa pigo kubwa kwa majeshi ya Israel.

Kwa upande wa majini majeshi ya Israel yaliweza kuziangamiza boat zilizokuwa zinabeba makombora za Syria na miji yote iliyokuwa inazunguka milima ya Golan wakazi wake waliondolewa na majeshi ya Israel.na baada ya siku 18 Majeshi ya Israel yaliweza kujijenga upya na kuchukua tena eneo lote la milima ya Golan na mlima Hermon

Kwa upande wa milima ya Golan peke yake vifaru vya Israel vilipambana na vifaru 1400 vya Syria na kwa upande wa Misri eneo la mfereji wa Suez Wanajeshi wa Israel 500 waliweza kupambana na wanajeshi 80,000 wa Misri.

Israel wakati huo ilipata msaada wa kijeshi toka Marekani pia ilipewa nyaraka mhimu zenye upelezi na nyaraka zilizokuwa zinaonyesha kuhusu ndege ya kipelelezi ya Marekani SR-71 Blackbird ndege ambayo iliweza kuwaonyesha ni wapi walipo askari wengi wa Misri maana ndege hiyo ilikuwa inaruka kipindi chote cha vita hiyo kwa msaada wa ndege hiyo Wanajeshi wa Israel waliweza kuvishinda vikosi vya Misri waliona sehemu inayoelekea Ismailia haikuwa na askari wa kutosha hivyo walipeleka huko vikosi vya vifaru na kuweza kuvishinda vikosi hivyo na kuanza safari ya kuelekea Cairo kirahisi sana.

Kwa Upande wa Misaada ya kijeshi Misri na Syria zilipata misaada kutoka katika nchi za kiarabu kama Ifuatavyo;
  • Iraq yenyewe ilituma kikosi cha ndege za kivita aina ya Hunter jet fighter kwa majeshi ya Misri miezi michache kabla ya vita kuanza vilevile Iraq ilitoa ndege za kirusi aina ya Mig na askari wa miguu 18,000
  • Saudi Arabia pamoja na Kuwait wao walifadhiri vita hivi pamoja na saudi Arabia kutoa askari wa miguu 3,000 ambao walipigana vita. Libya nayo ilitoa ndege za kivita aina ya Mirage zilizotengenezwa Ufaransa vilevile Libya ilitoa Dola za kimarekani Bilion moja ili kuliunda upya jeshi la Misri na kununuli zana za kivita za kisasa toka Urusi.
  • Nchi nyingine zilizosaidia Misri na Syria katika vita hivi ni pamoja na Tunisia,Sudan, Morocco na Jordan pia ilituma Brigedi mbili za vifaru na vikosi viwili vya Mizinga kusaidia Syria.

Majeshi ya Israel katika mapambano hayo mwanzoni ilionekana kuzidiwa sana katika viwanja vyote vya mapigano na ilipofika 08-10-1973 Israel iliwaita askari wote wa akiba na kuwapeleka kushambulia katika jangwa la Sinai siku hiyo walifanikiwa kuyarudisha nyuma Majeshi ya Misri na kuvuka mfereji wa Suez kusini mwa mji wa Ismailia hapo Majeshi ya Israel yaliweza kusonga Mbele kupitia Barabara ya Suez kwenda Cairo Majeshi hayo ya Israel yaliweza kusonga mbele kuelekea Cairo mpaka walibakiza maili 65 kufika Cairo.

Kwa upande wa Syria Majeshi ya Israel yalipata mafanikio katika milima ya Golan ambapo Majeshi ya Syria yaliweza kurudishwa nyuma na Israel iliweza kuzikamata tena sehemu zilizokuwa zimetekwa na Syria wakitumia Barabara inayotoka Tiberia kwenda Damascus Majeshi ya Israel yalibakiza maili 35 kufika mji mkuu wa Syria.

Tarehe 24-10-1973 juhudi za kusimamisha mapigano zilianzishwa na Umoja wa mataifa na Umoja wa mataifa ulituma walinda Amani katika sehemu kulikokuwa kuna mapigano na kufikia kati ya mwezi January na March 1974 Israel na Misri zilikuwa zimeweka mkataba wa kusimamisha mapigano kwenye eneo la Mfereji wa Suez hapa Israel iliweza kubaki na kulidhibiti eneo la Kimbinu (strategic) katika Jangwa la Sinai ambalo majeshi yake yanaweza kuona kwa mbali nakuweza kuzuia kama mapigano yatazuka tena katika eneo hilo.

