Ilipokosea SERIKALI mpaka kupelekea hali hii.

dadeez

Senior Member
Nov 30, 2010
112
139
Wakuu kwa mtazamo wangu na kwa Elimu yangu ya kawaida ninaona dhahiri kabisa SERIKALI ilikosea kwenda na 'beat' ya wimbo wa TEKINOLOJIA haikwepeki katika dunia ya sasa inayokua kwa kasi ya ajabu ya UTANDAWAZI.
Nina yasema haya nikiwa nimelenga kwenye hali ya matamko na mikakati inayoibuka kila kukicha kwenye wizara mbali mbali hasa upande wa ukusanyaji wa KODI kwa wafanya biashara na wakulima.
Hivi karibuni kulitolewa tamko la wafanya biashara ndogogo wawe na vitambulisho (Lengo hapa likiwa ni upatikanaji wa kodi), mafundi simu, TV na wote wa vifaa vya mawasiliano watambuliwe RASMI, imekuja na wakulima pia wapatiwe vitambulisho.
Kwa jumla hayo yote yanafanyika ni kupata Idadi sahihi ya watu unaowalenga ili kukurahisishia kuwaMANAGE kwa hali yoyote ukihitaji (DATABASE).

Sasa SERIKALI ilipokosea ni pale tu Ilipoidharau TEKINOLOJIA hususani IT kwenye kutengeneza DATABASE ya Taifa zima yenye kubeba karibu kila kitu, Unaweza kujiuliza si DATABASE ipo kule NIDA kwenye vitambulisho vya Taifa? kwa mtazamo wangu sidhani kama DATABASE ya NIDA imejitosheleza kiasi kwamba sasa hivi yanatoka matamko mengi ya watu waandikishwe vitambulisho sijui vya biashara mara vitambulisho vya wakulima, Basi kama DATABASE ipo sawa na imejitosheleza basi hakuna wataalamu wakueleweka kwa sababu ingetumka kwa usahihi kwenye haya matamko bila kutoa matangazo na kushtua watu.

Ushauri wangu SERIKALI iandae IT CENTRE rasmi kabisa wawepo wataalam wakueleweka watengeneze STRONG DATABASE na systems mbali mbali za kuMONITOR haya wanayokosea sasa hivi na kuhangaika, wapo vijana wengi sana wenye utaalamu wa hali ya juu, watafutwe wawekwe sehemu moja wabuni hivi vitu kwa faida ya TAIFA letu.

Mtazamo wangu BINAFSI.
 
Back
Top Bottom