Inakuwaje Doctor kumfungulisha mwanamke?

...kuna baadhi ya mambo... Tanzania yananisumbua ...mke amepata dharula ya kujifungua ...anapokelewa na doctor...kumfungulisha mwanamke.... doctor ana ruksa za kuweza kuona naniihii za wake wa watu ...ma nurse wanakazi gani zaidi hospital ....ndio elimu yetu tulipofikia au ndio mpangilio ambao umepangwa???

Brother Yassin, kwanza ukuhainisha daktari wa jinsia gani unamzungumzia, japokuwa wachangiaji karibia wote wameona kuwa unamaanisha madaktari wa kiume kuhusika na uzalishaji (Ukunga).

Ninavyo fahamu mimi, madaktari watahusika na uzalishaji pale tu hali ya mjamzito itakapo onyesha hali ya utata na atahitaji huduma ya dharura kutoka kwa daktari bingwa, awe wa kike au wa kiume.

Kwa mfano, mtoto ameonekana amekaa vibaya, au njia ya mama ni ndogo na atahitaji kujifunguwa kwa njia ya upasuwaji na mambo mengine yanayo hitaji utaalamu zaidi.

Kama mama mjamzito ataonekana kuwa anaweza kujifunguwa bila msada wa daktari (Mke/Mume), basi madaktari watakuja kumuona tu pale atakapokuwa tayari ameshajifunguwa.

Hao madaktari wa kiume wanaopenda kufanya utundu na unyanyasaji wa kijinsia, wanakiuka maadili ya kazi zao na wanapaswa kunyang'anywa leseni zao za udaktari.

Thanx

xp
 
Kwanini tusichukue juhudi za msingi kabisa...kuhimiza wanawake walioko kwenye masomo ya udaktari wa binadamu...wasomee hasa hasa magojwa yanayo wahusu wao.Ila kupunguza....huu utata wa kifikra ambao mgojwa wa kike akienda kwa hospital wasiwe na wasi wasi na udaktari wa kiume katika miili yao.

Inahitaji kautafiti kujua kwanini madaktari wengi wanaume wanapenda kusomea Obs & Gyn wakati wa kike hawapendi!Labda kuna sababu.Hilo ni moja. Pili kuna wanawake huwa wanasema huduma za madaktari au manesi wanaume ni nzuri kuliko za wanawawake wenzao - kwa maana ya kuwa wanaume wanawaonea huruma zaidi na kuwahudumia bila ukatili wakati wa kujifungua.

Tusiangalie mabaya tu labda tuangalie mazuri yafanywayo na madaktari/manesi wanaume pia.
 
Asante kaka Yassin kwa kuongelea hili. kwa kweli mie huwa najisikia vibaya sana daktari mwanaume anaponipima, hata kama anapima vizuri tu kadri ya utaalamu wake na anafuata maadili ya kazi, ...ok naelewa na naamini kabisa hakuna agenda nyingine but as human being It is SO EMBARASSING. so sad ...I wish madaktari wote wa wanawake wangekuwa wakike
 
Last edited:
Ukiamua kusomea udaktari wa binadamu, maana yake ni kwamba ukisha hitimu, unakuwa tayari kutoa huduma yoyote ya utabibu kwa mgonjwa yeyote bila kujali jinsia. Hapa ninazungumzia matatizo yote yenye kuhitaji kwa namna moja au nyingine msaada wa daktari. Ukiondoa nchi za kiislamu kama Iran n.k. ambazo kisheria inalazimu wanawake kutibiwa na wanawake na wanaume pia kutibiwa na wanaume, kwa Tanzania na hata nchi za ulaya na nyingine, tiba kwa kufuata jinsia ya mgonjwa au jinsia ya daktari sio kigezo cha lazima.

Kwa mazingira ya Tanzania, kwa mfano huko vijijini na hata wilayani, akina mama hupewa huduma ya kujifungua na matabibu/wakunga wanaume. Katika suala la tiba haijalishi ni daktari wa jinsia gani anakuhudumia, ila linapokuja suala la kujifungua kwa akina mama, kuna tendency ya baadhi ya wakunga au ma-nesi wa kike kuwa cruel au kutokuwa na huruma kwa akina mama wenzao. Lakini hali ni tofauti kwa madaktari au wakunga na ma-nesi wa kiume.

Lakini pia, kwa tanzania specilization ya Gyn. & Obst. ina madaktari wengi wanaume kuliko wanawake.
 
Kwanini tusichukue juhudi za msingi kabisa...kuhimiza wanawake walioko kwenye masomo ya udaktari wa binadamu...wasomee hasa hasa magojwa yanayo wahusu wao.Ila kupunguza....huu utata wa kifikra ambao mgojwa wa kike akienda kwa hospital wasiwe na wasi wasi na udaktari wa kiume katika miili yao.

Kabisa yaani mkuu maana kwa mpango huu wake zetu wanapata sana tabu ila sema hatujui tu........Mke wako anaambiwa na daktari wa kiume vua nguo nikusaidia sasa hii kweli inakuwa bomba au ndio kutesana hata yule mwanamke anakuwa katika hali gani hivi????Mimi nilikuwa kama inawezekana na wenyewe wanawake wasome kwa jitihada kwa ajili pia ya wanawake wenzao waweze kuwasaidia zaidi........
 
Inahitaji kautafiti kujua kwanini madaktari wengi wanaume wanapenda kusomea Obs & Gyn wakati wa kike hawapendi!Labda kuna sababu.Hilo ni moja. Pili kuna wanawake huwa wanasema huduma za madaktari au manesi wanaume ni nzuri kuliko za wanawawake wenzao - kwa maana ya kuwa wanaume wanawaonea huruma zaidi na kuwahudumia bila ukatili wakati wa kujifungua.

Tusiangalie mabaya tu labda tuangalie mazuri yafanywayo na madaktari/manesi wanaume pia.

Asante sana mkuu kwa mawazo yako mazuri...lakini kwa nini wenzetu huku nje wanaweza sisi tushindwe kufanya hivyo kama wenzetu???Au upeo wa elimu na vichwa vyetu ni vigumu zaidi kuelewa mapema????Labda naona ndio tatizo hilo kama hivyo nakubali........
 
Asante kaka Yassin kwa kuongelea hili. kwa kweli mie huwa najisikia vibaya sana daktari mwanaume anaponipima kwa kushika maziwa au nanihii, hata kama anapima vizuri tu kadri ya utaalamu wake na anafuata maadili ya kazi, yaani kile tu kitendo cha yeye macho yake kuona na mikono yake kunishika nyeti zangu huwa kinanichafua roho kabisa...siku moja alikuwa anapima matiti akayabonyeza bonyeza wee halafu mwishoni akaminya chuchu ili aone kama kuna discharge...ok naelewa alikuwa anafanya kazi yake na na naamini kabisa hakuwa na agenda nyingine but as human being I was SO EMBARASSED. so sad ...I wish madaktari wote wa wanawake wangekuwa wakike

Yeah ndio hivyo sasa kwa nini wasiwe wanawake ambao wamesomea hivyo vitu???Sasa naona kwamba kwetu bado tupo nyuma kidogo lakini dada wewe vumilia tu hamna cha kufanya.....ila huku kwa wenzetu hamna hivyo vitu
 
Ukiamua kusomea udaktari wa binadamu, maana yake ni kwamba ukisha hitimu, unakuwa tayari kutoa huduma yoyote ya utabibu kwa mgonjwa yeyote bila kujali jinsia. Hapa ninazungumzia matatizo yote yenye kuhitaji kwa namna moja au nyingine msaada wa daktari. Ukiondoa nchi za kiislamu kama Iran n.k. ambazo kisheria inalazimu wanawake kutibiwa na wanawake na wanaume pia kutibiwa na wanaume, kwa Tanzania na hata nchi za ulaya na nyingine, tiba kwa kufuata jinsia ya mgonjwa au jinsia ya daktari sio kigezo cha lazima.

Kwa mazingira ya Tanzania, kwa mfano huko vijijini na hata wilayani, akina mama hupewa huduma ya kujifungua na matabibu/wakunga wanaume. Katika suala la tiba haijalishi ni daktari wa jinsia gani anakuhudumia, ila linapokuja suala la kujifungua kwa akina mama, kuna tendency ya baadhi ya wakunga au ma-nesi wa kike kuwa cruel au kutokuwa na huruma kwa akina mama wenzao. Lakini hali ni tofauti kwa madaktari au wakunga na ma-nesi wa kiume.

Lakini pia, kwa tanzania specilization ya Gyn. & Obst. ina madaktari wengi wanaume kuliko wanawake.

