Ipo siku shetani atavidai vitu vyake kwako, we jifanye mjanja tu!

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!

Shetani anavyo vitu vyake na kwa bahati mbaya sana kuna wanadamu wameamua kuvitumia na hawataki kuviachia.

Furaha ya shetani ni kuona mwanadamu anakufa akiwa ameshikilia vitu vyake,Atahakikisha kitu chake unakitunza na kuking'ang'ania kwa gharama yeyote hadi unaingia kaburini.

1. Kama unaendelea kugida pombe kwa mbwembwe zote huku ukiziita majina mbalimbali ya kukupendeza elewa kwamba hiyo ni Mali ya Shetani na unaendelea kumtunzia mali yake hadi unaingia kaburini.

2. Kama bado unaendeleza zinaa/Uasherati/Ufuska/Uzinzi tambua kabisa ya kwamba hizo ni mali za shetani na endelea kumtunzia na ipo siku atakudai.

3. Kama bado unaendeleza kuiba,kutapeli na kulaghai wewe endelea kumtunzia shetani mali yake na ipo siku atakudai.

4. Kama bado unaendelea kutembea na shemeji yako kwa kificho ukidhani kuna mtu unamkomoa tambua ya kwamba hiyo ni mali ya shetani na muda si mrefu atahitaji mali zake.

5. Kama bado unaendelea kufira/kufirwa ukidhani huonekani we tambua ya kwamba hiyo ni mali ya shetani unaimiliki na ipo siku ataidai mali yake.

6. Kama bado unaendelea kutumia ushirikina kwenye biashara yako ukidhani huonekani,elewa ya kwamba hiyo ni mali ya shetani amekupatia na ipo siku atakudai.

7. Endeleza sana fitina hapo kwenye biashara na kazini kwako ukidhani hiyo ni mali yako,hiyo mali niya shetani na muda si mrefu ataidai.

8. Endelea sana kutembea na Mke/Mume wa mtu ukidhani kuna mtu unamkomoa kumbe unamiliki mali za shetani.

Je, unamiliki nini cha Shetani?

USIKAE NA MALI ZA SHETANI MRUDISHIE ILI ASIJE KUZIDAI.

ONYO :

Nyie mnaojifanyaga hamuamini Uwepo wa Mungu piteni kama mnaaga maiti msije nisababishia Ban.
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!.

Shetani anavyovitu vyake na kwa bahati mbaya sana kuna wanadamu wameamua kuvitumia na hawataki kuviachia.

Furaha ya shetani ni kuona mwanadamu anakufa akiwa ameshikilia vitu vyake,Atahakikisha kitu chake unakitunza na kuking'ang'ania kwa gharama yeyote hadi unaingia kaburini.

1.Kama unaendelea kugida Pombe kwa mbwembwe zote huku ukiziita majina mbalimbali ya kukupendeza elewa kwamba hiyo ni Mali ya Shetani na unaendelea kumtunzia mali yake hadi unaingia kaburini.

2.Kama bado unaendeleza Zinaa/Uasherati/Ufuska/Uzinzi tambua kabisa ya kwamba hizo ni mali za shetani na endelea kumtunzia na ipo siku atakudai.

3.Kama bado unaendeleza kuiba,kutapeli na kulaghai wewe endelea kumtunzia shetani mali yake na ipo siku atakudai.

4.Kama bado unaendelea kutembea na shemeji yako kwa kificho ukidhani kuna mtu unamkomoa tambua ya kwamba hiyo ni mali ya shetani na muda si mrefu atahitaji mali zake.

5.Kama bado unaendelea kufira/kufirwa ukidhani huonekani we tambua ya kwamba hiyo ni mali ya shetani unaimiliki na ipo siku ataidai mali yake.

6.Kama bado unaendelea kutumia ushirikina kwenye biashara yako ukidhani huonekani,elewa ya kwamba hiyo ni mali ya shetani amekupatia na ipo siku atakudai.

7.Endeleza sana fitina hapo kwenye biashara na kazini kwako ukidhani hiyo ni mali yako,hiyo mali niya shetani na muda si mrefu ataidai.

8.Endelea sana kutembea na Mke/Mume wa mtu ukidhani kuna mtu unamkomoa kumbe unamiliki mali za shetani.

Je,Unamiliki nini cha Shetani?

USIKAE NA MALI ZA SHETANI MRUDISHIE ILI ASIJE KUZIDAI.

ONYO :

Nyie mnaojifanyaga hamuamini Uwepo wa Mungu piteni kama mnaaga maiti msije nisababishia Ban.
kweli mtupu
 
Achana na pombe mkuu,mengine yote upo sawa,wewe kama Imani yako inaona ni haramu shauri yako. Acha Sisi tunywe kwa raha zetu.

Maandiko yana ilani nyingi juu ya kunywa kileo (mambo ya walawi 10:9; hesabu6:3; kumbukumbu la torati 29:6; waamuzi 13:4,7,14; samueli wa kwanza 1:15; methali 20:1; 31:4,6; isaya 5:11;22; 24:9; 28:7; 29:9; 56:12; mika 2:11; luka 1:15). Maandiko hayakatazi mkristo kunywa pombe, divai wala kinywaji chochote chenye kileo ndani. Maana maandiko mengine huzungumzia kileo kwa kuhalalisha matumizi yake. Mhubiri 9:7 inaamuru, “ kunywa kileo na moyo mkunjufu.” Zaburi 104:14-15 inaeleza Mungu hutoa divai “ inayofurahisha mioyo ya wanadamu.” Amosi 9:14 inazungumzia juu ya kunywa divai kutoka kwa shamba lako kama alama ya baraka za Mungu. Isaya 55;11 inapongeza “ naam, njoo ununue divai na maziwa…”
 
Ahsante mkuu kwa kuihalalisha pombe kwa usomaji wako!.

SOMA HAPA 👇

1 WAKORINTHO 6 : 9 - 10

"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."

*ZINGATIA - Neno " Wala walevi" limerudiwa mara mbili,siyo kwa bahati mbaya!

UTAAMUA WEWE
 
Ahsante mkuu kwa kuihalalisha pombe kwa usomaji wako!.

SOMA HAPA

1 WAKORINTHO 6 : 9 - 10

"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."

*ZINGATIA - Neno " Wala walevi" limerudiwa mara mbili,siyo kwa bahati mbaya!

UTAAMUA WEWE
Hao ni walevi,,,waliosemwa kila jambo linakiasi chako hata upendo uliopindukia ni Dhambi pia
 
Mkuu Swali halijibiwi Kwa Swali. Labda kama ni siasa.
Kwa kuacha kuvifanya mkuu!
Na kumkabidhi Mungu maisha yako, lugha nyepesi Kwa kumtegemea Mungu...
Mfano ;ulikuwa unategemea uganga,unaancha unaanza kumtegemea Mungu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom