Ingekuwa wewe...

...
Sasa kwa hao wanawake wenye vidumu ambao wengi wao sababu ya waume zao kuwa na vidumu pia, lazima heshima inapungua kwa wanandoa. Kwahiyo mume ataitwa jina kama bwege,zoba,ngumbaro, lakini hawezi save kwenye simu ni wakati wa storiz na wanawake wenzake.

...definately, hata mume hawezi save jina baya kwenye simu kumaanisha mkewe.

...imenifurahisha hiyo mw'ume kuitwa Bwege, zoba, ngumbaro kwenye storiz na wanawake wenzake...:D
 
...aaah, hiyo najua mamie. Hata mamsap akiniita 'Mbu!' najua mnhh... leo kunakuhesabu boriti wakati wa kutafuta majibu ya kina...!

nataka yale majina kwenye salooni na kitchen party ambazo 'hazijatulia', am sure baba nanihii, sio kabisa...kwani nishasikia mwiko kumremba remba mumeo huko... kuhofia kusaidiwa au kuchorwa unavosaidiwa!

All in all, mimi na kilongalonga changu, naye ana chake,...presha za nini?

Ni kweli mamsapu akikuita jina lako halisi wakati siku zote kuna manjonjo kama la'azizi na mahabuba ujue kuna jambo.

Majina mengi ya saloon ni bandia ili watu wasijue unamwongelea nani maana kuna mtu anaweza kumjua ikawa balaa hivyo ni kama kujilinda fulani kwenye maongezi na kuwaacha watu wengine solemba wasijue mwamwongelea nani.

Hivi wanaume wanasave majina ya kike kama ya kiume mfano 'Halima anasave Hamadi au Belinda anasave Benja' nk. Pia wanaume wana majina ya mafundi kibao kwenye simu zao mara fundi simu,fundi umeme,fundi bomba,fundi ujenzi,fundi seremala nk..kumbe hamna fundi hata mmoja hapo ili kama mamaa akamtindo wa kukagua simu ajue ni mafundi kumbe ndo wake wenza wa njee(vidumuz)..Hatari,siku hizi tunakimbilia simu za hao mafundi tena hata kama umeandika0save namba kama mama mzazi,itachekiwa tu..uwiiii,ha ha
 
...definately, hata mume hawezi save jina baya kwenye simu kumaanisha mkewe.

...imenifurahisha hiyo mw'ume kuitwa Bwege, zoba, ngumbaro kwenye storiz na wanawake wenzake...:D

Pia Gaidi..

Mengine siyajui Mbu..
 
Mh nimecheka kweli ngoja nione labda nami ntapata jina la kumwita wangu maana huniudhi kila mara hadi nachoka kubadili kwenye simu. Asubuhi anawezakuwa mtamu hadi basi nasave sweetie then ikifika mchana keshanibore zaidi ya mara moja natamani kusave Mbwa basi tu nashindwa! Leo I hope ntalipata la kumfit.
 
duh! yaani hapo sijui first reaction itakuwa kumchinja ama... ila the best thing is not to act immediately kwa sababu utajuta baadaye but then how do u live with that betrayal... eti lijinga liko jikoni.......hapo hata aje on his knees au head... sujui kama nitaacha kumchukia!
 
...
Hivi wanaume wanasave majina ya kike kama ya kiume mfano 'Halima anasave Hamadi au Belinda anasave Benja' nk.

...:D wanawake ndio wenye kamtindo hako...wanaume wengi hawajafikia bado ujuzi huo!

Pia wanaume wana majina ya mafundi kibao kwenye simu zao mara fundi simu,fundi umeme,fundi bomba,fundi ujenzi,fundi seremala nk..kumbe hamna fundi hata mmoja hapo ili kama mamaa akamtindo wa kukagua simu ajue ni mafundi kumbe ndo wake wenza wa njee(vidumuz)..Hatari,siku hizi tunakimbilia simu za hao mafundi tena hata kama umeandika0save namba kama mama mzazi,itachekiwa tu..uwiiii,ha ha

...:D:D:D ama kweli, duniani kuna mambo...shida yote ya nini hiyo!?
 