Ni kwa nini sasa inakuwa hivyo yaani wanawake upeo wao wa elimu mdogo au inakuwaje hapo????Maana inabidi tujiendeleze zaidi tusisubirie mtu fulani anasoma udoctor atakuja kutusaidia naona kama haijatulia kabisa.....inabidi na wanawake na wenyewe wajiendeleze zaidi na zaidi kiundani zaidi na kuelewa nini wanakifanya.......
 
Habari za sasa hizi.

Kitu muhimu ni maadili mfanyakazi akifuata maadili kazi inakwenda vyema sana na sio kwa madaktari tu hata kwa walimu na kazi nyengine kwani si tunashuhudia kwa walimu ambao wanakwenda kinyume na maadili ya kazi wanawachapa mimba wanafunzi? lakini ukenda kwenye maadili ni kosa hilo kufanyika kwa hivyo hata nafasi za kazi nyengine kalikadhalika.

mgonjwa au mama mja mzito akenda kujifungua maumivu anayesikia pale hajali wala hana muda wa kujua anayemzalisha ni nani na daktari kwa hakika huwa haangalii sana mambo kama walivyosema wenzangu kuwa anamtomasa tomasa ninavyojua anakuwa makini sana na kazi ya kuzalisha ila mtu akiwa na tabia mbovu anaweza kutumia nafsi hiyo kwa kufanya uovu kwake.

lakini daktari makini hata kama amempenda huyo mama au dada basi humaliza shughuli ya huyo mgonjwa yaani kumhudumia then masuala ya mahusiano hufuata baadae kwa kumuomba contact zake ili kuwasiliana zaidi after kujifungua.

lakini pamoja na yote ni vyema kuzalishwa na daktari mwanamke mwenzako isipokuwa panapotokea tharura mwanamme anaruhusiwa kuingia kama wanavyofanya utaratibu huo madaktari wa hapa zanzibar kwenye kuzalisha wanaume hawaingii unless dharura kubwa amabyo imewashinda wanawake ndio huingia wanaume ambao ni wataalamu zaidi kuliko waliokuwepo zamu hospitalini hapo.

maumibu anayopata mwanamke ni makubwa hivyo kama binaadamu mara nyingi hata madaktari nao huingia huruma anapomuona mwanamke anapojifungua
 
Teh teh teh!!!! Yasini, mi nadhani mama mjamzito anapokwenda kujifungua sidhani kama huyo Dr wa kiume atakuwa na mvuto na hiyo naniiii ya huyo mama hata kama alikuwa na hamu ya hiyo kitu sidhani kama atadiriki kufanya lolote..Mimi binafsi mke wangu amejifungua watoto wawili na wote amesaidiwa na dr wa kiume.Kwanza hata mama mwenyewe ukimuuliza kama kusaidiwa na Dr. wa kiume inamkwaza anakwambia kwa jinsi anavyopata machungu akili ya nani anaangalia dudu yake wala sio issue..So mkubwa jambo kubwa ni kuomba mungu mama ajifungue salama na kiumbe kiwe salama mengine ni mapito tu kwanza hata siku wakikutana njiani hawezi kukumbuka kama huyo mama alimsaidia kujifungua maana anahudumia wengi.
 
yote tisa .. nakuhakishieni bora doctor mwanaume akuzalishe kuliko mwanamke .. kwani wanawake wengi ambao ndo wanategemewa kuwa na huruma kipindi hichi wanaendeleza ukatili .. ataanza kukuzodoa na kukusimanga .. mbona hivi mbona unapiga kelele kwani unaumwa pekeyako .. sincerely hawakupi encouragement hata kidogo... am lucky am always attended by a male doctor that is in cases za kujifungua ... am taken good care of sincerely and i have never regretted it .. i would recommend that to every woman.

sasa wewe kama unawasiwasi na gudgets za mkeo unabidi ujifunze ukunga .. kwani hawa already madaktari wanaona mengi .. unless mwanamke ajishaue

ila sijui kwa ma gyn maana sijawahi kuonana nao
 
Najua mdr ni wachache ila inakuwa imetulia kama mwanammke akimzalisha mwenzie.Ila nasikia nao akina mama hawependani as a result nao wanapenda wanaume wawazalishe.
Ila inataka moyo sana Dr akute kitu mwake mwake alafu akiache,mbaya zaidi akiwa Muathilika si anaweza kuua bendi.
Namwachia mungu tuu,tena juzi tuu mamaa alienda kwa uchunguzi nilimdadisi sana juu ya ilo ila akananiakikishia kuwa hakuchomwa sindano ya usingizi na kila kitu kilikuwa live though nilipenda niwepo eneo la tukio ila nilikuwa safari.
 