Katika milima ya Golan askari wa kulinda Amani 1200 waliwekwa huko mwezi May 1974 na kuweka eneo lisilo la kijeshi kati ya Israel na Syria.Henry kissenger ndiye aliyekuwa anayaongoza mazungumzo hayo ya Amani,kufikia September 1975 Misri na Israel waliwekeana mkataba wa Amani na kuahidi kumaliza tofauti zao Kisiasa na si Kijeshi na hii ilipelekea kuanzishwa Mazungumzo yaliyokuja kujulikana kama Mazungumzo ya Camp David.

Rais wa Misri Anwar Sadat alipoona Majeshi ya Israel yanaelekea Cairo hakika aliona mambo yanaenda kuwa Magumu hasa akiangalia nguvu waliyotumia na misaada waliyopewa na nchi za kiarabu aliamua kwa Moyo mmoja kuachana na nchi zingine ili tu iwepo Amani maana wametumia nguvu lakini hata chembe ya kurudia ardhi yao haionekani basi kaamua tu kuunga mkono juhudi za kusimamisha mapigano maana hata kama angekataa huku Majeshi ya Israel yalikuwa yanasonga mbele kuelekea mji mkuu Cairo Anwar Sadat aliamuakuachana na vita na kuanza kutafuta suluhu ya kusimamisha mapigano baadaye waliweka mkataba wa Amani na Israel
Rais Anwar Sadat alionekana kama Msaliti na aliweza kuuliwa na waislamu wenye siasa kali mwaka 1981Lakini atakumbukwa sana hasa kwa juhudi zake za kutafuta Amani hasa alipoona Juhudi za Vita hazileti matunda kaamua kufanya njia Mmbadala ya Amani
What did Israel get out of the Yom Kippur War?

Pamoja na kupata mafanikio kwa kuyarudisha nyuma majeshi ya Misri na Syria yaliyokuwa yameingia katika eneo lao la ulinzi, Israel haikufanya vizuri katika vita hivi kwa kuwa ilikuwa vigumu kukabili viwanja viwili vya mapigano vyenye askari wengi kuliko vyao
Askari wapelelezi hawakufanya kazi yao vizuri ilionekana kama walikua wame-yadharau majeshi ya Misri kulikuwa na ishara za wazi kuonyesha kuwa Misri itawashambulia lakini hawakutilia maanani.

Askari wa Israel wale wa akiba hawakuitwa kwa wakati maana walianza kukusanywa tarehe 8-10-1973 hivyo wangeitwa mapema huenda Historia ingesoma vingine.

The war also served as a salutary lesson to the Arab nations that surrounded Israel in that initial victories had to be built on. The failure of the Egyptian and Syrian forces to defeat Israel pushed Sadat towards adopting a diplomatic approach. It also encouraged some Palestinians to more

extreme actions. On the diplomatic front, the Camp David talks took place while the actions of the PLO became more violent.
Why didn't the Arab nations build on their initial successes?

Clearly, the use of intelligence massively benefited the Israelis. However, as in 1948, the Arab nations did not fight as one unit. Their command structure was not unified and each fighting unit (in the Sinai and the Golan Heights) acted as individual units. With up to nine different nationalities involved on the Arab side, mere co-ordination would have been extremely difficult.

Secondly, the Israelis had to work to one simple equation: if they lost, the state of Israel would cease to exist. Therefore, for Israel it was a fight to the finish literally "death or glory". If the various Arab nations lost, they could survive for another day.
Mwandishi ni mchambuzi huru wa siasa za mashariki ya kati.

Ana uzoefu mkubwa katika medani ya sayansi ya siasa ya kimataifa. Nawashukuru wataalamu wengine na waandishi ambao tayari waliwahi andika juu ya habari hizi.

Bill HENRY EST
E-mail Henryest600@icloud.com
( nicheki upate nakala yote)
Nawashukuru wataalamu wote wa kufikiri jf intelligence ; Humble, yeriko, bold,na wote.

——-..........................————
Kitabu hard copy kitatoka soon, chenye operation zote. Maana nilichoachia hapa ni asilimia arobaini tuu. Nashukuru kwa wote mlionitumia email na kuniomba nitoe Hard copy haraka.japo sasa soft copy ndio ipo.
 
Israel si lolote si chochote bila ya marekani kuwadhamini silaha na pesa na ndio maana kabla ya kupewa hako ka-ardhi na hao wazungu huko nyuma walikuwa wanapigwa tu mwanzo mwisho.

Mfano huko poland 1943 wayahudi waliunda jeshi kuzuia mauaji ya wayahudi wenzao ila zaidi ya wayahudi 75 elfu walichinjwa au kupotezwa ama kutekwa.

