Inaniuma sana

Sep 25, 2012
63
15
....kwamba kuna binadam wasio na hatia wamepoteza maisha wiki iliyopita katika eneo la mashariki ya kati kutokana na "matumizi ya silaha" ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha...na kwamba baadhi ya masheikh na maimamu wetu wa kiislam wamekuwa wawazi mno katika kushutumu( sheikh mkuu wa bakwata mkoa wa tanga kaamrisha duah maalum ya kulaani mauaji ya wapalestina-kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la ijumaa ya tarehe 23-11-2012) mauaji ya wapalestina(waarabu)yaliyofanywa na vikosi vya kiisraeli,inaongeza machungu ambayo msingi wake ni maswali , hofu na hisia mbaya kwa masheikh na maimamu wetu...si siku nyingi zilizopita kulikuwa na taarifa kwa siku zaidi ya nne mfululizo, zikitaarifu juu ya mauaji na madhila waliyokuwa wakifanyiwa waislam(lkn hawa si waarabu) wa burma, lakini kama inavyotokea kwa mauaji ya waislam wengine ambao migogoro na masuala yao si mtaji wa kisiasa kwa watawala wa nchi tajiri za kiarabu, maimamu na wazungumzaji wetu mahodari wa kiislam ktk "eneo letu hili la ulimwengu" hawakulizungumza...na kama walilizungumza basi si kwa uwazi na ukali kama wa hili la wapalestina...sababu? hapanshaka, halina maslahi(ya kiumaarufu na kifedha labda) kwao..si kipaumbele kitakachofanya wapigiane simu na maofisa balozi wa kiarabu kuzungumza na ndani ya mazungumzo hayo "kupata hulua"...lkn hizi nihofu tu, kutokana na mienendo ya masheikh, maimamu, na wazungumzaji wetu wa kiislam juu ya masuala ya umma kiulimwengu...akichinjwa koplo muislamu unguja, hakuna kulaani..wakiuawa wasomali ktk somalia..kimya...janjaweed wakiuwa waislamu weusi...ah!!...... inaleta hisia mbaya juu ya masheikh, maimamu na wasemaji wetu wa kiislam kwamba, namna masuala ya wapalestina yalivyokuwa mtaji wa kisiasa kwa watawala wa kiarabu, yamekuwa pia mtaji wa kutafutia umaarufu (na mambo fulani yenye heri kwa uchumi binafsi) kwa masheikh , maimamu na wasemaji wetu wa kiislamu, vinginevyo tujiulize kiini cha ukimya wao, sawia na ukimya wa watawala wa nchi za kiarabu kwenye matukio mengine ya waislam mbali na waarabu wa palestina...
 
Back
Top Bottom