The Pentagon
Member
- Apr 20, 2016
- 19
- 16
Zanzibar ni too blind na dini kwa kweli hili ni shida ni ngumu kupiga hatua kama umekumbatia dini sana
Wanabodi,
Nimekuwa nikipitia matokeo ya form four kwa baadhi ya shule za Zanzibar, kwa shule nyingi nilizopitia, nimeshangazwa kukuta Div I, Div II, na Div III ni chache sana!, kule zimejazana zaidi Div IV na Zero kiasi kwamba kuna baadhi ya shule, shule nzima imepata Div 0!, hii inakuwaje?!. Jee kuna uwezekano kuna tofauti ya akili kati ya Watanzania Bara na Watanzania Visiwani?.
Set up ya baadhi ya taasisi za muungano, zinalazimisha kwenye top management, kama ni bara, deputy, lazima atoke Zanzibar!, moja ya taasisi hizi ni BOT, Gavana akitoka bara, Deputy lazima atoke Zanzibar!, lakini kwa miaka mingi, ile nafasi ilikaa wazi kwa kisingizio kuwa hakukuwa na Mzanzibar mwenye sifa, nilipouliza sifa gani, nikaelezwa lazima awe mchumi aliobobea kwa uzoefu usiopungua miaka 10!. Mimi nilidhani ni visingizio tuu, lakini kama matokeo ya wenzetu hawa ndio haya, na Tanzania ni nchi ya muungano, linapokuja suala la recruitment professionals wa muungano, itakuwaje?!.
Nimebahatika kusoma na kijana mmoja wa Kizanzibari pale UD, ile tumeingia tuu mwaka wa kwanza, kwa fedha za boom, alioa mke wa kwanza, mwaka wa pili akaoa mke wa pili!, mwaka wa tatu akaoa mke wa tatu!, tulipomaliza mwaka wa 4, alisema anakwenda kukamilisha idadi ya mwisho 4, ila kiukweli jamaa alikuwa fit sana upstairs, bado sipati jibu, ikiwa ni kweli Zanzibar ina Div I, Div II, na Div III, chache, hii itakuwa imekaaje kimuungano!. Jee kuna uwezekano kuna tofauti ya akili kati ya Watanzania Bara na Visiwani?!.
Ikithibitika ni makosa ya utungaji mitihani ambayo "sio", usahihisaji au upangaji matokeo, then yule mama wa NECTA, atakuwa hana jinsi, lazima awajibike akitanguliwa na waziri wake!.
Pasco.
Kwa masikitiko makubwa naomba kuwauliza wenzetu wa Zanzibar swali ambalo kwa kweli limekuwa likinitatiza miaka mingi sana. Nalo ni udhaifu mkubwa sana wa taaluma ya Zanzibar ndani ya baraza la mitihani NECTA.
Cha ajabu kabisa ni kuwa, wakati Zanzibar hiyo ikiwa hoi mbele ya NECTA, wapo Wazanzibar wengi sana ambao ni wana vipaji vya hali ya juu sana mfano kina Mohamed Gharib Bilal na wengine wengi sana. Hawa wana vichwa vilivyojaa vipaji.
Katika matokeo ya kidato cha sita ACSEE-2016 Unguja pekee imetoa shule saba kati ya kumi za mwisho, nini tatizo?
Siongelei kuhusu swala la ghafla bin vuu shule kongwe za serikali za vipaji kurudi kwenye chati maana hilo linahitaji uchambuzi wake. Ni wachache watakaoamini kuwa shule zote kongwe za serikali za vipaji kurudi "top ten" kwa kishindo kumetokana na jitihada binafsi za wanafunzi. Shule zote nne? Hapana! Hili tutakuja kulichambua baadaye! Kwanza niwaulize hawa watani zetu, nini tena kimewapata?
