Interview kufanyika online utumishi hiki ni kiini macho kingine kwa watoto wa wakulima

Sektretarieti ya ajira na utumishi wa umma, leo wametangaza kuanza mchakato wa kufanya usahili kwa njia ya mtandao (online interview) hiki ni kipigo kingine kwa watoto wa wakulima wasiokuwa na mjomba, shangazi, au baba wa kuwashika mkono..
Nilichojifunza watanzania wengi ni wapingaji wa kila kitu hata kama hawajui wanapinga nini. Kati ya jambo zuri ambalo secretariate wamelifanya ni hili la kugawanya interview sehemu mbalimbali za nchi.

Yani kama wewe uko bukoba haulazimiki kuhama nyumbani na kwenda kukaa kwa mjomba ambae yupo dodoma ili uweze kuwahi interview. Yani interview unaletewa hapo nyumbani.

Unatoka shambani kulima unaenda kwenye interview asubuhi unafanya hapohapo unapata majibu unarudi nyumbani unaendelea na shambalako la mchicha. Yani buku itakupeleka kufanya interview na kukurudisha.

Mtoa mada uwe unafanya utafiti. Acha kukurupuka na kuchanganya jamii. Sanyingine mafanikio huanza kwa kuwa na +ve mindset.

Kila aliewahi kufanya interview za secretariate atakuambia. Hakunaga vimemo kule. Unatakiwa uwe na msuli wa kushindana na watanzania wengine. Ukisikia mtu Akilalamika tafitinuwezo wake utagundua kashindwa kushindana.

Kuanzia secretariate walipo anza kufanyisha interview ndipo kila mtanzania mwenye uwezo alipoweza kupaata nafasi ya kufanya kazi popote.

Hongereni sana secretariate. Nyie ni kati ya taasisi yenye uadilifu mkubwa. Hongereni sana.
 
Nieleweshe mkuu. Interview zote(apt test,written and oral)zitafanyika online??

Hivi watanzania mtaogopa teknolojia mpaka lini? Nimesikia pia watumishi wa umma wanalalamika kuwa wanatakiwa kujisajili kwa mtandao kupata services za kiutumishi .
Mimi ni mtumishi nisijisifu sana kuwa niko wizarani hapana, niko Halmashauri flani kama mhasibu, changamoto ni kuna maeneo yako KM 120 tokea HQ ya halmashauri na huko mtandano unasumbua kuliko, itambidi mtumishi asafiri aroundi 40km kufuata mtandao ili awe anajaza kazi zake kila wiki.

USHAURI WANGU
HUU MFUMO WA KUWATATHMINI WATUMISHI ON-LINE UNGEANZA KWA HATUA NA MAKUNDI FLANI YA WAFANYAKAZI, mfano Ungeanzia wizarani na Halmashauri kwa wafanyakazi wa HQ za Halmashari ndipo waushushe huko chini

Watu wa UTUMISHI walikuja wilayani kwetu wakiwa na ratiba ya siku nne, mtandao ulikuwa unabuma tena mapema asubuhi siku zote wakaondoka na kuomba wawachukue watu watatu wa idara ya utumishi wawapeleke mkoani kwa mafunzo.
 
Unaumiza unaitaji hela..
Inamaana oral,written zote online?
Sidhani kama oral itakua online, huenda wataweka maswali yao then watalimit muda wa kufanya ukishayafungua.
Mchujo utaenda hivo mpaka watakapopatika clean wa kwenda oral.

NB. Hayo ni mawazo yangu.
 
Kila mwanachuo anasimu ya kutouch , naanajua kuitumia wengi wanalaptop so kuepuka gharama ya nauli na allowance ya njiani na pia gharama ya malazi , chakula kwa siku hizo zote unatoa wapi??

Sasa wewe ndio hujielewi why post yako umeiqndika tofauti?? ungeandika hivi kuliko kwenda dodoma kupoteza muda hujui nani atapita na hali ningumu na washukuru serikali kwa uamuzi wenyw busara wawatu kutoenda huko kuendekeza umalaya. Nabadala yake watu wanasailiwa online. Iwe whtsupp au messanger au google
 
Toa ushauri wafanye nini sasa ili mridhike?
Ndugu tulizoea ajira za bila interview sasa hapa hili swala la interview linatupa shida wengine tunakwendaga dodoma kwenye interview tukiwa weupe kichwani ndiomana tukikosa ajira tunaamini tumenyimwa kumbe interview zimetupiga ndiomana Kila mabadiliko yanayokuja tunapinga tu.ila huu mfumo utapunguza gharama Kwa job seekers.
 
Huu mfumo utapunguza gharama na competition itakuwa juu hata wale waliokuwa wanaona uvivu kwenda dodoma au pengine kuhofia gharama wataweza kufanya. Kule kwenye vyombo vya usalama jkt pia imeondolewa yaani itakuwa balaa
 
Kila siku Utumishi wanaanzisha mifumo mipya ambayo ni kama haina tija. Jiulize tangu utaratibu wa watumishi kuomba uhamisho kupitia mfumo badala ya kutumia makaratasi umeanzishwa umeshawafaidisha wangapi? Jibu hakuna.
 
Lakini huu mfumo wa online utawasaidia.
 
Back
Top Bottom