Hapo usisahau huko uhispania kwenye first crusade na huko ufaransa kwenye second second crusade walichinjwa kama kuku

Yaani kwa ufupi hakuna vita waliowahi shinda kwenye open play ila baada ya kuwekwa hapo na wazungu ndio wanawapa kiburi ila leo mmarekani akiachana na Israel asubuhi tu wanatandikwa ila nashangaa Kuna watu mnadai wanashinda kisa wana Mungu as if kabla ya kupewa hicho kiardhi kwa mabavu hawakuwa na Mungu wao!!

Tuache propaganda kiufupi bila marekani hakuna Israel that's all i can say
2 Kings 6:22,23 na 2Timothy 2:23-25 hapa tunapata kujua habri za wema.
Hakika mungu ni mwema. Watapigana lakini hawatashinda

aisee kweli,vita ni ya Mungu,haijalishi adui yako ana nguvu,kias gani,ukimtegemea Mungu utashinda....
 
Israel si lolote si chochote bila ya marekani kuwadhamini silaha na pesa na ndio maana kabla ya kupewa hako ka-ardhi na hao wazungu huko nyuma walikuwa wanapigwa tu mwanzo mwisho.

Mfano huko poland 1943 wayahudi waliunda jeshi kuzuia mauaji ya wayahudi wenzao ila zaidi ya wayahudi 75 elfu walichinjwa au kupotezwa ama kutekwa.

Hapo usisahau huko uhispania kwenye first crusade na huko ufaransa kwenye second second crusade walichinjwa kama kuku

Yaani kwa ufupi hakuna vita waliowahi shinda kwenye open play ila baada ya kuwekwa hapo na wazungu ndio wanawapa kiburi ila leo mmarekani akiachana na Israel asubuhi tu wanatandikwa ila nashangaa Kuna watu mnadai wanashinda kisa wana Mungu as if kabla ya kupewa hicho kiardhi kwa mabavu hawakuwa na Mungu wao!!

Tuache propaganda kiufupi bila marekani hakuna Israel that's all i can say
Mkuu sidhani kama umesoma thread yote.
.
Israel haijawahi kupigwa vita yoyote, haijawahi kuuliwa watu wake kwa kiasi kikubwa kuliko maadui zake watakavyokufa toka mwaka 1948 hadi leo.
.
Kuhusu mmarekani bila yeye hakuna Israel hapo unajidanganya yeye kama yeye hata leo hii anaouwezo wa kuwapiga waarabu wotee, kwa uwezo gani walionao?

Kwanza kabisa irael anajua amezungukwa na mataifa ya namna gani, anajua wanania gani dhidi yake, wanatamani apatwe na nini n.k.

Hivyo Israel kajipanga sana kijeshi kuliko mataifa ya kiarabu na hata yasiyo ya kiarabu yanayohasimiana nae.
.
Israel ni nuclear power country brother akiwemo Russia, US n.k muarabu analijua hili hawezi thubutu cheza na Israel zaidi ya kutaka tu "Negotiations".
.
Mataifa ya kikristo ndio yenye nguvu kubwa kuliko ya kiarabu achilia mbali mataifa ambayo yamejipambanua serikari zake hazina dini. Ila Germany, France, Denmark, Us, Brazil, Italy na mengineyo mengiiiii yako side ya israel hata Russia mwenyewe sema kwanini vita ikitokea baina ya waarabu na Israel atakuwa upande wa waarabu wakati wao ni taifa lenye idadi kubwa ya wakristo? Kwa sababu za kibiashara ili nao angalau wawe taifa lenye uchumi mkubwa zaidi duniani waepuke " Sanctions " za US.
.
Hitimisho
Tukirejea maandiko matakatifu ya Bible 2Kings 6:22,23 tunapata kujua wema wa mungu ubaya haulipwi kwa ubaya bali wema unalipwa kwa ubaya.
Elisha alikuwa mtu wa maono aliyemtonya mfalme wa israel juu ya mipango ya kutaka kuuangamiza ufalme wao hivyo kila anapopanga mikakati mfalme wa Syria Elisha alikuwa akipata maono, wakipanga kuwavamia Haifa wanakuta wamekwishaondoka Elisha alikuja kupata maono ya wanajeshi wa Syria waliopanga kumteka elisha lakini wao ndio waliotekwa badala ya kumteka Elisha na mfalme wa Israel kuamuru wauwawe lakink Elisha alishauri waachiwe wakasimlie matendo makuu waliyotendewa.
Brother hakuna taifa lenye historia kubwa ya kijeshi kama israel
 
aisee kweli,vita ni ya Mungu,haijalishi adui yako ana nguvu,kias gani,ukimtegemea Mungu utashinda....