Shishi wanawake tumeumbwa kusahau ndugu yangu utasahau hata kabla jua halijachwa na mavituz utampa jioni ah!! Ila wewe sema kisichoeleweka utakoma. Nakumbuka kuna siku nilimwambia wangu ' jamani dia mbona unakuwa mvivu kushughulisha kichwa chako kufikiri?' duh linasemwa hadi leo eti nimemwambia hana akili sasa sijui siku akisikia namwita lijinga si atanitafuna bila chumvi!
 
sista!
Usije kujipa ugonjwa wa moyo hata siku moja.unajua kuna wakina mama wengi hata wanashindwa kuonyesha affection kwa waume zao au hata kujivunia waume zao kwa sababu kama hizi.kuna misemo tunaiskia kwenye taarabu ati "wako akiwa kwako akitoka si wako", au ati mumeo ni kama dala dala linalobeba kila aina ya abiria a kupita njia zote - we lisubiri jioni lije li park!" jamani.... Hivi kwanini lakini imefikia huko?
Majina hata mie nimesikia ati siku hizi wake wanaitwa tibaigana.. Na huyu kaenda mbali zaidi kuita " hili jinga"....hivi kuna majina gani mabaya yanayotumika kuwaita wanaume?

fataki.....
 
Majina wanayoitwa wanaume na wake zao

1. Bwege
2. Zoba
3. Usiku wa Balaa
4. Baba xxx
5. Ngumbaro
6. Jamabazi
7. Baa (waweza kuitwa jina la baa unayopendelea kunywa)
8. Jina la Nyumba ndogo (kwa mfano Tausi)
9. Cha Pombe
10. Mzee wa (sehemu unayofanyia kazi)
11. Mzee wa (gari unaloendesha) kwa mfano (Mzee wa Baloon)
12. Wa (kijiji ulichotokea) kwa mfano Wa Kimanzichana
13. Li-(Baba_Enock)
14. Wangu (kwa mfano kwenye maongezi Wangu mimi urejea nyumbani mapema)
15. e.t.c
 
Shishi wanawake tumeumbwa kusahau ndugu yangu utasahau hata kabla jua halijachwa na mavituz utampa jioni ah!! Ila wewe sema kisichoeleweka utakoma. Nakumbuka kuna siku nilimwambia wangu ' jamani dia mbona unakuwa mvivu kushughulisha kichwa chako kufikiri?' duh linasemwa hadi leo eti nimemwambia hana akili sasa sijui siku akisikia namwita lijinga si atanitafuna bila chumvi!

yaani nimecheka mpaka ofisini wananiuliza nini tena.... eti linasemwa hadi leo... umemuita mjinga.... duh!!! nao haweshi kuwaambia watoto wajinga kama mama zao!!
 
yaani nimecheka mpaka ofisini wananiuliza nini tena.... eti linasemwa hadi leo... umemuita mjinga.... duh!!! nao haweshi kuwaambia watoto wajinga kama mama zao!!

Ndo hapo sasa ndugu yangu we acha tu........

Nakwambia mie limewekwa Bank siku nkikosea tu nikawa nasemwa bali ah linafunguliwa yaani najuta kwa nini lilintoka pamoja na kuwa nilitumia kwa sauti laini we acha tu
 
Majina wanayoitwa wanaume na wake zao

1. Bwege
2. Zoba
3. Usiku wa Balaa
4. Baba xxx
5. Ngumbaro
6. Jamabazi
7. Baa (waweza kuitwa jina la baa unayopendelea kunywa)
8. Jina la Nyumba ndogo (kwa mfano Tausi)
9. Cha Pombe
10. Mzee wa (sehemu unayofanyia kazi)
11. Mzee wa (gari unaloendesha) kwa mfano (Mzee wa Baloon)
12. Wa (kijiji ulichotokea) kwa mfano Wa Kimanzichana
13. Li-(Baba_Enock)
14. Wangu (kwa mfano kwenye maongezi Wangu mimi urejea nyumbani mapema)
15. e.t.c

Akiniita mimi mbona ataona cha mtema gogo kosovo.
Hii ni dharau hawezi niita hivyo.
 
Ukitaka mwanamke muheshimiane na kupendana usimuonyeshe kwamba wewe uko weak! Ukimuonyesha upendo wa kikweli kweli..wengi wanachukulia kama ni uzaifu ndo majina ya uzoba yanaanzia hapo....

Hivi niwaulize akina dada humu: Ni vipi mwanaume anaweza kukuonyesha upendo wa kikweli kweli..bila yeye kuonekana dhaifu au kuitwa Zoba au Bushoke type????
 
Back
Top Bottom