IKULU: Waziri Mkuu Mstaafu, Lowassa amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli; akiri Rais anafanya kazi nzuri

Ameenda kushkuru kwa babu seya kuachiwa huru maana ilikuwa ni moja ya agenda zake 2015
 
Cha ajabu ni kipi? Mbona kina mbowe walienda ikulu kumwona kikwete ilhali bunge ni walikuwa wanamwita dhaifu? Mbona hakukuwa na ganzi ila leo kuna watu mnaleta ganzi? Mav ya kuku...Lowasa anajua anachokifanya siyo kurudi ccm
Slaa alipigwa mabomu pale Arusha akajiapiza kuhusu Kikwete lakini ilipofikia hatua ili mambo yaende ilibidi aende ikulu. Kama siyo roho ngumu za kina Sitta leo tungekuwa na katiba inayohoji matokeo ya urais mahakamani. Ilifikia hatua mambo yote muhimu yalikuwa yakifanyika ikulu kati ya Chadema na Kikwete. Hadi CCM wakaanza kumuomba Kikwete awakatae maana walajua watapoteza. Lissu alifikia hatua akasifu sehemu Kikwete alipowasikiliza. Ukidinda na yeye akadinda mtaishia kwenye vurugu tu!
 
Labda kama hiyo habari ya kupongeza imeandikwa nusu nusu, na kwanini iandikwe nusu nusu Mkuu? Kwanini wasitupe kitu kizima kilichozungumzwa bila kuficha lolote lile?
haaaa kila taarifa ingeletwa yote taarifa ya habari ITV ingeeza saa mbili mpaka jioni saa mbili
 
Chadema acheni kumnanga Ndugu Lowassa

Lowassa aliombwa na Chadema kuja kugombea Urais sio Yeye ndio aliomba

Aliwasaidia kugombea Urais yapaswa mumshukuru sana
 
Mkuu naungana na wewe, kuna kila dalili yale maandalizi ya leo yalikuwa ya kumpokea Lowasa inawezekana Lowasa hakulizishwa na venue ya Pugu check point siyo level yake akawachenjia gia angani wakaenda kunywa juice na Magufuli Ikulu.

Mbowe ameifanyia makubwa Chadema , lakini kwa heshima na taadhima hili jahazi kwa sasa akabidhiwe Tundu Lisu Mbowe arudi kwenye nafasi yake ya zamani ya ukatibu mkuu.

Anayeziweza siasa za utawala huu ni Tundu Lisu peke yake ndio mwenye sifa ya kuwa mwenyekiti wa Chadema ili kupambana na huu mfumo dollar.

Wanasiasa wafanyabishara msiwaamini hata siku moja, Tundu Lisu hana cha kupoteza serikali ikimkamia, lakini Mbowe serikali ikimkamia ana vingi vya kupoteza na isitoshe hakuna mfanyabiashara msafi kwa 100% ukimpekenyuwa vizuri lazima ana makandokando yake na ndio hayohayo serikali inayatumia kukupiga speed gavana. Mbowe aachie uenyekiti kwa hiyari au aondolewe kwa nguvu.

New reform inahitajika Chadema, kna meya Jacob Boniface ndio watu wa kupewa vyeo kwa sasa, vivuli kama kina Mnyika vyote hivi ni vya kusafisha vikae pembeni waingie watu serious kwa ajili ya mapambano.

Huu ndio ushauri wa kuinusuru Chadema.

Mkuu siongezi chochote kwenye maelezo yako. Nimeshaongea sana kuhusu ukomo wa Mbowe kwa sasa ndani ya cdm. Tunaheshimu mchango wake, lakini ni vyema apumzike.
 
Back
Top Bottom