iPhone is disabled, connect to iTunes

zubery360

Senior Member
Apr 11, 2014
157
61
Wapendwa wanaJF, Nina tatizo kwa simu yangu. Simu yangu ni iPhone 5 nyeupe ambayo nimekuwa nikiitumia kwa muda wa mwaka mmoja sasa, lakini hivi juzi imejiblock na kuandika iPhone is disabled halafu chini ya hayo maneno imeandika connect to iTunes. Ukislide inaniletea sehemu ya Emergence call. Sasa nimejaribu kudownload iTunes kwa PC ili nii-connect lakini kila nikifanya hivyo inanipeleka kudownload item. Ikianza kudownload inachukua takriban masaa matatu ili imalize, lakini kabla ya kufika huko simu yangu inajiwasha na kurudi palepalee, yaani ile icon ya iTunes inatoweka na kuwaka upya . Sasa sijui niifanyeje maana mpaka sasa nimeiweka kama pambo ndani. Nisaidieni tafadhali ili niweze kuirudisha kwenye matumizi.

NATANGULIZA SHUKRANI
 
Back
Top Bottom