Iran yataka Umoja wa mataifa (UN) kulaani shambulizi la Israel nchini Syria

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
7,418
9,599
Iran kupitia balozi wake wa Umoja wa mataifa umeitaka UN kulaani shambulizi lililofanywa na Israel kwa kushambulia ubalozi wake uliopo Syria.

Iran imesema Israel ni tishio kubwa mashariki ya kati huku ikiapa kulipa kisasi.

Hapo Jana waziri wa ulinzi wa Israel alisema Taifa hilo lipo tayari kwa jibu lolote litakalotoka kwa adui yake yoyote na kwamba hawatasita kumshughulikia popote pale alipoalipo, huku akionya kuongezeka kwa mashambulizi zaidi.
 
Baada ya lile Shambulio nilitarajia Israel ndiye angekuja kutafuta huruma kwa kichapo kutoka Iran.

Kwa haya yanayoendelea, tutarajie Iran kufutwa kwenye Ramani na Israel badala ya yeye kuifuta Israel?
 
Mayahudi siku zote yanapewa kiburi na kaka yao Marekani. Bila ya Marekani, hao Mayahudi si lolote! Si chochote.
 
Iran kagoma kunasa, kha! Tumemsaka sana huyu, yaani kashikwa kidevu, kapapaswa na kupigwa vibao ila wapi amegoma kufanya kweli ili tumtandike.....
 
Haya mambo kila siku Iran anajiapiza kuifuta Israel lakini UN huwa hawasemi lolote kuhusu tishio hilo, wamekaa kimya, hata kuwaita ili wawasuluhishe hakuna. Israel amejibu kutokana na vitisho vya Iran kuwa inajiandaa kumshambulia na kuisukumiza Tel Aviv bahari ya Mediterranean, maneno hayo yametajwa na viongozi wa ngazi za juu za Iran, kwa mazingira hayo Israel lazima ajihami na uchokozi wowote wa Iran.
 
Walaani.....watoe laana........bwana katibu mkuu wa UN apande juu ya meza amwage lazi hapo atakua ameshalaani
 
Iran kagoma kunasa, kha! Tumemsaka sana huyu, yaani kashikwa kidevu, kapapaswa na kupigwa vibao ila wapi amegoma kufanya kweli ili tumtandike.....
Weee mbona unashabikia mambo ya vita!!!! Acha upumbavu, fikiria watu wangapi wanakufa kwa vita, acha ujinga, unakaa mitandaoni kuandika upumbavu.
 
Back
Top Bottom