Ikulu yamjibu Dr. Slaa juu ya Rais Kikwete na Udini

Status
Not open for further replies.
JK mkamate ilunga,

halafu nashangaa mbona jk hatangazi kuwa mtu akikamatwa anauza CD za uchochezi ama lake?? kuna nini jk anaogopa??

mbona hamkamati ilunga?

Kwa kweli hata mie hapa ndio huwa sielewi kabisaa, nikijaribu kulinganisha ile video ya Lwaka na ya Ilunga ndio huwa ninapata kizunguzungu! sasa taratibu ninaweza kuamini post no.22 maana ukiconnect dot. ni kama ninapata jibu ingawaje sitaki kuamini kuwa post no.22 ni kweli kuwa Rais anaweza kufanya vikao na Ilunga...
 
Wakati mnasambaza zile message na zile nyaraka mlikuwa mnafikiria tu ushindi lakini mkasahau dhambi ya ubaguzi ina nguvu gani. Haya ni madhara ya dhambi ya ubaguzi ndo yanaanza kututafuna.
 
huyu aliyeandika hii taarifa ya ikulu anaimbia kikundi gani cha taarab, hizi ajira za kupeana zitatutia aibu mpaka lini? ikulu haiwezi kutoa tamko illogical kiasi hiki.
 
""Kwa hakika, hakuna namna nyingine ama namna bora
zaidi ya kuielezea kauli hii ya
Mheshimiwa Slaa isipokuwa
kwamba kauli hiyo ni
riwaya nyingine isiyokuwa na
mshiko.""


kumbe wanajua ni mheshimiwa Slaa??wanajua ndo rais halali wa tz kwani walimpora urais wake 2010
 
Kuongozwa na mtu aliyezoea kucheza na kuchezwa ngoma au kushinda ngomani, sasa haya ndio madhara yake. hii "barua" imejaa mistari ya taarabu tupu...

Kweli hii taarifa ilitoka kwenye dawati la mcheza ngoma/vigodoro.Aibu tupu hii halafu kuna mtu alikua amevaa suti ametundika na badge (bendera ya Tanzania) akisoma tamko la kipuuzi kabisa nadhani tangia tupate uhuru.Watu wanajua kutafuta fedheha kweli
 

Kauli ya Dr. Slaa haina afya kwa amani ya nchi hii. Kwa hiyo anataka kusema kwamba Rais alishinda kwa sababu aliomba kura misikitini? Kwa hiyo Rais alichaguliwa na waislamu? Hii si kauli njema kwa kiongozi mkuu wa chama na ambaye yeye mwenyewe si tu ni muumini wa dini bali kiongozi wa dhehebu la dini mojawapo

yeye anaonyesha kwamba tuhuma za CCM na Jakaya Kikwete kwamba vyama vya upinzani ni vya kidini si kweli kwa sababu waasisi ni CCM kwenye ilani yao lakini matamko ya yeye mwenyewe mwenyekiti na makada wake wote wanahusisha vyama vya CUF na Chadema na udini ndio kuanzisha na kuasisis udini
 
Hii ni kweli kabisa mh Kikwete alifanya siasa za udini na ushaidi upo wa kutosha kuthibitisha hili na tayari mh Lema ameshasema ushaidi huo anao na yuko tayari kuwaelezea wananchi kupitia vikao vya bunge vinavyoendelea sasa mjini Dodoma. Kwa kuwa nimepata bahati ya kuona Video CD hiyo ikionyesha kampeni za udini alizokuwa akifanya Rais kwa kushirikiana na Lipumba na shekh Ilunga wa Mwanza hivyo ninakiri kabisa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete alifanya kampeni za udini kuingia madarakani. Na hii itamgharimu kwa mambo yanayoendelea kwa sasa hapa nchini.

Ombi langu kwa kamanda Lema ni kwamba endapo Spika wa bunge atagoma kuruhusu mh Lema atoe ushahidi wake bungeni basi auweke katika mitandao ya kijamii pamoja na youtube ila kila mtu aweze kuona mambo aliyokuwa akiyafanya mh Rais.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Duh mbona mambo yanaingiliana. Ina maana CCM na CUF walishirikiana kupiga kampeni misikitini kwa ajili ya ushindi wa CCM? Lakini kama ni hivyo mbona Rais Kikwete alivyoshinda hakuwachukua Waislamu pekee ndio wawe wasaidizi wake. Naona Rais amezungwa na wasaidizi wengi tu ambao ni wakiristo kama alivyosema Prof. Mwandosya
 
Mzee huyu alishafilisika cku nyingi ki siasa na mwl nyerere aliwaona watu kama hawa toka.zamani kuwa watakapo kosa sera watatatuta maneno ya kuwaambia wananchi hata kama ni yA uwongo
 
Ha ha ha ha!!!Ndiyo Ikulu ilivyoshuka, Tamko la Ikulu bila hata saini kujua mamlaka ya aliyeitoa! Tanzania umekwisha! Hakuna uongozi na hakuna

1. Wakati wa Kampeni militia tahadhari na kukemea udini takriban kwenye mikutano yangu yote zaidi ya 300 Kati ya mikutano 471. Nilikemea kwa kuwa ninajua maana ya Udini. Sikulelewa katika utamaduni wa udini,wala wa ubaguzi. Raisi mstaafu Mwinyi ni Mwislamu, mbona hakuna anayemnyooshea vidole. Wanaomtetea Kikwete wanamponza.

