Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,573
- 19,456
Kitu cha ajabu, irani wanatoa elimu nzuri sana; hasa ile ya kati. Sasa vijana wa kiirani wakishakamilika katika elimu ya kati wanakwenda kuchukua elimu ya juu marekani na kubaki huko wakisaidia kukuza teknolojia ya marekani. Tunao wairani kadhaa kazini kwetu, na kweli jamaa wanajua sana basic science. Iwapo Irani ingewavutia raia wake wote walioko Marekani, Kanada, UK, Australia na sehemu nyingine za ulaya ya magharibi, na kuwapa mazingira mazuri ya kufanyia kazi, ingekuwa ni nchi tishiso sana. Lakini jamaa hawataki kurudi kwao kwa sababu wanadai hawataruhusiwa mambo mengi sana mabayo wameyazowea marekani hata kama wakipewa mshahara wa namna gani, kwa mfano, hawataweza kukata kinywaji baada ya kazi na mambo menineyo ya kiwestern.