imekaaje kauli ya serikali waliofunga ndoa na wahamiaji haramu wavunje ndoa zao

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,054
6,281
mnazungumziaji kauli ya serikali kupitia kwa mkuu wa mkoa wa geita kuwa waliofunga ndoa na wahamiaji haramu wavunje hizo ndoa.
kwa uzoefu wangu nimeona wa Tanzania wengi ulaya na america wanafunga ndoa na kupata vibali vya kukaa. je kwa familia zenye watoto vip? je sheria zinasemaje?
ningependa mtoe maoni yenu bila matusi. tujadili kauli ya serikali kama ni sawa au siyo sawa.
 
Hii mbona ni kawaida kabisa ukienda nchi yoyote! Kama ukifunga ndoa na mhamiaji 'haramu' na usimhalarishe mpaka ukamatwe lazima atakuwa 'deported' na fine juu!
Hatua hii ya serikali naiunga mkono!
 
Hio kauli ni sawa kabisa Kila nchi lazima iwe na Sheria na zifatwe!! Bongo tunaishi kienyeji Sana
 
Hiyo kauli si sawa kuwaambia kuwa wavunje ndoa zao. Jambo serikali ilichotakiwa kufanya ni kuwarudisha kwao kwa maelezo kuwa wakitaka kurudi wafuate utaratibu uliowekwa. Uwezekano mwingine ni kuwaambia wale Watanzania wenye ndoa wawafuate wenzi wao huko nchini walikotoka.
 
Hiyo kauli sio sahihi%100
Kwani ni kutaka kutenganisha familia za watu
 
Kufunga ndoa na muhamiaji haramu ni kosa kama lilivyo kosa la kumuhifadhi muhamiaji haramu, kwahiyo ikiwezekana pia wawachukulie hatua wote waliofunga ndoa na wahamiaji haramu
 
toa kifungu cha sheria kinachosema hivo
 
mnazungumziaji kauli ya serikali kupitia kwa mkuu wa mkoa wa geita kuwa waliofunga ndoa na wahamiaji haramu wavunje hizo ndoa.
kwa uzoefu wangu nimeona wa Tanzania wengi ulaya na america wanafunga ndoa na kupata vibali vya kukaa. je kwa familia zenye watoto vip? je sheria zinasemaje?
ningependa mtoe maoni yenu bila matusi. tujadili kauli ya serikali kama ni sawa au siyo sawa.

naunga mkono amri ya serikali, watusi hawana nia njema hata kidogo na wananchi wengine wa afrika mashariki wanajiona wao wapo juu ya wengine ! issue hapa siyo ndoa tu bali ni uhalali wao wa kuishi ndani ya hii jamhuri, hapa siyo shamba la bibi kama wanahitaji kuishi Tanzania wafuate sheria. sio wapenyezwe na dikteta kagame kwa nia ya kuangamiza utaifa wetu hili halikubaliki watanzania tunatakiwa tuwe macho.
 
Kufunga ndoa na muhamiaji haramu ni kosa kama lilivyo kosa la kumuhifadhi muhamiaji haramu, kwahiyo ikiwezekana pia wawachukulie hatua wote waliofunga ndoa na wahamiaji haramu

Ni kweli kabisa kuwa ni kosa lakini ni wananchi wangapi wanaojua kuwa ni kosa? Hiyo serikali imefanya jitihada gani kuwaelimisha watu juu ya hili? Hususani wale ambao wanaishi maeneo ambayo serikali yenyewe iliamua kuwa ni mazuri kwa kuwahifadhi hao wakimbizi?? Mimi sidhani kama unawezamhukumu mtu kwa kosa ambalo hukuwahi kumueleza kuwa ni kosa. Sasa wanavunja ndoa afu familia zao zinakuwaje? Watoto waliowapata kutokana na ndoa hizo wafanyeje? Kwa nini serikali isitoe muda wa hao wenzi 'wageni' kuandikishwa au kufuata taratibu zinazotakiwa badala ya kuumiza familia zilizoundwa? na kwa nini kauli hii itolewe baada ya viongozi wa nchi hici mbili kutofautiana?
 
wewe umeeleza vizuri. nataman watu waelewe ulichoandika
 
Aksante ila na wewe Mtoa mada inabidi uwe neutral, usibase upande mmoja unaoutaka wewe. Sikiliza pande zote kasha reason.

asante kwa ushauri. unajua nishaona wa Tanzania wahamiaj haramu marekan wanavyooa raia wa uku na wanaishi vizuri.
marekan ina wahamiaj haramu zaidi ya million 1.

nimechambua hoja zote wengine wanasema wafukuzwe tu ila awajasema sababu za msingi. ila wewe umeelezea sababu za msingi pia.
 
Rais akiwa na akilikama za bata haya ndo madhara yake..huwezi utatoa kauli utumbo kama hizo...yaani niachane na mke wangu kisa mambo yenu na kagame!!!leta mtoto wako basi niwe nampiga kagera technology
 
Back
Top Bottom