Ili uweze kupanda Mlima Kilimanjaro andaa Bajeti ya Shilingi 1,700,000

Jadda unaona mambo haya?
Yeah binafsi huwa naona inategemea na kampuni inayokupeleka, route unayotaka na huduma unazotaka, tena hizo bei ni kwa wazawa wageni huwa wanapigwa parefu

Hiyo nimeona ni route ya Lemosho tu sijajua routes nyingine wanacharge Kiasi gani, maana kuna nyingine ni ndefu na nyingine ni ngumu mfano Umbwe, ila rahisi na pendwa kuliko zote ni Marangu nafikiri

Mimi ni mbahili ila honestly hizo gharama naona ziko fair kulingana na huduma zinazotolewa, kuna vivutio ukienda gharama ni za ajabu utashangaa na roho yako, halafu ukicheki huduma zinazotolewa hata haziendani unaweza ukalaani
 
Yeah binafsi huwa naona inategemea na kampuni inayokupeleka, route unayotaka na huduma unazotaka, tena hizo bei ni kwa wazawa wageni huwa wanapigwa parefu

Hiyo nimeona ni route ya Lemosho tu sijajua routes nyingine wanacharge Kiasi gani, maana kuna nyingine ni ndefu na nyingine ni ngumu mfano Umbwe, ila rahisi na pendwa kuliko zote ni Marangu nafikiri

Mimi ni mbahili ila honestly hizo gharama naona ziko fair kulingana na huduma zinazotolewa, kuna vivutio ukienda gharama ni za ajabu utashangaa na roho yako, halafu ukicheki huduma zinazotolewa hata haziendani unaweza ukalaani
Nendeni tu kwakweli, hiyo hela inatakiwa nikiitoa nisiteseke🤣
 
Gharama ni ndogo sana hiyo kwa mtu anayeitwa mtalii, vilevile gharama ni kubwa kwa mtu asiyekuwa mtalii

Kuna mambo mengine sio lazima watu wote wayafanye, hata magari pia kuna PASSO, na Lexus.

Nafikirià siku za usoni kutembelea mbuga za wanyama tarangire na ngorongoro, maana mlima nmeupanda tayari
 
Gharama hizo ni kubwa sana kwa mtanzania wa kawaida. Kipato cha Watanzania wengi ni kidogo. Hivyo kama serikali inawathamini na kuwapenda raia wake, iweke viwango nafuu kwa kupunguza gharama. Mfano: 1. Badala ya kulala hotel ya kitalii, watu walale kwenye mahema (tents) 2. Sio lazima watu walishwe vyakula vya gharama kama vile burger, pizza n. k 3. Itumike njia fupi badala ya ndefu 4. Wizara Husika iandae safati hiyo kama ofa ya kusherehekea jamuhuri. Kipindi cha maonesho ya sabasaba wizara hupeleka watu kwenye mbuga za wanyama. Nifanye hivyo hata kupanda mlima Kilimanjaro. Naamini kwa laki 5 watanzania wengi wataenda kwa makundi makubwa na selikali itaingiza mapato mengi tofauti na sasa. Serikali iwapende kwa kuwapa kipaumbele wananchi badala ya kuwadharau na kuwaheshimu wageni toka nje ya nchi
 
Hiyo ni bei rafiki sana Hebu Angalia siku unazotumia unakaa wapi unatumia nini ni juu yao wewe mpaka ufike juu na urudi.
Watu wanajipanga ndipo watumie angalia ilivyo rahisi unalala hoteli uhakika unapelekwa mpaka getini na usafiri wa uhakika unapewa watu wa kukusaidia yote hiyo ni pesa mkuu unapanda mpaka juu muda mwingine unasaidiwa kushikwa hayo yote kwa 1+m ni kitupoa sana.
 
Mbona cheap sana
Ukitaka kujua ni expensive, assume mnaenda kundi la 5 people, total cost inakuwa 8.5 million kwa ajili ya kupanda mlima, sijawahi kupanda ila logic tells me hakuna hotel ya kifahari wala chochote extraordinary katika service mtakazopewa. Unless mtaalamu aje kutupa breakdown ya 8.5m kama cost ya kupanda mlima watu wa5 then tucompare other tourist attractions
 
Ukitaka kujua ni expensive, assume mnaenda kundi la 5 people, total cost inakuwa 8.5 million kwa ajili ya kupanda mlima, sijawahi kupanda ila logic tells me hakuna hotel ya kifahari wala chochote extraordinary katika service mtakazopewa. Unless mtaalamu aje kutupa breakdown ya 8.5m kama cost ya kupanda mlima watu wa5 then tucompare other tourist attractions
Mkiwa watu 5 mtahitaji
√ tour guide 2
√mpishi 1
√waiter 1
√camping master
√ wapagazi/porters wasiopungua 10 ambao kazi zao pamoja na mpishi, waiter camping ni
  • kubeba mabegi yenu ambayo ndani yake mtakuwa mmeweka sleeping bag, nguo za joto, makoti, ya mvua, soksi za joto n.k
  • watabeba gesi ya kupikia
  • watabeba vyakula
  • watabeba mahema ya kulalia, jiko, na mess
  • watabeba viti vya kukalia
  • watabeba mtungi wa huduma ya kwanza pamoja na vifaa vingine vya tiba.