Asante sana mkuu kwa mawazo yako mazuri...lakini kwa nini wenzetu huku nje wanaweza sisi tushindwe kufanya hivyo kama wenzetu???Au upeo wa elimu na vichwa vyetu ni vigumu zaidi kuelewa mapema????Labda naona ndio tatizo hilo kama hivyo nakubali........

Mkuu,
Sidhani ni suala la kuweza.Labda kama sijakuelewa unazungumzia uwezo gani.Kama ni uwezo wa kiutendaji,uwezo mbona upo sana tu.Tanzania inaweza kuwa na upungufu wa madakatari kwa ujumla lakini haina upungufu wa uwezo wa madaktari.Inawezekana pia uko ukosefu wa zana na vitendea kazi.Ndiyo maana nikasema tunahitaji kuelewa kwanini katika specialisation madaktari wanaume wanapenda kuzamia kwenye obs & gyn wakati labda tungetegemea madaktari wakike wapende kuzamia zaidi huko wawasaidie wanawake wenzao.Binafisi ninajua madaktari wengi wanaume obs & gyn kuliko wakike.Inaelekea wanawake hawaipendi hiyo fani. Kihsitoria ya kazi za wanawake, wengi walikuwa wanasomea ukunga ( nursing) na sidhani tunaupungufu wa idadi ya wanawake wakunga ukilinganisha na wanaume.Isitoshe hata wakunga wa jadi wanawake wapo kuhudumia pale pasipo na manesi au madaktari waliosomea fani.Ila ukweli unabaki kuwa kama ilivyo kwenye fani nyingine abuse of "power & authority" inatokea na tumeona/kusikia madaktari wakichukuliwa hatua kwa kukiuka maadili ya kazi.
Labda tuwaulize madaktari wanawake kwanini hawapendi kuspecialise kwenye obs& gyn ili hatua za makusudi zichukuliwe kuwamotisha labda itasaidia.
Ila mwisho wa siku huwezi kulazimisha mtu kusomea asichopenda na pia inapokuwa hakuna uchaguzi we have to go by what we have.
 
yote tisa .. nakuhakishieni bora doctor mwanaume akuzalishe kuliko mwanamke .. kwani wanawake wengi ambao ndo wanategemewa kuwa na huruma kipindi hichi wanaendeleza ukatili .. ataanza kukuzodoa na kukusimanga .. mbona hivi mbona unapiga kelele kwani unaumwa pekeyako .. sincerely hawakupi encouragement hata kidogo... am lucky am always attended by a male doctor that is in cases za kujifungua ... am taken good care of sincerely and i have never regretted it .. i would recommend that to every woman.

sasa wewe kama unawasiwasi na gudgets za mkeo unabidi ujifunze ukunga .. kwani hawa already madaktari wanaona mengi .. unless mwanamke ajishaue

ila sijui kwa ma gyn maana sijawahi kuonana nao

Dada Naima wala hukosei wanawake wengi wanakuwa na Gubu na wanawake wenzao.... angalia hata manesi wengi wao unakuta wanamajibu makali sana kwa wanawake wenzao.... cjui kwanini wanakuwa hivi.. Kuna cku nilikwenda hospital fulani nikakutana na dr. wa kike hayo majibu yake tu nilijikuta napona mwenyewe, utafikiri wamelazimishwa kufanya hizo kazi..... mi kusema kweli kila ninapokwenda kutibiwa huwa naomba nimkute dr. wakiume.
 
yote tisa .. nakuhakishieni bora doctor mwanaume akuzalishe kuliko mwanamke .. kwani wanawake wengi ambao ndo wanategemewa kuwa na huruma kipindi hichi wanaendeleza ukatili .. ataanza kukuzodoa na kukusimanga .. mbona hivi mbona unapiga kelele kwani unaumwa pekeyako .. sincerely hawakupi encouragement hata kidogo... am lucky am always attended by a male doctor that is in cases za kujifungua ... am taken good care of sincerely and i have never regretted it .. i would recommend that to every woman.

