Ikungi, Singida: Gari la mbunge Lucy Magereri(CHADEMA) lapata ajali. Dereva apoteza maisha!

Nashauri serikali iwahakiki madereva wa hizi fuso, ukweli ni kwamba wengi ni vijana na wapo rough sana barabarani, mimi hua siwatofautishi na dereva wa hizi bodaboda
 
RIP dereva! Chanzo cha ajali nini
Gari la mbunge wa CHADEMA Lucy Magereri lenye namba za usajili T348 CSR limepata ajali eneo la Issuna wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambapo Dereva aliyefahamika kwa jina la Thomas Maro, amepoteza maisha papo hapo.


Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Fuso kuendesha gari upande ambao sio wake, na sasa amekamatwa yupo kituo cha Polisi kwa ajili ya mahojiano.

View attachment 830936
 
yaani unavyo sema utadhani kweli
nikudanganye nini mtoto mzuri? jongea karibu yangu upate nuru kama marumaru za ikulu, nakuhakikishia hutajuta you are on the right truck hamisa na katu sitokuangusha katika penzi letu na ujenzi wa Tanzania mpya
 
Chadema madereva wengi wa Chama ni wachaga .Rejea hotuba ya Mwita Waitara kuhusu madai ya marehemu Chacha Wangwe ambaye alikuwa mchaga akaipindua gari ikamuua Chacha Wangwe halafu akaenda kufichwa Kenya .hadi leo Yule dreva hayuko Tanzania
Unakuwa muongo kuliko shetani mwenyewe au ndiye yeye au mwanae? Hivi unajua kuwa mkataba wa dereva wa Mbunge na Mbunge ni wa mbunge mwenyewe? halafu usije kuta wachaga wanapata ajira nyingi kutokana na utendaji wao uliotukuka tofauti na nyie kina YEHODAYA mliokalia majungu na fitina tuu. Wewe hata kukupa banda la kuku unitunzie siwezi maana waweza "kutafuna" kitoweo wakashindwa kutaga bure!
 
HII HABAR YA KIDUWANZ TU HAINA MASHIKO MBUNGE HAKUWEPO NA KWAN WABUNGE HUTUMIA RAV 4 AU LAND CRUISER
 
Hivi madereva wa Wabunge wa Chadema wote ni WACHAGA? Pumzika panapostahili Mh. Dereva.
Aliyekufa kwenye ajali ya Mheshimiwa Kigwangala ni Mwandishi wa habari naye alikuwa machaga, Mbona hujasema waandishi wote wa mawaziri ni wachaga? Acha Ukabila wa Kipumbavuuu mno
 
Pole sana jamani. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape afueni ya haraka majeruhi. Amina.
Meanwhile, wakuu JamiiForums nahisi kama nimedukuliwa. Tangu asubuhi siwezi kucreate any NEW thread. Tatizo ni nini?
 
Hizi Toyota zitatumaliza.

Kitakachotumaliza ni zile speed zisizo kuwa na limit kwa magari binafsi. Zile sheria ambao Duniani kote hawatakaa kutuiga.

Wa fusso mtamlaumu bure mwendokasi utatumaliza.
 
Back
Top Bottom