Inawezekana niamkie Kariakoo na kupata kipato ikiwa sina ofisi wala chochote?

Inawezekana niamke asubuh na kwenda kariakoo ikiwa Sina office yeyote hapo ???? Udalali huwa unafanywaje jamani
Mkuu Kuna biashara nzuri ambayo watu hawajaigundua, fanya biashara ya kuuza ndizi za kuchoma kwenye mkaa. Tafuta ndizi flani sijui zinaitwaje, ni nzuri sana kwa kuchoma we kachome hizo uza 3 buku, kumbuka watu wengi hawataki vitu vya mafuta so ndizi utauza, ukifanikiwa ulete zaka kwangu.
 
Nimekuonea huruma sana, ngoja nikuombee watu waje wakupe mwanga kwakuwa una mwamko wa kufanya kazi.

MamaSamia2025 Wewe si una connection hadi kwenye machimbo China? Naamini huku pia una fahamu
Nelson Jacob Kagame Wewe mtoto wa mjini hukosi kujua...
Tuisaidie jamii sio kuwapa ubuyu tu...
Huyo nelson alikua dereva wa magari ya wakimbiz kule kigoma atoe connection
 
Wakinga na Wachaga au watanzania wanaoagiza mzigo kutoka China mara nyingi huuza wenyewe mizigo yao tofauti na wachina. Wachina huagiza mizigo kwao kwa simu tu, ambao naamini bei zao za manunuzi huko kwao zina punguzo maalum (kwa maana raia wa nchi mzigo utakapo) hivyo kufanya mzigo wanayo agiza wao kuwa cheap.

Kwa kujibu swali lako, ni hivi, wao wachina mfano kwa case ya viatu ama yeboyebo na bidhaa nyingine, hufungua mzigo wa aina mpya karibu kila siku.

Yale maduka uyaonayo wanaweka tu display lakn mzgo hasa huwa store eneo lingine. Sasa katika zile aina tofuati, huwa kunatokea ambayo hupendwa na wateja kupitiliza. Kwahiyo wewe dalali kwa hela yako, unaenda kwa huyo muuzaji unaununua huo mzigo wote kisha unauuza wewe kwa kuongeza bei kidgo juu yake. Lakn hapa lazma uwe na mtaji na ujulikane na ulijue soko vizuri.

Ukishakuwa tajir na una hela ya kutosha, basi ukisikia mfano (usininukuu lakan) kipodizi fulani original kinatembea sokoni wewe unapanda fasta china kwenda kuleta feki yake. Ukisikia piituuu zinakimbia wanaenda kuleta feki yake nk. Kwahiyo lazma uwe na mtaji na lazma uwe na uzoefu kdgo wa kuwa maeneo husika na kukutana na watu husika.

Ushauri wangu kwa Serikali mara zote ni mmoja tu, wasiruhusu importers hasa wakigeni kuwa retailers at same time. Hakuna sehm duniani wanaruhusu hilo. Yaani mchina anapoagiza mzigo kwao anakuwa na punguzo la bei, yy hasafiri zaidi ya kuagiza. Akifika hapa anashindana na raia ambaye ana container chache anayenunua bei juu huko china, ana mkopo wa riba kubwa kodi nyingi wanashindania soko moja.

Duniani kote ujasusi wa uchumi ni kulinda mapato ya nchi na kuwalinda ama kuwapa upendeleo raia wako kwny soko la nchi yako dhidi ya mgeni, ikiwepo Ajira.

Kwa kufanya hivyo Serikali inatakiwa iwe na sheria moja kali sana, wachina na raia wa nje wanapo import mizigo kwa bulk kutoka nje, wasiruhusiwe kuuza rejareja wakishindana na mmachinga. Chukulia muhindi aagize mitumba halafu baada ya kuagiza na yy auze rejareja karume ilala tandika nk.

