Iniesta na gaucho, Nani zaidi?

Abu Ubaidah Commando

JF-Expert Member
Sep 8, 2016
7,593
6,934
MichaelDonald660x879.jpg

260px-Ronaldinho_72.jpg
260px-Ronaldinho_72.jpg



KIUNGO MCHEZESHAJI ALIYEKAMILIKA
Andres Iniesta alianzia soka lake akiwa kwenye Academy ya La Massia inayomilikiwa na Barcelona. Uwezo wake wa kucheza kwenye nafasi tofauti, kujituma, na umuhimu kwenye mchezo, ulimfanya achukua nafasi kwenye kikosi cha kwanza akiwa na umri wa miaka 18 na alianza kucheza mechi mfululizo kwenye msimu wa mwaka 2004/05.

Akiwa kama mchezaji mchanga, Iniesta alianza kufanya mazoezi akiwa na kikosi cha kwanza na Pep Guardiola (kocha wa zamani wa Barcelona wakati akiwa bado mchezaji) alimwambia Xavi kuwa, yeye (Xavi) angemfanya Guardiola astaafu lakini Iniesta atawafanya wote wawili yaani
Xavi na Pep wastaafu.


Pep Guardiola na Andres Iniesta

Guardiola aliona mbali na hakukosea kwa kauli aliyoitoa, Iniesta hakuwa bora kwenye pasi pekee bali alikuwa mzuri kwenye ukokotaji wa mpira, alikuwa na uwezo mkubwa wa kucheza maeneo tofauti ya uwanja na alikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga mabao na kutoa pasi muhimu.

Ilikuwa chini ya Guardiola ambapo Iniesta aliuteka ulimwengu. Guardiola alimtengeneza Iniesta na kumfanya kuwa mchezaji muhimu kwa Barcelona na Hispania na kubwa alilofanya Guardiola ni kumfanya Iniesta ambaye kwa kawaida ni mtu mkimya, kuwa kiongozi kwenye timu yake.

Chini ya nahodha huyu wa zamani wa Barcelona, soka la Iniesta lilifikia kiwango cha juu kupita hata Xavi na Guardiola kama ilivyokuwa kauli ya Guardiola. Alikuwa kiungo mchezeshaji aliyekamilika na hadi sasa ameingia kwenye orodha ya wachezaji bora waliowahi kucheza Barcelona.

MFUNGAJI WA MABAO MUHIMU 
Iniesta siyo mfungaji wa mabao mengi, lakini ni mfungaji wa mabao mazuri na muhimu kwa timu yake kama Vile Zinedine Yazid Zidane. Iniesta alikuwa akifunga kwenye mechi muhimu na kubwa.



ya mabao ambayo yatakumbukwa na wengi ni bao alilowafunga Chelsea mwaka 2009 kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ulikuwa mpira wa mwisho kwenye mechi hiyo na ulikuwa mpira ambao Iniesta alifunga bao lililoivusha Barcelona hadi fainali akiwa na mshambuliaji hatari kuwahi kutokea Leonel messi.

Kwenye Kombe la Dunia 2010, Iniesta alifunga bao muhimu kwenye historia ya soka la Hispania. Huku ubao wa matokeo ukisomeka 0-0 wakati wa fainali hiyo dhidi ya Uholanzi, mpira ulimfikia Iniesta upande wa kulia wa eneo la 18, halikuwa bao kama la Zidane kwenye fainali ya mwaka 2002 wakati Real Madrid walipocheza na Bayer Leverkusen, lakini umuhimu wake ulikuwa ule ule.

Hispania waliweka historia hiyo na Iniesta alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya 2012. Aliiongoza timu yake akiwa ndani ya uwanja kwa uwezo wake na miaka minne baada ya Xavi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya 2008, Iniesta alitimiza utabiri wa Guardiola.


Vicente Del Bosque ambaye aliwahi kufanya kazi na Zidane kwenye klabu ya Real Madrid, alimtaja Iniesta kama mchezaji aliyekamilika kuliko wote aliowahi kuwaona.


Na mchezaji mwingine, Samuel Eto’o alimtaja Iniesta kama mchezaji bora duniani kwani kila awapo uwanjani huwa anatengeneza maajabu.

Hakuna ubishi kuwa Iniesta amekuwa akibadilika kwenye nafasi ya kiungo mchezeshaji bora kuendana na mchezo wa soka.

Akiwa kwenye mfumo wa Barcelona huku akicheza soka kuendana na umbo lake dogo, Iniesta alijifunza kumiliki mpira na kuuelewa mchezo kwa jinsi anavyotengeneza ‘movement’ zake, mbinu na hata maamuzi ambayo anayafanya, kitu kinachofanya soka kuonekana rahisi kwake.

Iniesta link hapa;
Andrés Iniesta - Wikipedia, the free encyclopedia
Andrés Iniesta - Wikipedia, the free encyclopedia

Kuhusu Ronaldinho link hapa;
Ronaldinho - Wikipedia, the free encyclopedia
Ronaldinho - Wikipedia, the free encyclopedia
 

Attachments

  • andres-iniesta-joven-y-guardiola.jpg
    andres-iniesta-joven-y-guardiola.jpg
    10.1 KB · Views: 123
  • Andres-Iniesta-Barcelona_2827555.jpg
    Andres-Iniesta-Barcelona_2827555.jpg
    5.8 KB · Views: 140
Ebwana ee tuacheni utani Iniesta anatisha aise, ukiweka ushabiki pembeni..kisoka Iniesta anatisha

Shikamoo Iniesta... gaucho ni level za akina jj okocha,Henry,batistuta..
alaf kuna mijitu mingine huwa inam-comparrison na Zidane, sijui huwa inaandika ikiwa imepiga wiski ama?..Zizzou na Gaucho wapi na wapi?,ni kama mbingu na Ardhi.
 
Ebwana ee tuacheni utani Iniesta anatisha aise, ukiweka ushabiki pembeni..kisoka Iniesta anatisha

Shikamoo Iniesta... gaucho ni level za akina jj okocha,Henry,batistuta..
alaf kuna mijitu mingine huwa inam-comparrison na Zidane, sijui huwa inaandika ikiwa imepiga wiski ama?..Zizzou na Gaucho wapi na wapi?,ni kama mbingu na Ardhi.
sio iniesta tu hata messi hamfikii gaucho,gaucho habari ingine,anaburudisha na kusaidia timu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom