Imeandikwa ishi nao kwa akili, sikusikia yamenikuta

Status
Not open for further replies.

Helixir

JF-Expert Member
Mar 17, 2022
462
1,203
Toka hapo awali nilikuwa nina ndoto na hamasa ya kufikia mafanikio kwa kutatua matatizo ya Jamii inayonizunguka. Nilianza kupenda habari za anga za juu na Sayari KWA ujumla , nilijisomea kila kitu kuhusu anga kilichokuja mbele yangu .

Katika harakati za kutafuta mwekezaji nikaangukia KWA huyu dada/mama SINGO MAMA, ambayo aliamua kutumia vulnerabilities zangu kunihadaa na kunipamba panna hatimaye nikaingia kingi.

Inaanza baadae ya kuacha KAZI kampuni x nikahamia mkoa Y kuangalia fursa zingine za kijasiriamali. MNilikuwa na plans nyingi za kuanzisha startup company Zenye/yenye tija na faida kwangu na Jamii KWA ujumla, Mara nyingi nilipenda kushare Mawazo yangu na watu/Jamii lengo ni kutafuta mbia, mwekezaji .

Upendo wangu KWA watoto ukaniponza , picha linaanza Nilipofikia kuna movie library so Mara nyingi jioni huwa ninafika kubadilishana movies na kijana wa hapo, basi huwa anafika bidada mmoja na mwanae umei wa miaka miwili hivi, udadisi wa huyu mtoto ambaye sasa hivi ni mwanangu KWA lazima ulinivutia na kuanza kuzungumza naye.

Baadae ya kupita dakika kumi hivi mama yake alimaliza kuhudumiwa wakiwa wanaondoka nilimwita dada samahani Naomba tuzungumze nilimsifia mwanae kisha nikamwambia kama hajaanza shule mpeleke udadisi alio nao autumie kwenye mambo ya msingi.

Akacheka pale Mtoto akanambia kwaheri ankoli. Ikawa ni ankoli ankoli, mara nimnunulie vitabu vya namba na Wanyama huku nikisisistiza mama yake amkazanie kujifunza.

Siku zikasonga hatimaye nikaalikwa KWA bimkubwa huyu , kweli nilifika na niliulizwa unajishughulisha na nini nikatoa maelezo pia nikazungumza ndoto yangu Kubwa niliyo nayo. Na kushare feasible ideas zangu ,plans na models za kibiashara Nilizozifanyia utafiti wa kina, alifurahi na kuniambia You are a genius ,hakuna kijana wa umri wako anayewaza mambo kama hayo ,pale aliniuliza kuhusu Maisha yangu ya utotoni na mambo kibao ..mwisho akatoa jibu nitakusaidia .

Nitakutimizia lengo lako na wewe inabidi utimize la kwangu kwa furaha niliyokuwa nayo sikutaka kuuliza lengo lake ni nini. Nikamwambia niandae legal structures basi na yeye Tufungue kampuni na stuffs kama hizo akagoma akasema haina shida Huku akinishika shavuni.

Siku zinasonga nkatengenezewa kipindi nikajikuta tunafanya ngono Mara ya kwanza ya pili ya tatu hii hapa , akadai ameshika mimba , mshahara wa dhambi mauti , huruma yangu inaniponza nikamwambia usitoe si unajua risks zake , vipindi vikaanza kutengeneza mara oh silali kuna watu wananiloga usiku, KWA sababu ya ujauzito wako huu , mara alete vitimbi kazini kwao marafiki zake wanipigie simu waseme mimi nikiwepo anapata ahueni, Ilibidi niwe nashinda nae mara KWA mara , nkiacha KAZI zangu Ili kumliwaza . Kumbe ni Kipindi kilitengenezwa huruma zangu zikaniponza.

Kufanya ndefu fupi kupitia ujauzito huo nililipishwa kishika uchumba na fines KWA lazima .

Last year mungu kanibariki Mtoto wa kiume ambaye siku hiyo nilimwaga machozi ambayo walijua ni furaha pekee kumbe ni huzuni mixer furaha kidogo ,majuto na mengine mengi .

Im chained ila soon nakwenda kuwa huru.

Hivi sasa mimi ni Balozi wa kuzuia vijana wasioe wala kuwa na mahusiano na masingo mamas wengi wapo tayari kutumia mbinu yeyote ile wakunase uwe baba wa mwanae KWA kupenda au KWA kutokupenda.

Muwe na siku njema.
 
Hujaeleza matatizo hasa unayokumbana nayo rudi ueleze matatizo yanayokufanya uchanganyikiwe
Bro huruma yangu iliniponza baadae ya kupata ujauzito ambao ni matokeo ya ngono zembe ,alianza vitimbi mara ajiumize mara ajibamize ukutani .. all in all ni kuamsha huruma zangu .

Na kweli aliziamsha nkajikuta mda wote nawaza namna ya kumsaidia. Nlikuwa na Biashara ikabidi niiuze na hela nipange nyumba nzima Ili niwe karibu nae as long as ako na ujauzito wangu. Presha za mimba za kutengeneza , vikao vya uongo alivyounda yeye mama yake na marafiki zake Ili mimi niende kwao kujitambulisha. Alipokaribia kujifungua alitaka kujiua ety mimi simjali na kama namjali niende kwao la sivyo atajiua na vitisho vingi.

Aliumba taarifa nyingi za uongo za kitabibu , na yote haya nimekuja kungundua juzi baadae ya kusikia akizungumza na Rafiki yake kwamba sasa hivi nimeshtuka na nimegundua mchezo wao.
 
Toka hapo awali nilikuwa nina ndoto na hamasa ya kufikia mafanikio kwa kutatua matatizo ya Jamii inayonizunguka,

Nilianza kupenda habari za anga za juu na Sayari KWA ujumla , nilijisomea kila kitu kuhusu anga kilichokuja mbele yangu...
Hao ni wakula mbususu tuu. Usijidanganye kuwa mwanaume maenzio alikuwa mjinga kumkimbia
 
Toka hapo awali nilikuwa nina ndoto na hamasa ya kufikia mafanikio kwa kutatua matatizo ya Jamii inayonizunguka,

Nilianza kupenda habari za anga za juu na Sayari KWA ujumla , nilijisomea kila kitu kuhusu anga kilichokuja mbele yangu .

Katika harakati za kutafuta mwekezaji nikaangukia KWA huyu dada/mama SINGO MAMA, ambayo aliamua kutumia vulnerabilities zangu
Story yako ina hang mahali,au labda mimi kwa uzee wangu ndio siielewi...
 
Bro huruma yangu iliniponza baadae ya kupata ujauzito ambao ni matokeo ya ngono zembe ,alianza vitimbi mara ajiumize mara ajibamize ukutani .. all in all ni kuamsha huruma zangu .

Na kweli aliziamsha nkajikuta mda wote nawaza namna ya kumsaidia. Nlikuwa na Biashara ikabidi niiuze na hela nipange nyumba nzima Ili niwe karibu nae as long as ako na ujauzito wangu. Presha za mimba za kutengeneza , vikao vya uongo alivyounda yeye mama yake na marafiki zake Ili mimi niende kwao kujitambulisha. Alipokaribia kujifungua alitaka kujiua ety mimi simjali na kama namjali niende kwao la sivyo atajiua na vitisho vingi.

Aliumba taarifa nyingi za uongo za kitabibu , na yote haya nimekuja kungundua juzi baadae ya kusikia akizungumza na Rafiki yake kwamba sasa hivi nimeshtuka na nimegundua mchezo wao.
Duh hatari, sasa kama yeye mwenyewe hajiwezi ilikuaje ukahisi ataweza kukusaidia kutimiza ndoto zako.
 
Duh hatari, sasa kama yeye mwenyewe hajiwezi ilikuaje ukahisi ataweza kukusaidia kutimiza ndoto zake.
Ndoto zake zilikuwa kupata mume brother.

Baadae ya kushtuka nikafanya uchunguzi nikagundua kuwa amelazimisha Sana ndoa .

Lastly Akaangukia kwangu
 
Ndoto zake zilikuwa kupata mume brother.

Baadae ya kushtuka nikafanya uchunguzi nikagundua kuwa amelazimisha Sana ndoa .

Lastly Akaangukia kwangu
Yani swali langu nilidhani uliposema alisema atakusaidia utimize ndoto zako basi atakuwa anajiweza kifedha, ila sasa it seems naye kawaida kama hadi ilibidi wewe ndo ikapange nyumba nzima basi hana uwezo huo.
Sasa ilikuaje ukaamini atakusaidia timiza ndoto zako au msaada wa kimawazo?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom