Interview kufanyika online utumishi hiki ni kiini macho kingine kwa watoto wa wakulima

Ngoja tuangalie na hii itakuaje ni vizuri kukubali mabadiliko kulingana na ulimwengu unavyoenda. Inauma sana kujikuta unashindwa kwenda Dodoma na sifa pamoja na vigezo vya hiyo kazi unavyo, mimi naamini njia hii ita rahisisha sana kwa wengi wetu ambao tulikua tunashindwa kwenda Dodoma kutokana na kukosa nauli na sababu nyingine.
 
Sektretarieti ya ajira na utumishi wa umma, leo wametangaza kuanza mchakato wa kufanya usahili kwa njia ya mtandao (online interview) hiki ni kipigo kingine kwa watoto wa wakulima wasiokuwa na mjomba, shangazi, au baba wa kuwashika mkono..
Sasa hauoni kama wamerahisishiwa badala ya mtu kusafiri kutoka kwao tandahimba uko masasi au Ligangabilili mkoa mpya simiyu kwenda Dodoma kwa "indavyuu" saivi atapiga indavyuu akiwa ukouko kwao?.

Nini ghali kati ya nauli ya safari ndefu ivo na ela ya kulipia cafe kufanya indavyuu?

Mbona mna mawazo ya kimaskini hivi?

Grow up!
 
Back
Top Bottom