Information kuhusu barabara ya Dar - Mtwara - umoja bridge

bwegebwege

JF-Expert Member
Jul 30, 2010
1,071
185
Habari!

Na mimi najitahidi kutangaza vivutio vya utalii Tanzania!

Jamaa yangu anataku kutembelea TZ mwezi ujao n akusafiri mikoa ya kusini hadi Mozambique. Kutokea kule (Mozambique) nadhani ataunganisha nchi nyingine bil akurudi Tanzania. Ameniomba taarifa za namna ya kusafiri kutoka Dar hadi mpaka wa Tanzania na Mozambique; angependa kujua umbali, hoteli nzuri za kufikia (Lindi, Mtwara na Kilwa) pamoja na hali ya bararbaza (kilometa ngapi na zinapitika?

Naomba wadau mnaoishi huko au mnaofahamu maeneo hayo mnipe data, either kwa kunitumia PM au reply lkwenye thread hii hhapa jamvini!

Nawasilisha
 
nyie wakereketwa mna matatizo saaaaana, kusudio lako hapa ni kutaka kutufahamisha mafanikio ya serkali yenu kwenye harakati za kuendeleza mikoa ya kusini, kwa vile hujiamini ndo maana unakuja kinyumenyume la sivyo hii mada ungeipeleka kwenye jukwaa sitahili.
 
Anaenda na usafiri binafsi au?? Kama hana usafiri ataishia Mtwara....
 
nyie wakereketwa mna matatizo saaaaana, kusudio lako hapa ni kutaka kutufahamisha mafanikio ya serkali yenu kwenye harakati za kuendeleza mikoa ya kusini, kwa vile hujiamini ndo maana unakuja kinyumenyume la sivyo hii mada ungeipeleka kwenye jukwaa sitahili.

Brother/Sister;

Kama kuna unalolifahamu wewe nisaidie, nimeomba info tu, hakuna siasa hapa!
1. Mimi ni mtanzania, siwezi kuacha kumpa mgeni maelekezo sahihi kwa kuwa eti mikoa ya kuisini imeendelezwa
2. Hiyo serikali "yenu" unayoizungumzia ni ipi? Ni hii ya wachakachuaji au ya mafisadi? Aliyekwambia mimi nina serikali ni nani?
3. Unasmea nimekuja "kinyumenyume"..kimbelembele inguwaje? Ati sijiamini? Wewe mwenye taarifa ninazoomba na kuogopa kuzitoa ndiyo hujiamini, Tanzania ni yetu, hata kama kusini kumeendelea kuliko ninakotoka mimi sasa ndiyo niache kufika? Au kama mgeni wangu ana nia ya kufika huko nisimpeleke kisa nitaonekana sijui vipi mbele za wanafiki kama wewe?

Acha kusobokea mambo usiyoyafahamu, usikurupuke, kama huna la kusaidia kaa kimya
 
Rudi ktk mada mkuu.
Kutoka Dsm mpaka Ikwiriri ni Km 160 na barabara ni ya lami, hapo Ikwiriri ndipo kuna daraja la Mkapa.

Daraja hilo lina urefu wa mita 800 hivi, pana upepo mkali sana hapo darajani. Kutoka Ikwiriri baada ya kuvuka daraja unaanza kipande cha vumbi, hicho kipande ni km 60 mpaka Somanga. Kuanzia Somanga kwenda mbele huko ni lami tupu mpaka Ntwara.

Sijui kutoka Somanga mpaka Ntwara ni km ngapi. Wengine watajazia taarifa unazotaka.
 
Dar hadi Mtwara kuna umbali wa kilomita 589, barabara ni ya lami na inapitika mwaka mzima isipokuwa kuna kipande chenye urefu wa kilomita 60 baada ya kuvuka daraja la Mkapa bado haina lami, lakini inapitika kipindi hiki cha kiangazi. Yapo mabus mengi yanayofanya safari za kwenda mtwara kila siku saa 12 asubuhi. Usafiri wa anga pia upo kila siku.

Mtwara haina hoteli nzuri sana za kulala, zipo lodges kama Msemo, Lutheran hostel, Igunda lodge, VETA au unaweza kulala Old Boma Mikindani.
 
Rudi ktk mada mkuu.
Kutoka Dsm mpaka Ikwiriri ni Km 160 na barabara ni ya lami, hapo Ikwiriri ndipo kuna daraja la Mkapa.

Daraja hilo lina urefu wa mita 800 hivi, pana upepo mkali sana hapo darajani. Kutoka Ikwiriri baada ya kuvuka daraja unaanza kipande cha vumbi, hicho kipande ni km 60 mpaka Somanga. Kuanzia Somanga kwenda mbele huko ni lami tupu mpaka Ntwara.

Sijui kutoka Somanga mpaka Ntwara ni km ngapi. Wengine watajazia taarifa unazotaka.

Asante sana mkuu!
 
Back
Top Bottom