Inasemekana neno Ikulu, lilitokea kwa Wagogo (Makulu)

Hennes kolon

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
673
1,287
Hii historia ya neno Ikulu nilianza kuisikia miaka kadhaa iliyopita , tangu nikiwa primary, na secondary pia ila ukweli halisi siujui.

Inasemekana pale Dodoma, kulikuwa/Kuna mji unaitwa Mvumi Makulu, nadhani ndio kwao na Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wa Kwanza Mstaafu wa Tanzania John Malecela. Huo mji ulikuwa ndio makao makuu ya mtemi wa Dodoma (Mtemi Mazengo) na makao makuu ya Mtemi kwa kabila la Wagogo waliyaita MAKULU .

Kwa kuwa makao ya mtemi wa wagogo wote , yalikuwa ndani ya mji/Kijiji cha Mvumi , Basi eneo hilo likajulikana kwa jina maarufu la Mvumi Makulu, Hadi leo panajulikana hivyo Kama Mvumi Makulu .

ilikuwaje Makulu makao makuu ya Mtemi Mazengo- Hadi ikulu makao makuu ya nchi (Rais kwa Sasa!?)

Iko hivi: wagogo wanasema mwal. alipokuwa kwenye harakati za kupata kuungwa mkono na watemi/ma chief wa makila yote ya Tanganyika katika harakati za kudai Uhuru kutoka kwa wakoloni, alipofika Dodoma alipokelewa na mtemi mazengo , huko makulu kwake mvumi , baada ya mazungumzo mtemi alikubali na kuunga mkono wazo la mwal. nyerere na akaahidi kumpa ushirikiano wa kila aina , Mali na ulinzi (wa kimila )

Mtemi akatoa baraka zake zote na kumfanyia tambiko hukohuko makao makuu (makulu ya mtemi),baadae mtemi akatoa ombi kwa mwal. ya kuwa atakapofanikisha wazo lake la kuwa unganisha watemi na machief wote kuwa na utawala mmoja na mamlaka moja Basi makao makuu ya utawala mpya yaitwe makulu , mwal. akamuahidi atatekeleza, Basi wagogo wanasema mazengo akatoa na fimbo yake ya utawala akampa mwal. nyerere ikiwa ni ishara ya kumkabidhi mamlaka ya utawala. wagogo husema ndo kale kafimbo ambacho mwal. alikuwa akikiweka kwapani kwake na kutembea nacho , wanadai hako kafimbo kalikuwa na nguvu za kijadi na vimbwanga vyake.

Baada ya kupata Uhuru , mwal. akatimiza ahadi na kuyaita makao makuu ya utawala wa nchi yaitwe ikulu , Hadi leo iko hivyo.
 
Back
Top Bottom