X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,610
- 1,810
...kuna baadhi ya mambo... Tanzania yananisumbua ...mke amepata dharula ya kujifungua ...anapokelewa na doctor...kumfungulisha mwanamke.... doctor ana ruksa za kuweza kuona naniihii za wake wa watu ...ma nurse wanakazi gani zaidi hospital ....ndio elimu yetu tulipofikia au ndio mpangilio ambao umepangwa???
Brother Yassin, kwanza ukuhainisha daktari wa jinsia gani unamzungumzia, japokuwa wachangiaji karibia wote wameona kuwa unamaanisha madaktari wa kiume kuhusika na uzalishaji (Ukunga).
Ninavyo fahamu mimi, madaktari watahusika na uzalishaji pale tu hali ya mjamzito itakapo onyesha hali ya utata na atahitaji huduma ya dharura kutoka kwa daktari bingwa, awe wa kike au wa kiume.
Kwa mfano, mtoto ameonekana amekaa vibaya, au njia ya mama ni ndogo na atahitaji kujifunguwa kwa njia ya upasuwaji na mambo mengine yanayo hitaji utaalamu zaidi.
Kama mama mjamzito ataonekana kuwa anaweza kujifunguwa bila msada wa daktari (Mke/Mume), basi madaktari watakuja kumuona tu pale atakapokuwa tayari ameshajifunguwa.
Hao madaktari wa kiume wanaopenda kufanya utundu na unyanyasaji wa kijinsia, wanakiuka maadili ya kazi zao na wanapaswa kunyang'anywa leseni zao za udaktari.
Thanx
xp