Ikiwa huku ndiko kumtegemea Mungu, ?? Inabidi Bashite aombe radhi :p:p:p:p:p

Welcome to Tel Aviv, the gayest city on earth - The Boston Globe


1542520121234.png



Tel Aviv trumps New York to be named world's best gay city | Daily ...

Daily Mail

Tel Aviv trumps New York to be named world's best gay city | Daily Mail Online
https://www.dailymail.co.uk/news/ar...umps-New-York-named-worlds-best-gay-city.html
 
Mkuu sidhani kama umesoma thread yote.
.
Israel haijawahi kupigwa vita yoyote, haijawahi kuuliwa watu wake kwa kiasi kikubwa kuliko maadui zake watakavyokufa toka mwaka 1948 hadi leo.
.
Kuhusu mmarekani bila yeye hakuna Israel hapo unajidanganya yeye kama yeye hata leo hii anaouwezo wa kuwapiga waarabu wotee, kwa uwezo gani walionao?

Kwanza kabisa irael anajua amezungukwa na mataifa ya namna gani, anajua wanania gani dhidi yake, wanatamani apatwe na nini n.k.

Hivyo Israel kajipanga sana kijeshi kuliko mataifa ya kiarabu na hata yasiyo ya kiarabu yanayohasimiana nae.
.
Israel ni nuclear power country brother akiwemo Russia, US n.k muarabu analijua hili hawezi thubutu cheza na Israel zaidi ya kutaka tu "Negotiations".
.
Mataifa ya kikristo ndio yenye nguvu kubwa kuliko ya kiarabu achilia mbali mataifa ambayo yamejipambanua serikari zake hazina dini. Ila Germany, France, Denmark, Us, Brazil, Italy na mengineyo mengiiiii yako side ya israel hata Russia mwenyewe sema kwanini vita ikitokea baina ya waarabu na Israel atakuwa upande wa waarabu wakati wao ni taifa lenye idadi kubwa ya wakristo? Kwa sababu za kibiashara ili nao angalau wawe taifa lenye uchumi mkubwa zaidi duniani waepuke " Sanctions " za US.
.
Hitimisho
Tukirejea maandiko matakatifu ya Bible 2Kings 6:22,23 tunapata kujua wema wa mungu ubaya haulipwi kwa ubaya bali wema unalipwa kwa ubaya.
Elisha alikuwa mtu wa maono aliyemtonya mfalme wa israel juu ya mipango ya kutaka kuuangamiza ufalme wao hivyo kila anapopanga mikakati mfalme wa Syria Elisha alikuwa akipata maono, wakipanga kuwavamia Haifa wanakuta wamekwishaondoka Elisha alikuja kupata maono ya wanajeshi wa Syria waliopanga kumteka elisha lakini wao ndio waliotekwa badala ya kumteka Elisha na mfalme wa Israel kuamuru wauwawe lakink Elisha alishauri waachiwe wakasimlie matendo makuu waliyotendewa.
Brother hakuna taifa lenye historia kubwa ya kijeshi kama israel


Ni kweli , kwa hali hii




WORLD'S TOP GAY CITIES

The most popular destinations for gay travellers, as voted for by readers of GayCities.com, are:

1. Tel Aviv - 43 per cent

2. New York - 14 per cent

3. Toronto - 7 per cent

4. Sao Paolo - 6 per cent

5 London - 5 per cent

6 Madrid - 5 per cent

7. New Orleans - 4 per cent

8. Mexico City - 4 per cent
 
Ni kweli , kwa hali hii




WORLD'S TOP GAY CITIES

The most popular destinations for gay travellers, as voted for by readers of GayCities.com, are:

1. Tel Aviv - 43 per cent

2. New York - 14 per cent

3. Toronto - 7 per cent

4. Sao Paolo - 6 per cent

5 London - 5 per cent

6 Madrid - 5 per cent

7. New Orleans - 4 per cent

8. Mexico City - 4 per cent

Aibu tupu walahi
Ni mambo ya kishirikina walahi
Piga chini milele yote walahi
 
Ni kweli , kwa hali hii




WORLD'S TOP GAY CITIES

The most popular destinations for gay travellers, as voted for by readers of GayCities.com, are:

1. Tel Aviv - 43 per cent

2. New York - 14 per cent

3. Toronto - 7 per cent

4. Sao Paolo - 6 per cent

5 London - 5 per cent

6 Madrid - 5 per cent

7. New Orleans - 4 per cent

8. Mexico City - 4 per cent
Ungehariri basi kaka😂😂😂😂 "The most popular destinations for gay travellers" Ungetoa hii inaondoa maana ya ulichotaka kukikusudia ngoja.
.
Kumbe hiyo miji haina mashoga ila mashoga husafiri kwenda huko!!! 😱
 
Back
Top Bottom