Shule 10 zilizofanya vibaya:
1.Mpendae-Unguja
2.Ben Bella-Unguja
3.Tumekuja-Unguja
4.Green Bird Boys-Kilimanjaro
5.Jang'ombe-Unguja
6.Kiembe Samaki-Unguja
7.Tanzania Adventist-Arusha
8.Al- Ishan Girls-Unguja
9.Azania-Dar es Salaam
10.Lumumba-Unguja
Pasco,
Usipindishe hoja na kuharibu mjadala. Umeanza vema kwa kuonesha shida ya matokeo kwa shule za Zanzibar (matoke ambayo ni mabaya kwa nchi nzima), hilo liko sawa. Sasa kama Zanzibar wamefeli 'zaidi', huyu mwanamama anahusikaje na usahihishaji? Kama syllabus inayotumika Zenji na bara ni moja, kwa nini Ndalichako alaumiwe linapokuja suala la wanafunzi kufeli mitihani? Nimesoma na Wazanzibari kwa miaka mingi tu bara, tangu sekondari, wako vema sana upstairs kama walivyo wanafunzi wengine. Inawezekana kuna mazingira flani ambayo si 'wezeshi' kwa upande wa visiwani Zanzibar ambayo yanafanya performance ya wanafunzi iwe chini, lakini sio shida ya usahihishaji! Tujipe homework ya kuangalia shida ilipo kwanza, kabla ya kunyosheana vidole!
Katika matokeo ya kidato cha sita ACSEE-2016 Unguja pekee imetoa shule saba kati ya kumi za mwisho, nini tatizo?
Shule 10 zilizofanya vibaya:
1.Mpendae-Unguja
2.Ben Bella-Unguja
3.Tumekuja-Unguja
4.Green Bird Boys-Kilimanjaro
5.Jang'ombe-Unguja
6.Kiembe Samaki-Unguja
7.Tanzania Adventist-Arusha
8.Al- Ishan Girls-Unguja
9.Azania-Dar es Salaam
10.Lumumba-Unguja
Unataka kumzuia asiseme anachowaza.acha udini mkuu utaharibu thread nzuri hii.
Jee kuna uwezekano matokeo mabaya ya Zanzibar na shule za dini fulani yanahusiana na imfluence ya dini hiyo kwenye akili za waumini?!, au ni imfluence ya Waarabu?!.
Pasco
Hahaha wewe jamaa unaweza ukawa mtabiri aseeeDr. Ndalichako ni shupavu hata kuliko Kikwete, Billal Mikasi, Pinda Nyuki kwa upamoja
Wanakunywa mtundula...Iyo shule ya wasabato arusha nasikia jamaa hata majani ya chai hawatumii wala soda,wapo busy na dini sana! Wanatakiwa wabalance kati ya mafundisho ya dini na elimu za humu dunia pia.Likewise shule za unguja la sivyo wasubirie jecha afute matokeo
mkuu umenenaDini ku-influence matokeo ya darasani ni swali muhimu.
Lakini tujiulize, vipi Irani, Egypt, Algeria, Saudi Arabia na maeneo mengine duniani ambako wakazi wengi ni wa 'dini' hiyo, hali ya elimu ya kimagharibi ikoje?
Kuhusu Zanzibar, maoni yangu ni kwamba kuna mgongano mkubwa kati ya imani za kitamaduni za wazanzibari na imani za 'dini'. Mgongano huu wa imani hizi ni kama umepea zaidi kwenye imani potofu zinazofifisha ustawi wa jamii badala ya kuzamia kwenye imani chanya zinazohanikiza maendeleo.
Ni jukumu la 'scholars' wa dini na scholars wa sayansi ya ustawi wa jamii kuwakwamua Wazanzibari hapa walipokwama.
Duuuh shida kweli kweli, kipi kifanyike ili hawa watu wanyanyuke kielimuMimi ni mwl wa chuo kikuu nchini zaidi ya miaka 20. Nimewafundisha wanafunzi kutoka zanzibar. Wengi ni dhaifu sana kwenye masomo. Usiombe upate mwanafunzi wa ku supervise dissertation, hapo ndipo utakapojua uzito wa kazi hiyo. Tuseme kweli wengi ni wadhaifu hata wale waliomaliza na GPA nzuri ktka degree ha kwanza.