Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Kuna jambo limekuwa linanitatiza kila siku. Ilikuwaje Chadema iliweza kuipiku CUF katika kukubalika huku Bara? Sote twajua baada ya NCCR kupotea CUF ndiyo ilikuwa moto wa kuotea mbali katika kuihenyesha CCM na hiii ilionekana katika uchaguzi wa 2000 na 2005 hasa katika kura ya urais.
Baada ya 2005 CUF ilianza kupotea pole pole. Bila shaka ni kwa sababu CDM waliweza kuipiku CUF katika hoja ya ufisadi na hii inashangaza -- kwani CUF hawakuiona hoja hiyo na kuifanya yao? Kitu gani kiliwazuia?
Umaarufu wa Chadema ulianzia September 2007 kule Mwembeyanga wakati Dr Slaa aliposimama jukwaani na kuitaja ile orodha ya aibu ya watu 11 ikiongozwa na JK mwenyewe. Hilo lilikuwa ni bonge la bao la kisigino dhidi ya CUF, na tangu hapo chama hicho hakikusimama tena sawasawa kilianza kuchechemea.
Na uzuri ni kwamba orodha ile ilikuwa ya ukweli mtupu, na ndiyo yakaja mambo ya EPA, Meremeta, Deep Green na mengineyo mengi isipokuwa Richmond ambalo lilianzia katikati 2006.
Ingekuwa ni Profesa Lipumba ndiyo alipanda jukwaani na kutaja orodha kama hiyo, hadi leo hii Chadema ingebakia kama zamani, chama cha Wachagga.
Hii inaonyesha Dr Slaa ana uthubutu na ujasiri wa kuweza kufanya maamuzi magumu na mazito, sifa ambayo Profesa Lipumba hana, ingawa yeye anaweza kuwa anamzidi DR Slaa katika kuyaelewa matatizo ya nchi hii na kuyaelezea kwa ufasaha, lakini si katika ujasiri wa kuchukuwa maamuzi mazito.