ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
[h=1]IPHONE 6 PLUS NA KASHFA YA BENTGATE[/h]
Kabla ya kuichambua kashfa hii kwanza tulinganishe wembamba wa iPhone 6 Plus na simu zinazofanana au kukaribiana na kwa ukubwa na simu hii. Samsung Galaxy note 4 ambayo ina skioo chenye ukubwa wa inchi 5.7 ni pana kuliko iPhone 6 Plus kwa 1.3 mm nzima ikiwa na upana wa inchi 8.4mm, nayo Samsung Galaxy Note 4 Edge nayo ina upana sawa na Galaxy Note 4. Nokia Lumia 1520 yenye skrini yenye ukubwa wa inchi 6 ni pana zaidi ya iPhone 6 kwa 1.6 mm ikiwa na upana wa 8.7mm. Nayo LG G Flex yenye kioo chenye ukubwa wa inchi sita nayo ina upana sawa na Nokia Lumia 1520. Ukitaka kutambua jinsi simu hii ilivyo nyembamba hata Samsung Galaxy S5 ambayo ni ndogo kuliko iPhone 6 Plus inaizidi iPhone hii upana kwa 1 mm nzima.
Sababu ya uchambuzi huu wa mlinganyo wa wembamba ni kuwa tunaamini kuwa wembamba wa iPhone 6 Plus ukilinganisha na ukubwa basi unachangia kuwepo kwa udhaifu hii kwenye simu hii ukizingatia ukubwa wake. iPhone 6 ambayo ina kioo chenye ukubwa wa inchi 4.7 haikuripotiwa kuwa na tatizo hili.
Kupinda kwa iPhone 6 Plus ambako kumepewa hashtag ya bentgate (#bentgate) kunatokea unapoikalia simu yako ukiiweka mfuko wa nyuma wa suruali, pia wako wanaodai kuwa simu zao zimepinda zikiwa mfuko wa mbele bila ya hata kuikali. Simu hii imetengenezwa ikiwa na gamba la madini ya aluminium.
Wakati habari za kupinda kwa simu hii zinasambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, blogu za teknolojia na hata mashirika rasmi ya habari kama vile BBC, Apple bado hawakutoa kauli yoyote rasmi kutokana na tatizo hili.
Wadau wa mtandao wa Unbox Therapy walijaribu kuipinda simu hii kwa makusudi wamepatwa na ยmsibaย kwani baada ya kutaka kuinyosha wanadai iPhone 6 Plus ilivunjika kioo na pia kukatika fremu kwa upande wa kushoto chini ya vifungo vya kuzidisha na kupunguza sauti. Hata hivyo wadau hao walijaribu kupinda Galaxy Note 3 ambayo ilipinda kwa kiasi kidogo sana ukilinganisha na iPhone 6 Plus, hata hivyo Samsung hii imetengenezwa ikiwa na gamba la plastiki. Ni vigumu kuthibitisha nguvu walizotumia kuipinda iPhone 6 Plus ukilinganisha na Samsung Galaxy Note 3, hata hivyo mdau huyo wa Ungox Therapy Norm Uhl alidai kutumia nguvu zaidi katika jaribio lake la kuipinda Samsung Galaxy Note 3, hata video inaonyesha akiwa katika hali hiyo. Ikiwa Norm Uhl ni mkweli angalau sasa tunajua kwamba simu za plastiki nazo zina faida yake.
Chanzo:gajetek habari
Amini usiamini Apple bila ya kukusudia wametoa simu inayopinda! Simu hiyo pamoja na ndogo yake yaani iPhone 6 tayari inarajiwa kuongoza kwa mauzo baada ya kuuza simu milioni 10 kwa muda wa wikiendi moja tu, Watumiaji wa Phone 6 Plus wamekuwa wakililalamikia jambo hili kwenye mitandao ya kijamii. iPhone 6 Plus ambayo ina kioo chenye ukubwa wa inchi 5.5 huku ikiwa na wembamba wa 7.1 mm ni moja kati fableti (simu kubwa) nyembamba mno. Kabla ya kuichambua kashfa hii kwanza tulinganishe wembamba wa iPhone 6 Plus na simu zinazofanana au kukaribiana na kwa ukubwa na simu hii. Samsung Galaxy note 4 ambayo ina skioo chenye ukubwa wa inchi 5.7 ni pana kuliko iPhone 6 Plus kwa 1.3 mm nzima ikiwa na upana wa inchi 8.4mm, nayo Samsung Galaxy Note 4 Edge nayo ina upana sawa na Galaxy Note 4. Nokia Lumia 1520 yenye skrini yenye ukubwa wa inchi 6 ni pana zaidi ya iPhone 6 kwa 1.6 mm ikiwa na upana wa 8.7mm. Nayo LG G Flex yenye kioo chenye ukubwa wa inchi sita nayo ina upana sawa na Nokia Lumia 1520. Ukitaka kutambua jinsi simu hii ilivyo nyembamba hata Samsung Galaxy S5 ambayo ni ndogo kuliko iPhone 6 Plus inaizidi iPhone hii upana kwa 1 mm nzima.