sasa wewe kama unawasiwasi na gudgets za mkeo unabidi ujifunze ukunga .. kwani hawa already madaktari wanaona mengi .. unless mwanamke ajishaue ila sijui kwa ma gyn maana sijawahi kuonana nao

Sina wasiwasi na mke wangu na sijatoa hii mada kwa ajili ya mke wangu bali ni kwa jamii yote sisi sote inayotuzunguka tunakokwenda na ambao wameshapata kufanikiwa na pia hii ni kama mtizamo ambao upo kwenye jamii yetu.......Sasa ni kujadili hili swala linakuwaje ila ukisema kwamba nina wasiwasi wa mke wangu hujajua bado nipo vipi......Kwa hiyo cha muhimu mada ndio izungumziwe zaidi sio kumtolea mtu mfano..

Lakini pia mawazo yako ni mazuri kwa ujumla inabidi na sisi tujiendeleze kwa upande fulani kielemu.......
 
Last edited:
Najua mdr ni wachache ila inakuwa imetulia kama mwanammke akimzalisha mwenzie.Ila nasikia nao akina mama hawependani as a result nao wanapenda wanaume wawazalishe.
Ila inataka moyo sana Dr akute kitu mwake mwake alafu akiache,mbaya zaidi akiwa Muathilika si anaweza kuua bendi.
Namwachia mungu tuu,tena juzi tuu mamaa alienda kwa uchunguzi nilimdadisi sana juu ya ilo ila akananiakikishia kuwa hakuchomwa sindano ya usingizi na kila kitu kilikuwa live though nilipenda niwepo eneo la tukio ila nilikuwa safari.

Pamoja kaka maana inabidi kwa upande fulani tuangalie wapi tunakwenda na wapi tunatoka nadhani ndio inakuwa vizuri zaidi........Pia hiyo kuhusu kutopenda ni kweli kabisa hawapendi lakini kila mtu anakupenda ila inabidi tuwe na muongozo fulani katika jamii na maadili mazuri.
 
Hivi kisaikolojia huwa inakuwaje kwa "madaktari wa wanawake" kwa wake zao. Maana wanaona nyeti nyingi sana za wanawake wa kila aina hii haiwafanyi kupungukiwa na muhemko kwa wake zao, kwa kuona kuwa ni kitu cha kawaida?.
 
yote tisa .. nakuhakishieni bora doctor mwanaume akuzalishe kuliko mwanamke .. kwani wanawake wengi ambao ndo wanategemewa kuwa na huruma kipindi hichi wanaendeleza ukatili .. ataanza kukuzodoa na kukusimanga .. mbona hivi mbona unapiga kelele kwani unaumwa pekeyako

Hii nakubaliana na wewe nimeshasikia wanawake wengi sana wanawalalamikia wakunga wa kike. ukiwa unapiga kelele sana kwa uchungu wanafikia hata kukwambia kuwa ashakum " Mbona wakati wa tendo ulikuwa unafurahia na kuachia miguu, panua miguu utaua mtoto wewe ulizania Chai"
 
Hivi kisaikolojia huwa inakuwaje kwa "madaktari wa wanawake" kwa wake zao. Maana wanaona nyeti nyingi sana za wanawake wa kila aina hii haiwafanyi kupungukiwa na muhemko kwa wake zao, kwa kuona kuwa ni kitu cha kawaida?.

Mkuu hapo nashindwa kuelewa kwa kweli ila mimi nilikuwa naonabora zaidi kama wanawake wazalishwe na wanawake wenzio maana madoctor wanaona vitu vingi sana pia rahisi zaidi kuhudumiana wenyewe kwa wenyewe maana kama kuna vitu vingi amavyo doctor hapaswi kufanya basi anafanya......
 
Hii nakubaliana na wewe nimeshasikia wanawake wengi sana wanawalalamikia wakunga wa kike. ukiwa unapiga kelele sana kwa uchungu wanafikia hata kukwambia kuwa ashakum " Mbona wakati wa tendo ulikuwa unafurahia na kuachia miguu, panua miguu utaua mtoto wewe ulizania Chai"

Mhhhh mkuu hiyo siku sasa itategemea utamkuta nani hiyo sehemu na huyo dada utamkuta vipi lakini naona kuna baadhi yao wanahafadhari kidogo na hicho kitu......na pia sio katika 100% ni 10% ndio watakuwa wanafanya hivyo kwa hiyo ni kidogo afadhali
 
Back
Top Bottom