Iringa - Matukio na Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015 kama yanavyotujia

kama msigwa kashindwa tutakuwa na bunge la ajabu sana magufuli atafanya kazi mbaya kuliko anaemwachia coz ni vilaza vinajazana ndiooooooooooo
 
mpaka sasa nimeshachanganywa, tusaidie kutupa taarifa inayoeleweka mkuu hali ya mbunge wangu Msigwa ikoje?
Msigwa AMESHINDA na mpaka sasa tuna madiwani zaidi ya 10 kati ya Madiwani 18, kwa maana nyingine hii Halmashauri itaongozwa na CHADEMA!!
 
Msigwa AMESHINDA na mpaka sasa tuna madiwani zaidi ya 10 kati ya Madiwani 18, kwa maana nyingine hii Halmashauri itaongozwa na CHADEMA!!

hii habari itakuwa nzuri sana kwangu, vinginevyo ningewachukia sana watu wa iringa mjini, hivi unawezaje kumpiga chini mbunge kama msigwa? Unakuwa unataka aina gani ya mbunge?
 
Mkuu tuvumiliane tu watanzania wameamua

Mimi hakuna shida mradi nina uwezo wangu wa kifikra wa kutafuta pesa naona serikali hainisaidii kwa chochote sema wivu unanishika tu nikiangalia nchi za wenzetu zinavyopiga hatua sisi tunabaki nyuma. Ila kwa swala la individuals kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe
 
Mimi hakuna shida mradi nina uwezo wangu wa kifikra wa kutafuta pesa naona serikali hainisaidii kwa chochote sema wivu unanishika tu nikiangalia nchi za wenzetu zinavyopiga hatua sisi tunabaki nyuma. Ila kwa swala la individuals kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe

Ndo unajua leo kama serikali haisaidii lolote bila kupiga kazi teh teh teh
 
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu utangazaji wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu kwa vyombo vya utangazaji kwa mujibu wa Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015. Kanuni hizi zipo kwa mujibu wa Sheria kama ilivyotolewa na Gazeti la Serikali la Tarehe 26 Juni, 2015. Kanuni hizi zinalenga kuweka utaratibu mzuri wa kutangaza shughuli za kampeni na uchaguzi mkuu kuwa wa amani na utulivu.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapenda kuwakumbusha kuwa ni marufuku kwa vituo vyote vya utangazaji kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu bila kupata taarifa sahihi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa utaratibu waliojiwekea.

Vilevile, vituo vyote vya utangazaji vinapaswa kuzigatia Sheria na Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015.

Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015, Na. 16 (1) na 16(2) inaelekeza kama ifuatavyo:-

16(1) kwamba kila mtoa huduma za maudhui atakuwa na wajibu wa kuuarifu umma juu ya matokeo ya uchaguzi, kadiri yanavyopatikana. uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha usahihi wa matokeo yote yanayotangazwa.

16(2) Mtoa huduma za maudhui hatatangaza maoni ambayo yanaweza kuchochea vurugu au kuhamasisha chuki kwa misingi ya mbari, kabila, jinsia, dini au Imani za kisiasa na ambayo yanajenga uchochezi wa kusababisha madhara.

Hivyo basi, vituo vya utangazaji vinatakiwa kufuata kikamilifu Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015 na kwamba vituo vya utangazaji vitawajibika na matokeo ya maudhui ya matangazo ambayo hayatozingatia Kanuni.

Mamlaka inatoa wito kwa vituo vya utangazaji kutumia weledi katika maamuzi ya kihariri kuchanganua kipi kinafaa kutangazwa na uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha kuna usahihi katika kutangaza matokeo yote yatakayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAREHE 25/10/2015

Kwa mtaji huu watakamatwa weengi itabidi bajet ya mahakama na magereze iongezeke kushughulikia wakosaji....

Matokeo hubandikwa vituoni...pana shida gani?! Nafikiri shida itakuja uthibitisho wa NEC ukiwa tofauti na mbao za kwenye vituo.
 
Back
Top Bottom