- pesa unayotoa itahitajika kumlipa mpagazi angalau 15-20k kwa siku na wastani wa njia ya Lemosho ni siku 7 hivyo mtu 1 ni 140k mshahara plus Tip ambayo ni minimum 5-10 per day apo ni wastani wa 35 kwa siku 7.

  • garama ya kununua vyakula vya siku 7
  • garama za usafiri kutoka moshi mpaka lemosho gate sijui ni km ngapi apo watu 5 plus wahudumu wenu mtahitaji land cruser 2 kuwafikisha
  • garama za park kwa siku njia ya Marangu kuna nyumba za kulala ni 60$kwa siku lemosho inaweza kuwa 30-40$ kwa siku minimum park fee kwa siku 7 ni 35$ × 7 =245

- garama za hoteli siku unapofika moshi kutokea kwako labda morogoro, tanga, mwanza ... Ni juu yao.

- ukirudi mlimani wanakupa malazi kwa siku moja tena kesho yake ndio mkataba unaisha.

Malipo ya tour guide nilisahau na wale wenye vitengo.

Kwa kawaida bei ya kupanda mlima kilimanjaro ni wastani wa kuanzia 2000$ - 3500$ hapo ndio utapata huduma zenye ubora kidogo.

Kampuni nzuri za kupanda mlima Kilimanjaro zinacharge kuanzia 7500-15000$ kwa mtalii 1 hizo ndio kampuni za uhakika zenye kutoa huduma za dharura za kuaminika ikiwemo ndege ya kukubeba na kukuwahisha hospitali ya karibu ndani na nje ya Tanzania.

Kupanda mlima Everest garama zake ni kuanzia 25,000$ mpaka 150,000$ ambazo ni sawa na 60m - 300+ million kwa siku 18- 60. Sio lelemama kabisa.
Kuna kujiandaa kimwili na kisaikolojia...Niishie hapa kupata consultancy kutoka kwangu ya maandalizi ya kupanda milima mirefu ni 60$ kwa saa 1.

Hata hivyo utalii kwa Tanzania kiujumla garama zake zipo juu ukilinganisha na nchi kama Africa kusini, Morocco, Congo na Misri ambazo zinapokea watalii wengi kuliko Tz. Park fees za Tz ni nyingi sana na kuna baadhi ya maeneo yana geti mbili au zaidi kwa kivutio kimoja. Pia watu kuuzia watalii bei juu sana kitu cha buku mtalii anauziwa dola 5-10 ambayo ni zaidi ya 25k sio poa.
 
Hiyo ni dola ngapi umaskini mbaya sana. We hujui maana ya utalii. Acha ushamba na kuendekeza umaskini. We ni wa kulalamika kila kitu siyo?
Hii gharama lazima ziangaliwe Upya na hapa eti ni bei ya ofa.

Hivi wanaopanga hizi Bei Huwa wanalenga kumkomoa nani?

Kwamba Tanzania itafikiaha watalii mil.5 Kwa gharama za Juu kiasi hiki?

Hawa watu wa huko Serikalini Huwa wanafikifia sawa sawa kweli? Mtalii gani atakuja Tanzania harafu aje kurudi Kwa gharama za hivi?

Nyie watu wa Utalii lazima muwe na akili za kujiongeza ,faida na mapato ya Utalii sio kuishia tuu kulipa hizo tozo,inatakiwa mtalii alipe bei nafuu huko harafu sehemu ya pesa aingie shopping lakini Kwa gharama hizi automatically watakimbilia Nchi jirani. Punguzeni gharama,Utalii ni biashara ya Ushindani.

======
"Gharama ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa njia ya Lemosho kwa ofa iliyotolewa na Mamlaka ya Hifadhi kusheheherekea miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika ni Tshs Mil. Moja na Laki Saba"

"Kwenye hii gharama inakulipia hotel na chakula kuanzia Siku unafika katika Mji wa Moshi. Inakulipia usafiri wa kukutoa katika hotel hadi kwenye lango la Mlima. Inagharamia chaji zote za Hifadhini.

"Watu watakaokusaidia kupanda Mlima kuanzia wapagazi, wabeba mizigo, wapishi na waongoza Watalii" Joel Siao, muongoza watalii kutoka, African Scenic Safaris.
,
 
Kama huduma zitolewazo ni nzuri ni gharama za kawaida hizo kwa mtu alijipanga kufanya utalii.
 
Dah mngesemaga mnataka kwenda tungewasaidia muende kwa bei nzuri tu kipindi watu wanafanya kazi kwenye makampuni ya tours
 
Back
Top Bottom