Ikulu yageuka ukumbi wa sherehe mbalimbali!

regam

JF-Expert Member
Jan 4, 2011
269
51
Jamani wana jf inakera saaaana! Kuna tetesi kuwa eti sherehe za kutimiza miaka 50 ya UDSM zikiambatana na uchangiaji wa student center zitafanyika ikulu mwishoni mwa mwezi huu wa kwanza. Inasemekana wageni waalikwa ni walewale wafisadi papa wanaoitafuna nchi hii km RA, EL,na wafanyabiashara maarufu hapa tanzania. Cha kujiuliza ni kwamba, hii sherehe ni ya chuo kikuu, kwa nini isingefanyika hapo chuo halafu wao na huyo jeykei akaalikwa? Nafananisha na ukumbi wa sherehe kwani tangu mwaka uanze ikulu imekuwa booked ile mbaya! Bethdei, etc.
Wenye data zaidi changieni.
 
ni kweli Reagam sasa hivi kila sherehe ni Ikulu mpaka Birthday tunaziona kwa sasa usishangai jamaa akija kujitangazia ni Rais wa maisha!yaani kila kitu kwake ni easy tu!anatake simple
 
sure kaka eti first lady anasherekea mwaka mpya tarehe 14 january tena ikulu na wake za mabalozi kwanini asingeenda kusheherekea na watoto yatima au makundi mengine yasiyojiweza?!
 
Kula bata kwa kwenda mbele kama wanabembea vile. 150001_154388677939262_100001043926248_283431_7927141_n.jpg
 
mungu awape nini waswahili hao kutoka bagamoyo na mkuranga sijui lindi....typical.
 
Ikulu haina hazi tena kama enzi za Nyerere/Mkapa, Saizi imekua kama Kasino Fulani.
 
ni kawaida kwa mswahili akipata atataka kila mtu ajue kapata na kujua kanunua nini au ana kitu gani kipya.habari ndio hiyo bado sherehe 2000 hadi amalize miaka iliosalia.kuna kumbukumbu ya harusi, kupata mjuku, kuongeza mke nk nk nk nkkkkkkkkk
 
Jamani wana jf inakera saaaana! Kuna tetesi kuwa eti sherehe za kutimiza miaka 50 ya UDSM zikiambatana na uchangiaji wa student center zitafanyika ikulu mwishoni mwa mwezi huu wa kwanza. Inasemekana wageni waalikwa ni walewale wafisadi papa wanaoitafuna nchi hii km RA, EL,na wafanyabiashara maarufu hapa tanzania. Cha kujiuliza ni kwamba, hii sherehe ni ya chuo kikuu, kwa nini isingefanyika hapo chuo halafu wao na huyo jeykei akaalikwa? Nafananisha na ukumbi wa sherehe kwani tangu mwaka uanze ikulu imekuwa booked ile mbaya! Bethdei, etc.
Wenye data zaidi changieni.

Sasa ulitaka ifanyike wapi? na hiyo ni heshima kutoka kwa mtawala wako.
 
naona ikulu imekuwa ni venue ambayo imechukua nafasi ya Diamond Jubilee Hall(s). Watuambie ni kiasi gani kukodi ilibiashara ianze rasmi!
 
Ikulu haina hazi tena kama enzi za Nyerere/Mkapa, Saizi imekua kama Kasino Fulani.

Hivi Ikulu mnafikiria ni kitu gani? acheni ushamba,

tunacho pinga ikulu ni kutumia adress kufanyia ufisadi kama alivyotumia Benjamin Mkapa na Mkewe, ile ni office kama office nyingine za kazi
 
Back
Top Bottom