2. Hakika hili limeninginia shingoni na hamuwezi kujikomboa wala kumwokoa Kikwete kwa kuwa mnamdanganya kila siku na kila wakati. Kataeni wakati Kampeni zinaanza Kikwete hamkumwandalia kwenye hotel ya Ufukweni? Kama mlikuwa na nia njema kwanini hamkuwaita wadau wote!

3. Kidogo tu kabla ya uchaguzi hamkutumia vijana wa usalama wa Taifa kupitia viongozi wa Dini. Bisheni tuwashushie ushahidi. Tukinyamaza msifikiri hatujui. Mahitaji ajibu Kikwete kwani yaliyofanyika yalikuwa na Baraka zake.

4. baadhi ya masheikh kupita nchi nzima kuwashawishi waislamu. Tena uamuzi ulifanyika ndani ya Ikulu yetu, na wakatumwa kwa Kodi ya Watanzania. Kataeni tuwaache uchi. Usichezee mto uliotulia. Tumefika mahali hatuwezi kuwanyamazia tena!

5.NATO Challenge kwa Serikali, Ikulu, Usalama waweke hadharani ushahidi wa Dr Slaa kufanya Kampeni kupitia Kanisa lolote! To a ushuhuda nimepita Kanisa gani, tulifanya mkutano na askofu gani au na wachungaji Gani.
 
Ha ha ha ha!!!Ndiyo Ikulu ilivyoshuka, Tamko la Ikulu bila hata saini kujua mamlaka ya aliyeitoa! Tanzania umekwisha! Hakuna uongozi na hakuna Raisi..
[/QUOTE]
Dr.W.Slaa Shukurani kwa kuja na kutoa ufafanuzi. Naona ninyi wapiga kampeni wa mwaka 2010 mnajuana vyema na mnafahamu mlitumia mbinu gani. Manake hawa wanasema tuna ushahidi na hawa pia wanasema tuna ushahidi. Tusubiri tu siku kia mtu atakapotoa ushahidi dhidi ya mwenzake ndipo tutajua nani ni nani katika kutuharibia nchi yetu. Jambo moja ambalo siijui lilitokea kwa bahati mbaya ama makusudi kwamba minong'ono ya Udini ilianza kusikika kwa kwa kasi mwaka 2010 wakati wewe ukiwa mgombea wa CHADEMA, sijafahamu hasa kwa nini kipindi hiki na wala si huko nyuma kabla hujagombea wewe au ni kwa sababu ya historia yako? Kulala Mission nadhani si suala la kidini kwani hata Mkapa alikuwa akilala mission lakini hatukusikia tetesi za udini.

Hapo kwenye wekundu, vipi umerudi tena kwenye msimamo wako kwamba nchi haina Rais?
 
Last edited by a moderator:
Hili mbona tamko mbona limesimama?, yani hapa mzee Yusuph mwenyewe aliandika mistari,kurugenzi yamawasiliano ikulu wakaweka muhuri na sahihi tuu. Kitu ni tamko la ikulu kuhusu watu wanaomchafua mama salma kwa kumuhusisha na umiliki wa home shopping center...... Tafuta hili tamko ndio utajua kweli hii kurugenzi inajua taarabu. Bora hata huyo nepi wa lumumba



Kusema kweli hata mimi nimelisoma hilo tamko sikuamini kama limetolewa na watu ambao wamebobea kwenye tasnia ya Habari kama Rweyemamu. Ni tamko jepesi na lenye maneno ambayo hayaonyeshi kwamba linatoka ofisi kuu ya nchi hii ambayo ina Mamlaka. Maneno kama santuri sijui kama yana mantiki. Na pia kumwita Dr. Slaa Mheshimiwa sijui kama ni sahihi. Hivi viongozi wa vyama ambao si wabunge nao ni waheshimiwa kwa mujibu wa sheria?
 
Dr.W.Slaa Shukurani kwa kuja na kutoa ufafanuzi. Naona ninyi wapiga kampeni wa mwaka 2010 mnajuana vyema na mnafahamu mlitumia mbinu gani. Manake hawa wanasema tuna ushahidi na hawa pia wanasema tuna ushahidi. Tusubiri tu siku kia mtu atakapotoa ushahidi dhidi ya mwenzake ndipo tutajua nani ni nani katika kutuharibia nchi yetu. Jambo moja ambalo siijui lilitokea kwa bahati mbaya ama makusudi kwamba minong'ono ya Udini ilianza kusikika kwa kwa kasi mwaka 2010 wakati wewe ukiwa mgombea wa CHADEMA, sijafahamu hasa kwa nini kipindi hiki na wala si huko nyuma kabla hujagombea wewe au ni kwa sababu ya historia yako? Kulala Mission nadhani si suala la kidini kwani hata Mkapa alikuwa akilala mission lakini hatukusikia tetesi za udini.

Hapo kwenye wekundu, vipi umerudi tena kwenye msimamo wako kwamba nchi haina Rais?[/QUOTE]

kwa taarifa yako JK 2010 aliona anashinda bila kigugumizi. Baada ya kusikia Dr Slaa atagombea kupitia CDM aliogopa sana, kumbuka hotuba aliyotoa pale Lumumba kuhusu kutumia silaha mbali mbali kama combania n.k. Silaha pekee ya kikwete ilikuwa udini ingawa ilishindwa akaamua kuiba kura
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom