Inaniuma sana kuona ndugu zangu wakikimbia ukimbizini kila kukicha

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Inaniuma saana kuona kila kukicha ndugu zangu wa sud kivu wao tu ndo wanakuwa wakimbizi, wao tu wanateseka. Watu wanaacha nyumba zao na kila kitu chao wanaenda kuwa wakimbizi nchi zingine.

Watu ambao walikuwa wanakula vizuri wanalala vizuri Watoto wao wana soma vizuri.

Leo wanalala sehemu ambazo ni mbaya saana. Halafu huku yule bwana kule Ikulu anadanganya kila kukicha nitakufa kwa ajili ya nchi hii kutafuta kiki tu.

Nashindwa kuelewa hivi FRDC wanalipwa kweli au Vipi. M23 wanazaaga mitaani

Hivi kama ni Rwanda ndo wanaleta vurugu hizi ndani ya nchi kweli DRC tumeshindwa kabisa kuji organise kuangalia jinsi gani ya kumtoa huyu Kagame madarakani?

Mbona 1992+ Kagame, Mseveni, na Laurent Kabila waliunganisha nguvu zao wakamuondoa Mobutu madarakani.

Sisi tumeshindwa nini kufanya hivyo
Kama shida ni western kwanini tusiombe msaada wa kijeshi Urusi kuangalia jinsi gani ya kuwafukuza ndani ya nchi yetu?

Ni lazima nifanye kitu kama situation itaendelea kuwa hivyo, sitakubali kuona ndugu zangu wakiwa wakimbizi kila kukicha na wakati nchi wanayo.
 
Siku madini yakiisha amani ya kudumu itapatikana au atokee rais mzalendo aongoze kwa mkono wa chuma amani itakuja.
 
Kuna pahala nilisoma kua hao jamaa wanachana sababu kubwa ikiwa wao ni nguvu kazi ibayotumika kwenye vita mbalimbali. Yaani kwa sababu ya hayo masaibu wengi wao huchukuliwa kwenda kupigana/kua waasi sehemu zenye maslahi na westerns na huko mbilinge linaendelea kama kawa.
Kwahiyo hutokaa uone hapo kuna amani.
 
Waafrika hawakosi visingizio kwa madhaifu yao kila siku ni kutafuta visingizio kuhalalisha umaskini wao.

Kaburu P.W. Bother aliwahi kusema, "wewe kama unataka kuharibu nchi yako ni rahisi sana, mpe mtu mweusi atawale uone hiyo nchi itakavyokuwa ya hovyo."

Sasa anayebisha kauli hiyo ya Bother asimame atueleze kama ni uongo. Kila siku tunaambiwa Tanzania ni nchi tajiri sana lakini zaidi ya nusu ya watu wake wanaishi chini ya dola moja kwa siku.. Sisi waafrika ni watu bure kabisa.
 
Back
Top Bottom