Inter House - Colour peeling off?

Mutensa

JF-Expert Member
Feb 20, 2009
421
90
Hello Wakubwa,

Kwa mara ya pili jengo la Inter (Interhouse) lililoko mkabala na Millennium towers, limeanza kudondosha rangi. Tulitegemea "consultants" kama hawa ndio watushauri kwa masuala yote yahusuyo ujenzi. Sasa jamani hili tunalichukuliaje, ina maana consultant wao hakuliona rangi/material zinazoendana na hali ya hewa ya hapo mahali?

Hata hivyo, jengo hili ni kivutio kikubwa sana cha macho, rekebisheni kasoro hizo jamani.

Wataalamu, hebu tushauri ili yaliyowapata interhouse yasije yakatukuta kwenye tujibanda twetu.
 
Mambo ya kudondosha rangi ni dalili mojawapo ya asbestos, ambayo ni hatari kwa afya.

Hivi bongo tunajali mambo ya asbestos? Au wengine ndiyo kwanza tunaitumia kama mapaa?
 
asante bluray.
Wahandisi wengine mko wapi?????
au mnaendelea kuparamia majukwaa ya siasa?????
 
Inawezekana jamaa (hata kama walikua na wazo sahihi la aina ya rangi), walibambikwa rangi...labda haikufikia kiwango stahiki.

Lakini mbona hawarekebishi? Au ni kitu kisichorekebishika? Just thinking loudly.
 
Back
Top Bottom