Inflation ya hatari, Mchele kilo 2800?

Mkuu ni hatari sio sh2800, huku mitaa flani ni tsh 3000 mpaka 3200 kwa kilo ya mchele, mpaka 2015 wakati wa uchaguzi akili itakuwa ishatukaa sawa na kujua kuwa CCM sio, viongozi wetu wamebaki kuhudhuria misiba na kukenua meno tu kwenye mikusanyiko ya watu.
 
When there are no further means, people will begin to think seriously. As long as there are still several options, business is as usual.
 
Hivi inawezekanaje mchele kilo 2800? viongozi hawafanyi kitu? Mi na kashule na kakazi kangu shughuli naipata sasa yule mwenzangu na mimi inakuwaje? Imagine this is May, come december mtaniambia.

Zile hela za ziara za mawaziri mikoa ni kuwaambia wananchi nini kimefanywa na serikalli yao nashauri wakanunue grains nje waziflood sokoni kushusha bei. Ile hifadhi ya chakula SGR vipi mbona wameshindwa kucurb price hikes za vyakula? au ndo siasa nao. Life is too tough.

Unajua nchi hii kila mtu huwa anajifanya ni mchumi ivi mkuu nani alikwambia INFLATION ni kupanda kwa bei ya kitu flani pekee,kwa kukusaidia inflation refers to a rise in the general level of prices of goods and services in an economy over a period of time,ukisahau neno "general" ni kosa kichumi,haihitaji uwe na shahada ya kwanza ya uchumi kutoka pale UDSM ili uelewe vitu vidogo kama hivi hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza pale THE AMAZON COLLEGE anajua mambo hizi.............!
 
Huku mikoani nadhani mambo yanaanza kuwa mazuri,juzi nimepita pale sengerema watu wameanza kuvuna bei imeshuka mpaka 1300/=kwa kilo moja lakini cha kushangaza kilometa 40 tu, kutoka hapo ukivuka ziwa ni Mwanza mjini bei ni 2000/=per kg.
 
Unajua nchi hii kila mtu huwa anajifanya ni mchumi ivi mkuu nani alikwambia INFLATION ni kupanda kwa bei ya kitu flani pekee,kwa kukusaidia inflation refers to a rise in the general level of prices of goods and services in an economy over a period of time,ukisahau neno "general" ni kosa kichumi,haihitaji uwe na shahada ya kwanza ya uchumi kutoka pale UDSM ili uelewe vitu vidogo kama hivi hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza pale THE AMAZON COLLEGE anajua mambo hizi.............!

Nyie wachumi wa madesa ndo mnatupeleka huku, mbona jamaa kaeleweka? au ulitaka aorodheshe vitu vyote ambavyo bei zimepanda ndo uelewe?
 
Mkuu tunakufa kimyakimya bila kupiga kelele!

Mwezi uliopita mchele ulikuwa unauzwa Tsh. 2300
Mwezi huu ni Tsh. 2800
ongezeko ni Tsh 500 bila change
Mwezi wa kumi na mbili mwaka jana mchele uliuzwa Tsh. 1700 mpaka 2000.

Poleni sana,huku kwetu umeshuka bei toka 2200 hadi kufikia 1500 so karibu Mwanza.
 
Dr alisema tuchague cdm simenti na mabati yawe buku tano hamkusikia na hamkulinda kura haya mchele buku 3 tusilaumu,2015 tusifanye kosa!!!
 
Hayo ndio matokeo ya baba zako na bibi zako walioichagua CCM mwaka 2010,sasa waache wakione cha moto,na bado mimi naomba ifike buku tano kabisa ili ndugu zako watie adabu ili 2015 akili ziwe zimewarudi!

tatizo sio bibi,babu wala mtu mwenye uelewa mdogo wa kuichagua ccm tatizo ni sisi wenye uelewa je tunachukua hatua gani kukomesha ujinga huu?
 
Kwa sehemu ninayoishi 2800 ni bei ya Decembre 2011.Sasa hivi bei elekezi ni 3000 kwa kilo ya mchele.
Na sioni kama kupanda huku kwa bei za bidhaa ni tatizo,maana cc watz huwa hatushindwi kununua,hata bei ikipanda vp watu watanunua tu,ukishindwa utashindwa peke yako!Kifupi cc watz ni makondoo,hata wauzaji wa bidhaa wanajua hili.Pengine hii ni kwa sababu hela za wengi wetu ni za magubegube,kwa hiyo haziumi.Pandisha bei ya bidhaa Ulaya uone!Tazama hata humu badala ya kuona kuwa hili ni tatizo,tunaanza kulumbana!Ha ha ha ha!Tza ni zaidi ya uijuavyo!
 
hahahahahahahaha ngoja nicheke nafikiri Ilala Temeke na kigamboni na majimbo mengine ya dsm waliochagua CCM nakufunga kanga na kucheza ngoma mnaipata fresh na hili liwe somo kwa wewe uliyekuwa unamshangilia Mahanga kushinda Kesi kwani unamchango wako katika kuwafanya watoto wa familia yako wali wali sikukuu hadi sikukuu. pole wewe unayehongwa kanga na husikii la mnadi swala wala kengeli ya kanisani wanaekutaka usali na utambue kuwa Mungu kakupa Akili ya kupembue mbichi na mbivu kwa kuweza kujua jinsi serkali yako inavyokufanya watoto na ndugu zako wa karibu washindwe kupata chakula kama haki ya msingi kwa bei nzuri. Pole wewe unayeona kijani na manjano ni kila kitu tz. Pole wewe mzee wa Dar es Salaam unayeitwa kwenye mkutano wa mheshimiwa sana na kupiga makofi kwa kushangilia kinafiki mimi kasimba123 nakupa pole.

Mungu yu mwema alianza na mafuta sasa kaja na vyakula ilikuweza kuwafungua wale ambao bongo zao zimelala kuwa wanahitaji kujikomboa kwani hakuna kinachotia uchungu kama kuona familia inalala njaa wakati baba upo ndani umekosa 3000 kununua msosi poole sana na ahsante Mungu kwani hakika Yu mwema

Poleni na hizo ni salaam tu
 
Changamoto zinazojitokeza humfanya kiumbe chochote kutafuta namna ya kukabiliana nayo. Watz hatutakuwa tofauti, ni lazima tutafute suluhisho au namna ya kukabiliana na changamoto hii ya mfumuko wa bei. Shauku yangu hata huku kupanda kwa bei hakujatosha kuwa changamoto kwa Watz, kwani kama alivyosema mmoja wetu tumekuwa kama kondoo. Zambia mkate ulipanda bei kidogo tu watu wakamininika barabarani. Hapa kwetu wafanyabiashara(sio wakulima) wamekuwa na power kubwa ya kuwaendesha Watz kwa kisingizio cha soko huria, wanawanyonya Watz hadi tone la mwisho. Ni lazima tuamke, tujipiganie wenyewe, tukisubiri serikali ya sisiem ya wakulima na wafanyakazi ikutetee itakula kwako. Kama huwezi kupigana kuzuia inflation, basi pigana kuhakikisha kuwa kipato chako kinakuwa kikubwa kukabiliana na hiyo inflation.
 
Back
Top Bottom