Muhindi akifanya hivyo lazma ataua kazi za wamachinga. Kwahiyo endapo Serikali ingewatengea importers eneo lao na kupiga marufuku importers kuwa wauzaji rejareja, kwa swali lako inamaana mtu yoyote kwa mtaji wowote anachagua niche yake, anaenda kununua kwa wachina kisha anauza rejareja, hapa Serikali inakuwa imetengeza Ajira na kodi mpya na imelinda raia wake.

Hivi Mtanzania anaruhusiwa kwenda china halafu aagize mzgo kutoka Tanzania na kisha akiwa kule auuze rejareja? Ataambiwa umeshaleta china sharti uuze kwa mchina, baada ya hapo tembea. raia wao watauza wenyewe rejareja kwa bei zao.
 
Mkuu Kuna biashara nzuri ambayo watu hawajaigundua, fanya biashara ya kuuza ndizi za kuchoma kwenye mkaa. Tafuta ndizi flani sijui zinaitwaje, ni nzuri sana kwa kuchoma we kachome hizo uza 3 buku, kumbuka watu wengi hawataki vitu vya mafuta so ndizi utauza, ukifanikiwa ulete zaka kwangu.
Auze na mishkaki nikiwaga kariakoo ndio chakula changu nikiwaga kariakoo
 
Wakinga na Wachaga au watanzania wanaoagiza mzigo kutoka China mara nyingi huuza wenyewe mizigo yao tofauti na wachina. Wachina huagiza mizigo kwao kwa simu tu, ambao naamini bei zao za manunuzi huko kwao zina punguzo maalum (kwa maana raia wa nchi mzigo utakapo) hivyo kufanya mzigo wanayo agiza wao kuwa cheap.

Kwa kujibu swali lako, ni hivi, wao wachina mfano kwa case ya viatu ama yeboyebo na bidhaa nyingine, hufungua mzigo wa aina mpya karibu kila siku.

Yale maduka uyaonayo wanaweka tu display lakn mzgo hasa huwa store eneo lingine. Sasa katika zile aina tofuati, huwa kunatokea ambayo hupendwa na wateja kupitiliza. Kwahiyo wewe dalali kwa hela yako, unaenda kwa huyo muuzaji unaununua huo mzigo wote kisha unauuza wewe kwa kuongeza bei kidgo juu yake. Lakn hapa lazma uwe na mtaji na ujulikane na ulijue soko vizuri.

Ukishakuwa tajir na una hela ya kutosha, basi ukisikia mfano (usininukuu lakan) kipodizi fulani original kinatembea sokoni wewe unatemb
 
1.Cheza maeneo ya karibu na ofisi hasa zile za mizigo.,wanaposhusha mizigo huwa kunakuibeba kupanga ofisini.
Pia Kaa nao vizuri,,huwa kuna kubeba kupeleka kwa wateja
(Hapa cheza na zile ofisi zilizo maghorofani sanasana)

2.Zunguka kukusanya takataka maofisini kwa bei nafuu.
Kariakoo huwa hakuna sehemu za kutupa taka hivyo zikijaa namna ya kutupa huwa ni changamoto.
Hakikisha unapita mara kwa mara maofisini...punguza bei ya huduma ili upate wateja

3.Mchana unaweza kujumuika na wale vijana wanauza nguo za mtumba,Hasa vijora...wanaimba sana na kupiga makofi,huku wamama wakichagua.

*Hizi ntakazoweka ni nzuri ila sidhani kama zitakufaa kwa sababu bado huna pesa;

4.Asubuhi zungusha mayai ya kuchemsha
Target yako iwe kwenye maofisi...watu wananunua wananywea chai.
Hapa unaweza kujiongeza kuweka vitafunwa vingine.

5.Ungekuwa na vitendea kazi,Kuna mtu huwa anazunguka kupima presha watu maofisini.

5.Ipo biashara ya maji,ila inahitaji uvumilivu..Zungusha maji ya kunywa ofisini.

6.Biashara ya kuuza chakula.

7.Ingia Karume mtumbani,chagua nguo nzurii jeans na nightdress ,yaani zile nguo light za kuvaa wadada Hasa muda wa joto.
Komaa zungusha,target wateja kulingana na nguo ulizonazo.
Pitisha maofisini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom