Ipi sahihi; kufanya kazi kwa bidii au kufanya kazi kwa welevu?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,456
40,446
Wengi wanashauri, ili ufanikiwe lazima ufanye kazi kwa bidii; lakini miaka nenda rudi, kuna wasukuma mikokoteni wanafanya kazi kwa bidii, waponda kokoto wanafanya kazi kwa bidii, mkulima analima kwa bidii, mchoma mahindi anahoma kwa bidii, muuza nyanya anafanya kwa bidii n.k lakini maisha yao yako vile vile.

Sasa, hii kufanya kazi kwa bidii inamaanisha nini? Kwa nini tusiseme kufanya kazi kwa werevu?​
 
Bidii ni juhudi, werevu ni akili (takriban sawa na weledi).

Hizi sifa mbili ni tangamani, zinategemeana.

Mtu anaweza kuwa na bidìi, lakini asiye na werevu. Vilevile anaweza kuwa mwerevu lakini bidii kiduchu.

Watu wengi werevu ama weledi wanafeli kimaisha kwa sababu wanadhani werevu wao utawafanyia wanachotaka.

Fikiria werevu na bidii ya mtu anayetengeneza aplikesheni inayomwezesha mtumiaji wa umeme kuingiza luku moja kwa moja pale anaponunua kwa simu yake, bila kupitia mzunguko wa kujaza zile tarakimu 20!!!
 
Fikiria mmama anaponda kokoto mpaka ajaze tipa, alafu anaambulia elfu 30
Aangalie improvement ya kazi yake aelekeze wapi ili uzalishaji uongezeke, Labda hiyo elfu 30 awekeze kwenye nyundo kubwa ili kuongeza speed ya uzalishaji, hizi McDonald tunazokula sasa hivi walianza kama wachoma chips tuu wa mtaani lakini baada ya miaka mingi ya improvement sasa ni mabilionea, naamini Kila kitu kina room ya kufanya improvement na kuongeza thamani, ndio unahitaji hard work na akili na kuachana na visingizio vya kutofanya kazi
 
Ni sawa na mchimbaji mdogo wa madini, anapoteza nguvu na muda kuchimba sehemu ambapo hakuna madini
 
Nishawahi shudia Jamaa amejaliwa bahati,Hana bidii Wala Welevu. Yeye yaan akichekecha kidogo tu mambo bie anatumia pesa inaisha👐
 
Back
Top Bottom