Inasikitisha naomba ushauri wako mwana JF

gfsonwin hakika umempa ushauri mzuri ila nami naongeza kidogo, afanye utafiti kujua kama huyo mtoto ananyanyaswa na mkeo. Wakati mwingine unaweza kudhani kila kitu ni sawa kumbe mkeo anampa mateso na vitisho kama "ukisema nakuua". YOU NEVER KNOW.

Mi sikubaliani na hilo kwani jana wife hakuwepo nyumbani alirudi jioni na kunikuta mimi ..........na yeye ndiye alikuwa wa kwanza kumuuliza nini tatizo na kumueleza umuhimu wa elimu.
 
Mimi nilikuwa nimeamua kwanza nimrudishe Dodoma kwasasa matokeo yakitoka ndio nijipange.

never do this aisee,
kama una moyo wa asubira, upendo, uvumilivu na utash usmrudishe kaa nae na kata mawasiliano yyte na nje yaani hao mama wadogo/wakubwa na wengine wote.
 
never do this aisee,
kama una moyo wa asubira, upendo, uvumilivu na utash usmrudishe kaa nae na kata mawasiliano yyte na nje yaani hao mama wadogo/wakubwa na wengine wote.

kaka unaushauri mzuri sana ila....................
 
Umenikumbusha wakati nilipo maliza drs la 7 sikupataga bahati ya kuchaguliwa sec. Mjomba wangu alinifanyia mpango wa kurudia shule katika kijiji kingine mbali na kile kijiji chetu. Tulipokwenda kufika kule ajaniacha tayari kwa kuanza na kuendelea na masomo na yeye akaondoka kurudi kijijini kwetu. Nilipokaa siku ile pale ugenini pasipo uwepo wake nilijiona mpweke sana na yale mazingira hayanifai. Hivyo asubuhi iliyofuata nilirudisha daftari kwa mwl.mkuu,mana nilikabidhiwa na madaftari mapya ya kuanzia masomo. Niliporudi nyumbani nikachukua vinguo vyangu na kuanza safari ya kurudi kule kijijini kwetu. Njiani nilikutana na mjomba anarudi kule kijijini aliko niacha kuna kitu alikuwa amesahau. Alipo niuliza vipi mbona unarudi nyumbani nilimjibu kama alivyo jibu huyo mtoto hapo kwamba mimi siwezi kukaa kule kwani sipapendi. Basi mjomba alivunja fimbo pale pale na kunitandika sana na kunirudisha mpaka kule shuleni na aliamua kukaa kule kunisimamia kwa muda wa wiki nzima mpaka nilipozoea mazingira na nilisoma hatimae nilifaulu kujiunga na sekondari mpaka muda huu nina kazi yangu nzuri na ninamsaidia hata yeye. Hivyo usimchukulie hasira huyo mtoto kwani wakati mwingine watoto huwa hawafamu faida za lile jambo lililo mbele yake. Hapo alipo ameimis ile company yake kule alilotoka lakini baadae atazoea tu mazingira.
 
Huo ni hofu kama walivyosema wengine, yaani anahisi kuna mapungufu kisaikolojoia. Nakumbuka tuliwahi kuwa na house girl kutoka Dodoma, kwa mujibu wa ndugu zake, alikuwa anapenda sana kufanya kazi DSM, ila alipofika nyumbani akawa anakasirika. Mama alipanga baada ya muda kumpeleka shule ya ushonaji lakini bado hakuridhika na mazingira.

Siku moja nikafanikiwa kumdadisi, ndipo akaniambia ya kwamba amezoea kuimba na bibi yake jioni, kucheza na wadogo zake, kupiga stori na rafiki zake, kulima karanga n.k vitu ambavyo havipati, kisha aliamua kuondoka na sasa tulipata habari tayari ameshaolewa.
Huyo mtoto atazoea tu na kufurahia mazingira, pia hakikisha anapata nafasi ya kuchangamana na wenye umri kama wake, usisahau kuwa nae karibu na kumueleza unachotaka kufanya kwa ajili yake. Mtoto wa ndugu yako ni wa kwako.
 
