Mangungo II
JF-Expert Member
- Jul 6, 2012
- 18,022
- 26,351
Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Irene Uwoya leo kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa INSTAGRAM ameabandika picha akiwa anakula- MAKANDE na kuandika kuwa hicho ndio chakula anachokipenda kuliko vyote, kitu ambacho baadhi ya watu walipinga na kusema mrembo huyo ameFEKI kusema hivyo.
"Namshukuru MUNGU kwakunipa BIBI anae nipendaaa asante sanaaa bib yangu kipenz kwa chakula kitamu nachokipenda kuliko vyote"-Uwoya aliandika mara baada ya kuweka picha hiyo hapo juu.
Mvutano kati ya wale amabo wanaona kaongea kiukweli na wale ambao wanaona anaigiza tu , ulipelekea posti kumiminiwa komenti kibao.
"We muongo sikwel eti unakipenda hicho chakula kulko vyote coz chakula chenyewe umekikuta kwa bibi yako inaonesha kwako huwa hukipiki"mmoja aliandika.
Lakini wengi wameonyesha-kukumbuka mbalii na kuelezea utamu wa makande. Mimi pia nayapenda wewe je?
Mzee wa Ubuyu
31.03.2015----Tags:- UWOYA-