Pole sana ndugu yangu, wadogo zetu ndivyo walivyo lazima uchezenao kwa saikologia yao, mi nafikiri usikate tamaa, kaa naye, mwambie kwanini hasa unataka kumsaidia, mfungue kidogo maisha yalivyo kama hata soma, na pia labda kuna jambo kaliona japo ni mapema naye angekuwa mvumilivu kidogo, na zaidi kama unakauwezo ndugu yangu mpeleke boarding school hapohapo moro huku anaaweza funguku zaid, huwez jua labda kaona mazingira fulani akajua wenyeji wake ni wakali, please usikate tamaa ili ikishindikana baadaye damu yake isiwe kwako
 
Hili limetokea sasa hivi naomba ushauri wako ili angalau maamuzi yangu yasiwe mabaya.

Mimi nina ndugu yangu amabaye ni mtoto wa Mama yangu mdogo yeye kwa sasa ni marehemu ambaye alijaliwa kuzaa watoto wanne wakike wawili na wakiume wawili, sasa nilipokwenda liziko mwezi uliopita nilikuta yule mtoto wa mwisho yupo darasa la saba. Nilipomuona hali waliyokuwa nayo hao watoto mimi niliona ni bora nimuhaidi kuwa atakapomaliza darasa la saba nitamsomesha hadi hapo atakapopata mafanikio na kuwa mkombozi wa familia yao.

Niliona kwa kipindi atakachomaliza elimu ya darasa la saba basi aje nyumbani kwangu Morogoro ili aweze kujiandaa na mitihani ya shule mbalimbali kwa kusoma pre form one ili atakapoanza mipango ya kupata shule basi yeye interview iwe rahisi kwake na aweze kupata shule.

Jana amekuja kwa kusafirishwa toka Dodoma alipofika mimi kutokana na mihangaiko sikuweza kukaa nae nakumueleza cha kufanya na nini nimemuandalia kwaajili ya masomo yake. Basi leo nilitembelea shule mbili na kuchukua form kwaajili ya kupata nafasi.

Niliporudi mchana baada ya kupata chakula cha mchana na familia yangu basi walikwenda kulala wote mimi nikiwa nachat alinifuata sebuleni na kuniambia kuwa yeye hawezi kukaa kwangu kwani maisha haya hatoyaweza. Nikamuuliza kunatatizo gani? akasema yeye hawezi kukaa nilishtushwa sana kwani huyu mtoto ni mdogo ana umri wa miaka kumi 13 sasa. Mimi nilijiuliza maswali mengi na kukosa majibu ndipo nikampigia dada yake ambaye mimi ni mdogo wangu na kumueleza yeye alianza kwa kulia na kusema nimwambie akirudi yeye si ndugu yake. Kumbuka huyu mtoto hakuwa anaishi na dada yake yeye ndio anajua maisha anayoishi huko aliko kwa mama yake mkubwa.
Dada yake akasema nisimruhusu nikae nae mimi naona kama huyu mdogo wangu anaweza kuniletea matatizo mbeleni kwani ameonesha picha mbaya mapema sana.

Mimi baada ya kufanya mawasiliano na baadhi ya ndugu niliamua kumwambia kesho nitakusafirisha na urudi huko utakakoishi maisha unayotaka . Baadae baada ya kuongea na dada yake akaja na kuniomba msamaha eti anaomba aendelee kubaki mimi nikamuuliza kwanini? hana jibu sasa mimi uamuzi wangu ni kumruhusu aende ili asije leta matatizo katika familia yangu. Mimi hapa ninaishi na mke mtoto mmoja pamoja na mtoto wa kazi hakika Mungu ametujalia maisha ya kuweza hata kubadilisha mboga mara moja moja. Na hata makazi yetu yanaridhisha . Naomba ushuri wako ili niondokane na hili jambo au kwa kusaidia au kutokusaidia kwani mimi naona bora hata nikatafuta mtu baki na mkumsaidia sasa hivi hapa namuangalia yupo mezani anapata chakula.

kwa maelezo ya mtoa mada i can truly gues what his blood type is!
Na kwa msaada zaidi plz u can go through da children's guidance and counselling's articles!
Hali hiyo ni normal sana with da consideration of da kid's age!
 
Nimewaelewa wana JF ngoja nikapumzike kesho nitapitia hapa kabla ya uamuzi wangu kuuchukua ila nimepata ushauri mzuri sana .
 
kwa maelezo ya mtoa mada i can truly gues what his blood type is!
Na kwa msaada zaidi plz u can go through da children's guidance and counselling's articles!
Hali hiyo ni normal sana with da consideration of da kid's age!

haya bwana hata ukinitukana ila nilikuomba ushauri tu
 
mimi nakuomba uubebe huu msalaba kwani ukimsaidia huyo mtoto hata yule marehemu ndugu yako atakushukuru atakapomwona mwanae amefanikiwa,vikwazo ni kwa kila mtu usikate tamaa na kitu kingine lazima ujue mtoto anaona karibu ila wewe unaona mbali hivyo ujue kua hizo ni akili za utoto tu!na ukimruhusu aende dodoma hawezi kurudi tena, na pia umwandae mkeo kisaikolojia ili ampende na kumjali huyo mtoto kama wake; ni hayo tu!
 
Nimekuelewa kwa yote ila ni wazi kuwa labda house girl ndio atakuwa amemtisha ila mke wangu ndiye aliyetoa pendekezo la kumsomesha huyu mtoto. Hata hivyo kunauwezekano alikotoka ameambiwa aje acheki kwanini kuna mama yetu mkubwa ndio anakaa nae sasa mara baada ya kumaliza darasa la saba na amekuwa kama mfanyakazi wake wa ndani na dada yake amesema anauza ice cream sasa uwezekano mkubwa wapo watu waliomfeed ujinga.
Ndio maana nataka kmrudisha kwanza akajipange upya na kutafakari maana wakati anaongea alikuwa anaconfidence za ajabu huku akitoa sauti ambayo mimi mwenyewe sikuelewa. Na hata nilipotoa taarifa huko nilipomchukua basi walisema mpakie kwenye basi kwani nyumbani anakujua atakuja mwenyewe mara niliposema wampokee ......

hivyo hapa mimi naona naweza kujikuta naiingia kwenye matatizo kwa huyu mtoto ....

Inawezekana kweli hose girl labda kaona ushindani (kama ni binti mdogo labda alijua amekuja kumreplace hivyo akaanza kujidefend). Ni habari njema kama wife wako anasapoti. Kaa naye huyo mtoto wa kike msaidie asome!
 
kaka unaushauri mzuri sana ila....................

ila nini?..............usiogope maisha yana changamoto sana na hizi hazikimbiwi bali lazima uziface kwani umesharisk mangapi toka ukue na akili yako?

imagini ulipommimba mkeo hukurisk maisha yako? ama unapoendesha gari hurisk maisha yako? basi sasa na hili nalo lazima urisk.
 
Hili limetokea sasa hivi naomba ushauri wako ili angalau maamuzi yangu yasiwe mabaya.

Mimi nina ndugu yangu amabaye ni mtoto wa Mama yangu mdogo yeye kwa sasa ni marehemu ambaye alijaliwa kuzaa watoto wanne wakike wawili na wakiume wawili, sasa nilipokwenda liziko mwezi uliopita nilikuta yule mtoto wa mwisho yupo darasa la saba. Nilipomuona hali waliyokuwa nayo hao watoto mimi niliona ni bora nimuhaidi kuwa atakapomaliza darasa la saba nitamsomesha hadi hapo atakapopata mafanikio na kuwa mkombozi wa familia yao.

Niliona kwa kipindi atakachomaliza elimu ya darasa la saba basi aje nyumbani kwangu Morogoro ili aweze kujiandaa na mitihani ya shule mbalimbali kwa kusoma pre form one ili atakapoanza mipango ya kupata shule basi yeye interview iwe rahisi kwake na aweze kupata shule.

Jana amekuja kwa kusafirishwa toka Dodoma alipofika mimi kutokana na mihangaiko sikuweza kukaa nae nakumueleza cha kufanya na nini nimemuandalia kwaajili ya masomo yake. Basi leo nilitembelea shule mbili na kuchukua form kwaajili ya kupata nafasi.

Niliporudi mchana baada ya kupata chakula cha mchana na familia yangu basi walikwenda kulala wote mimi nikiwa nachat alinifuata sebuleni na kuniambia kuwa yeye hawezi kukaa kwangu kwani maisha haya hatoyaweza. Nikamuuliza kunatatizo gani? akasema yeye hawezi kukaa nilishtushwa sana kwani huyu mtoto ni mdogo ana umri wa miaka kumi 13 sasa. Mimi nilijiuliza maswali mengi na kukosa majibu ndipo nikampigia dada yake ambaye mimi ni mdogo wangu na kumueleza yeye alianza kwa kulia na kusema nimwambie akirudi yeye si ndugu yake. Kumbuka huyu mtoto hakuwa anaishi na dada yake yeye ndio anajua maisha anayoishi huko aliko kwa mama yake mkubwa.
Dada yake akasema nisimruhusu nikae nae mimi naona kama huyu mdogo wangu anaweza kuniletea matatizo mbeleni kwani ameonesha picha mbaya mapema sana.

Mimi baada ya kufanya mawasiliano na baadhi ya ndugu niliamua kumwambia kesho nitakusafirisha na urudi huko utakakoishi maisha unayotaka . Baadae baada ya kuongea na dada yake akaja na kuniomba msamaha eti anaomba aendelee kubaki mimi nikamuuliza kwanini? hana jibu sasa mimi uamuzi wangu ni kumruhusu aende ili asije leta matatizo katika familia yangu. Mimi hapa ninaishi na mke mtoto mmoja pamoja na mtoto wa kazi hakika Mungu ametujalia maisha ya kuweza hata kubadilisha mboga mara moja moja. Na hata makazi yetu yanaridhisha . Naomba ushuri wako ili niondokane na hili jambo au kwa kusaidia au kutokusaidia kwani mimi naona bora hata nikatafuta mtu baki na mkumsaidia sasa hivi hapa namuangalia yupo mezani anapata chakula.

mkuu inaweza kukuletea matatizo na familia yako usipokua makini , kwa haraka haraka ongea na familia yako vizuri kuna uwezekano mkubwa wakati ulikuwa katika mambo yako ni ngumu kumeza ila walisha mnyanyapaa huyu kijana mdogo full dozi.

sasa kutokana na unyonge wake akajionea bora ya mussa kuliko asiyoyajuwa . pia na wewe pamoja na kuwa na niya ya kumsaidia unatakiwa usikate tamaa kirahisi tumia busara za umri wako utapata black and white. muweke kitako na familia yako umtambulishe akiwa ni member nae katika familia kwa kumuonyesha mapenzi makubwa.
 
Ni kweli nitakuwa makini kama ni mapenzi makubwa ameoneshwa kwa siku mbili hizi sema kuna kitu nafuatilia huko alikotoka inasemekana alikuwa anasaidia kazi na yule aliyemruhusu kuja ndiye amemjaza ujinga.
 
Kuku wa kienyeji huyo!!!

Sasa amefika mahali amekuta mabanda lazima ajiulize mara mbili mbili? Kule shamba alikuwa amezoea vitu vya kienyeji sasa hapo amkuta tofauti kabisa, hivyo jaribu kuwa naye karibu. Usipende kumwongelesha Kiswahili Mkuu piga kikwenu mtoto huyo atafunguka tu!! Ila akija kuzoea mazingira atawazidi hata waliozaliwa mjini. Sisi wengine tulishachoka kabisa na hawa watu wetu wa kijijini. Kumsaidia kutokea huko huko alikkuzoea ndo dawa iliyobaki, hawana fadhila hawa!!!
 
Anahitaji msaada inawezekana ni ushamba anaogopa mazingira yako ya maisha ya kisasa lakini vitoto vya siku hizi ni balaa usikute ana mpenzi wake huko alikotoka sasa anammisi akili yote Dom chunguza kwa makini kisha chukua hatua!
 
Kama wengine walivyosema, shida ni mazingira yanampa shida. Kila kitu kwake ni kigeni na kila anacfanya anaona atadharulika na kuchekwa. Jaribu kumtia moyo wewe na mkeo na baada ya siku si nyingi atapafurahia tu. Hii ni hali yakawaida ya watoto wanapokuwa mahali pageni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom